Nilivyonusurika kuchomwa moto nikiwa dukani usiku wa saa 9 South Africa

Nilivyonusurika kuchomwa moto nikiwa dukani usiku wa saa 9 South Africa

Habari zenu wakuu

Nianze moja kwa moja na hili tukio

. Duka nililokuwa nafanya kazi lilivyo

Limmeunganika na chumba cha kulala, alaf mlango wa kutokea ni mmoja tu huo huo ni wa kuingilia dukani wa wateja

Usiku wa saa tisa nikiwa kwenye usingizi mkali sana nikiwa chumba hicho kilichokuwa hapo dukani kwetu, nilihisi kama naota lakini ilikuwa kweli , nilisikia sauti kama za kuteketea kwa kitu kikavu kwa moto, walikuwa wamemwagia petrol sehemu ya mlango wa duka na kuwasha moto

Kwa sisi wageni kulala SA ni kwa mitego tu ukilala fofofo, unaweza ukafa mda wowote kwa ilee mentality waliokuwa nayo wazawa juu ya sisi wageni.. kuwa tunawachukulia fursa zao

Nikaamka faster, nikaona moshi mkali sana so nawahi mlangoni naona moto ndio unapamba, nikawahi kuuzima na nikafanikiwa baada ya kupambana kama dk 15 hivi, niliuwahi na blanket/jovet kwa kuufunika ukizima natoa blanket nawahi sehemu ingine , ilikuwa hivyo na ulivyokuwa unakubali kuzimika nikachukua maji niliyokuwa nimehifadhi ndani kama ya kunywa kwenye ndoo na kuunyunyizia na ukazimika mazima, maji nilikuwa nayo kidogo sana kama nusu ndoo, nishukuru zilee blanket/jovet kwa kunisaidia kuuzima ule moto hiyo ni saa 9 usiku.. ashukuriwe M/Mungu, M/Mungu ni mwema sana

Kitu kibaya zaidi duka limetengenezwa na mbao then limezunguushiwa na bati, duka/jengo kubwa sana , vuta hisia mbao zikikubali moto

Alaf hawakuja kuchoma duka langu peke yake, mtaa wa nyuma yangu, siku na saa hiyo hiyo nachomewa mimi walianza kwenye duka hilo la nyuma yangu aisee, duka limeungua lote, wafanyakazi wa duka walikuja kuokolewa na fire-gari la kuzima moto

Baada ya kufanikiwa kuzima moto dukani, wakaja askari-low forcement na gari lao, wakaniuliza nini? Kimetokea nikawaelezea kuwa nimeamshwa na mitetemo ya moto so sijui nini? Kimetokea na nimefanikiwa kuzima moto, wao wa kanambia niache milango wazi mpaka hasubuhi na wakanambia kuna duka lingine mtaa wa nyumba limezuka moto nalo so fire-zimamoto wanapambana kuzima moto

Mda huo nasikia ving’ora vya gari la kuzima moto-fire .. vinaelekea kusaidia kuzima moto duka jirani

Mara nikaanza kupokea simu kutoka kwa watanzania wenzangu kuuliza kuwa wamesikia kuna maduka yamechomwa moto je? Duka ambalo nafanyakazi ni mojawapo! Nikawajibu na kupokea pole ila niliwaambia M/Mungu mwema nilifanikiwa kuuzibiti moto so sijapata madhara makubwa

Kisa ilikuwa manamba namba/watemi wanataka pesa kila mwezi kwa kila duka , pesa isiyopungua r1500 kama pesa ya ulinzi kwa madai wanalinda maduka kwenye kitongoji hicho, wamiliki wamaduka walikataa sababu kila baada ya mda maduka yanavamiwa na kupora pesa na hata kuuliwa wafanyakazi wa madukani, watemi wakaamua kuja na hiyo inshu ya kuchoma maduka, walifanikiwa kuchoma maduka mengi sana na kama hauna mtaji wa kutosha au hakiba biashara yako ndio inakuwa imekufa kwa mtindo huo

Na hata kusikia kuwa maduka yanachomwa moto, mabosi hawajali kuhusu sisi wafanyakazi wao, kikubwa anakulipa tu kwa mwezi yeye anaona sawa tu hata uhatarishe maisha yako kwa kulala dukani, wakati kila usiku lazima duka moja au mawili yateketee kwa moto na watu wakiiwa ndani

Story ni ndefu sana
Kilichonifanya nikubali kazi ya duka ni kukataa kazi ya kuuza drugs/madawa, maana south africa ukiuza madawa ndio utakuwa na pesa za kutosha, binafs nilikataa kazi za madawa kwa kuwa siwezi nikakubali kumuuzia mwenzangu sumu kitendo hicho hicho sitakubali afanyiwe ndugu yangu, rafiki yangu au jamaa yangu so nimeona bora nisishughulike na hizo mambo

Sipendi hii habari/tukio maelezo yawe marefu ila matukio ni mengi sana yakiyonikuta nikiwa south africa

Now nipo Tanzania Nina miezi 5, kama ikifanikiwa kupata nchi ya kusafiri nitasafiri lakini sio south africa.

Ila tanzania hali mbaya sana wakuu labda kwa kuwa mimi nimekuwa mgeni hapa nyumbani nafikiri nitazoea tu kadri ninavyokaa.

Asanteni
Watu wa SA wamesahau mara moja kwamba sisi tuliwasaidia mno kupata uhuru. Kweli maskini akipata matako hulia mbwaaa!
 
Watu wa SA wamesahau mara moja kwamba sisi tuliwasaidia mno kupata uhuru. Kweli maskini akipata matako hulia mbwaaa!
Kiuhalisia watu wa south africa, wanatupenda sana Watanzania ila ikifika maswala hayo ya kudai kuwa tunawachukulia fursa, hawaangalii yeyote wanakudhuru one time.. sio binaadamu kabsa

Nipo tanzania katika vugu vugu hili la kufukuza wageni nimeona imepostiwa picha ya jamaa mtanzania kachomwa moto na mwanamke wake wa kisouth.. mpaka wamekufa wakiwa ndani

Roho imeniuma sana nikakumbuka sana ilee siku nachomewa moto duka nikajisemea moyoni kuwa sio mzaha, wangeniua kweli walee jamaa

Hata hivyo wangeniua mda tu, nikiwa dukani nimekoswa koswa na pistor.. sio watu walee
 
Kihalisia watu wa south africa, wanatupenda sana Watanzania ila ikifika maswala hayo ya kudai kuwa tunawachukulia fursa, hawaangalii yeyote wanakudhuru one time.. sio binaadamu kabsa

Nipo tanzania katika vugu vugu hili la kufukuza wageni nimeona imepostiwa picha ya jamaa mtanzania kachomwa moto na mwanamke wake wa kisouth..

Roho imeniuma sana nikakumbuka sana ilee siku nachomewa moto duka nikajisemea moyoni kuwa sio mzaha, wangeniua kweli walee jamaa

Jata hivyo wangeniua mda tu, nikiwa dukani nimekoswa koswa na pistor.. sio watu walee
Mpaka sasa ubalozi imekiri wabongo 90 wapo polisi kuhis hii inshu ya wasouth na wageni
 
Mpaka sasa ubalozi imekiri wabongo 90 wapo polisi kuhis hii inshu ya wasouth na wageni
Serikali ilibidi iseme chochote kama kujali kuhusu raia wao waliopo huko

Sio wote hawana vibali, wengine wengi wanaoshi kwa vibali so ilibidi itoe muongozo wa kauli kuhusu raia wake waliopo huko

Nimependa sana serikali ya Ghana na Nigeria
 
Tofauti na mambo ya kuuana uana, chuki za kufukuzana, kuchomana moto

Jamaa wanauchumi mzuri sana ndio maana wageni wanaenda na wapo kwa wingi huko, fursa nyingi , wenyeji hawafanyi kila kazi huko so wageni wanazifanya na zina pesa nyingi sana

Unaweza ukawa mfanya kazi tu wa duka ila mshahara wako ukawa sawa na mfanyakazi wa serikalini Tanzania
 
Back
Top Bottom