Nilivyonusurika kufa: Niliingia na kujinasua katika kundi hatari la uhalifu

Nilivyonusurika kufa: Niliingia na kujinasua katika kundi hatari la uhalifu

Ikiisha mniite wakuu. Sitaki alosto
Habari zenu wakuu, True story!!

Sikuwahi kufikiria kuwa siku moja ningeweza kujikuta katikati ya mchezo hatari uliopangwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Ilianza kama jambo la kawaida tu — ofa ya kuvutia na ahadi za mafanikio ya haraka.

Lakini kadri nilivyozidi kujihusisha, nilitambua kuwa nilikuwa nikiingia kwenye mtego wa kundi la matapeli wenye ujuzi wa hatari.

Huu ni ushuhuda wa jinsi nilivyokabiliana na hofu, kuchukua hatua ya ujasiri, na hatimaye kujinasua kutoka mikononi mwa kikundi hiki hatari.

Mimi Ibn Unuq baada ya kumaliza chuo cha NIT, Dar-es-salaam nilirudi nyumbani MBEYA, ili kutulia kusubiria ajira huku nikiangalia nifanye nini wakati huo.

Binafsi mimi ni kijana mtaratibu sana, ninafanya mambo yangu kwa utaratibu na utulivu, sina papara wala hofu, Sio muongeaji sana - mimi ni mkimya mno ila ninapenda kuandika - ni mchangamfu sana kwenye maandishi.

Ninavutiwa na matendo zaidi kuliko maneno - action oriented. Ukiniambia well done nakua proud sana kuliko ukiniambia Well said.

Sipendi sauti kubwa iwe mtu anazungumza kwa kelele ama mziki mkubwa unapigwa [kichwa hunigonga sana] hivyo huwezi kunikuta kwenye sherehe au club yeyote au vibanda umiza.

Hua nakua comfortable sana ninapokua pekee yangu - nikikaa na watu wawili au watatu baada ya muda kidogo najihisi siko comfortable kabisa - naondoka, Hata shemeji yenu anajua kuna muda hua nataka tu kua pekee yangu, ila sasa ukinikuta kwenye mood hua napiga story kama OKOT P' BITEK.

Kukaa tu pekee yangu ikawa inakua boring hivyo nikawa nautumia muda wa peke yangu kucheki movie [Napenda movie zinazotisha sana], pia kusikiliza muziki [Hiphop], kusoma vitabu na articles tofauti tofauti - na hapa ndipo niliijua "JF", Nikajifunza meditation toka kwa Mshana Jr, hivyo nikaongeza jingine la kufanya ninapokua pekee yangu pia hua ninatumia alone time kufanya mazoezi na huyu ni mimi kwasasa Ibn Unuq. View attachment 3178603

Kuna bro mmoja jirani yetu Jimmy alikua anavutiwa na mimi akaniomba tuwe tunakimbia wote asubuhi.

Tukawa marafiki sana, akanifundisha kuendesha pikipiki yake aliyokua akiitumia kutembelea tu , hii ikanifungulia fursa, nikajitoa mhanga nikachukua pikipiki ya kupeleka pesa kwa siku, shilingi elfu7 kipindi hicho "Deiwaka'.

Kutokana na muonekano pamoja na usafi nilikua napata wateja wengi sana kwa siku - watu mchanganyiko.

Siku moja nilimpakia jamaa mmoja pale Soweto alikua anaenda Uyole, bhasi kwakua mimi sio muongeaji tulitembea kimya kimya mpaka tunafika, nilichovutiwa na huyu jamaa, yeye pia hakuongea chochote - tofauti na wateja wengine wao huvunja ukimya.

Aliposhuka akaniuliza "dogo mbavu, unakula chuma?" Nkamwambia yaah!! Akaniuliza bodaboda inalipa nikamwambia kiasi chake, Akasema amependa Confidence yangu, kuna dili la pesa ndefu anataka kunipa, nkamwambia sawa nipe namba tutaongea, Tukaachana!!

Nikampotezea tu, ikapita kama miezi mitatu hivi boss wangu wa ile pikipiki sijui kilimkuta nini, akasema anataka kuiuza, ana Emergency, Sasa mimi sio mtu wa Ku-beg beg, nikairudisha muda huo huo, nikamshukuru tu kwa kunisaidia mana kwa muda huu nilishapanga hadi ghetto langu tayari, nikarudi ghetto.

Nikawa nawaza nitafute boss mwingine, katika kufikiri nikamkumbuka yule jamaa wa dili la pesa ndefu, nikajiambia "Liwalo na liwe, nikamchekii".

Nilidhani nitatumia nguvu kubwa kumkumbusha, lakini nilivyomwambia mimi fulani akasema nakukumbuka, uko tayari? Nkasema ndiyo, akasema ntakupigia simu muda wowote nikupe maelekezo.

Ikapita kama siku 2, Jamaa akanicheki akaniambia saa1 usiku atanicheki anipe maelekezo.

Hawa jamaa wanamanage time aisee, Saa1 kamili simu ikalia, jamaa akaniambia niende mtaa wa Isyesye karibu na uwanja unaojaa maji, nkakodi boda chap - ningeweza kumuomba mshkaji wangu yeyote anisogeze lakini angeanza kuniuliza uliza nataka nikafanye nini?

Nilivyofika nikampigia simu, akaniuliza, unaiona hiyo pikipiki uwanjani, ifuate. Nikamwambia naiona Boxer BM150 akasema ichukue, Ina mafuta full Tank, nipitie hapa Nane nane getini, tuna safari ya Igawa, Nilitamani kuuliza ila nilivuokumbuka tunaenda wote nikajikaza nikaiwasha.

Ilikua ni boxer gear4 Mpyaaah!! ina funguo na Chest cover yake na Groves za kuendeshea, nlishtuka.

Kweli nikamkuta, akapanda, Jamaa akaniambia nijitahidi kuitembeza kadiri niwezavyo.

Sikuwahi tembeza chuma kama siku ile, Niljitahidi kutembea ila niliishia kutumia saa1 na madakika kufika igawa- kila utaponikuta mimi Ibn Unuq lazima niwe na stop watch, sababu ninapenda sana kuhesabu muda.

Mfano niwaibie siri, Mimi hua ninatumia dakika 7 sec 32 kwa round ya kwanza 🛏️, mzabzab unaweza hii 🤣🤣.


Tufocus na Story sasa;


Tukaingia njia ya porini sana, jamaa akanipa code nikiona gari, niwashe na kuzima taa mara4, Na mwenye gari inatakiwa awashe na kuzima mara5, huyo ndiye mwenzetu.

Tukafika sehemu tukaona gari Landcruiser prado kama hii 👇View attachment 3178623
iko mbele nikafanya vilevile na jamaa naye akawasha mara5 , tukapaki kuifuata.


Akauliza huyu ni begginer,Yule jamaa nlieenda nae akasema, dogo ana roho ya paka.

Tukaingia mlango wa nyuma wa ile cruiser, Aisee kulikua na jamaa wanne kila mmoja yuko busy na laptop yake - jamaa wa IT.

Mle ndani ya gari mlikua mmetapakaa laini za mitandao tofauti tofauti bado mpya kabisa zaidi ya 600.

Jamaa mmoja wa IT akasema wa makambako wameshafanikisha mission, Hivyo tuwahi haraka tukutane nao njiani, Akaniuliza unaweza kutumia hii, akawa amemulika taa kichakani nikaiona Pikipiki baja, nikasema naweza kuonyesha tu ubabe ila ukweli sikuwahi kuendesha baja, ikabidi niulize nisije nikapuyanga, hii ni gia ngapi? yule IT akasema tano, unapanga kama zingine tu.

Nikaiwasha, jamaa akapanda kama kawaida, unajua mi mrefu 5ft8, Hivyo Nilikua nayo comfortable sana, Sema kazi ilikua kila pikipiki nayokutana naya kuwasha taa mara4, nijibiwe mara5, maana nao walikua wanakuja na pikipiki.

Tukafanikiwa kukutana nao hata sijui ni wapi pale, hapo ni arround saa6 usiku, wakatugei bag ya mgongoni tukageuka tena kurudi igawa porini, jamaa akaingia na ile bag kwenye gari, Mi nkaambiwa nitulie nje, jamaa wako na muda kama dakika 10, jamaa yule akatoka akasema niwashe ile boxer, Turudi Mbeya.


Safari hii nilikua sina hofu tena, nilishajua nimeingia kwenye mchezo gani, ndani ya lisaa tukawa mbeya, Jamaa akasema nimuache uyole, hapohapo tukafunga na plate number halali, Jamaa akanipa laki4 na Elfu30 halafu akasema ile pikipiki nibaki nayo, nisiogope, niendelee kuzugia kama ndio kazi yangu, ila nikae mkao wa kula muda wote.

Nilitoka kwa hamu ili niwahi nikazipigie hesabu zile pesa ghetto, nilijiona tayari nina pikipiki boxer mpya na Pesa ya kutosha mfukoni, nikajiambia nikipiga dili5 hivi, nawakimbia naenda kuishi Dizim 🤣.

Bhasi nikashinda zangu nalala mpaka mida ya mchana, then nkaenda kijiweni kuzugia, jamaa wakaisifia sifia sana chuma, wengine wakajaribu kuiendesha, kwa Mbeya zilikua chache sana time hii.

Mi nikawambia nilipata boss mpya hivyo yule nimemrudishia chuma lake, Tena nikawaambia safari hii nimechukua mkataba kabisa.
[Mana Yule jamaa aliniambia siri ikivuja ni kifo].

Nikaendelea kuzunguka na yule jamaa sehemu tofauti tofauti, tukapiga kazi kama4 hivi [Nitaelezea zaidi siku nyingine- nazikumbuka zote hatarii sana].

Mimi kazi yangu ni udereva wa chap tuu, jamaa kazi yake kupokea tu pesa na mali tofauti usiku kwa usiku, Maana asubuhi inatakiwa tuwe mbeya, hakuna anayetakiwa kujua tulikua wapi usiku.

Na kwa kazi yangu ya bodaboda hata nikirudi saa7 usiku majirani wanajua kawaida tu, mana bodaboda wanakesha mpaka asubuhi, ndio maana hawa jamaa wanapenda kutumia madereva bodaboda.


Ila usiku plate number inabadilishwa, tunaweka fake.

Wahenga walisema za mwizi arobaini, Siku hiyo tukaingia porini bhana kama kawaida, tukafika mpaka chimbo la kupangia mikakati.

Wakati nakaribia nikawasha taa mara4 kama kawaida, ajabu Ile cruiser ikawasha mara3 badala ya mara5 tuliyoizoea.

Jamaa akasema kimenuka, wawashie tena, nikawasha tena mara4, , round hii akajibu vilevile tena mara3, Jamaa akaniambia tumejaa, Akili ikacheza, nikageuza chuma U-turn haraka, yani almanusra tuanguke.

Nilichomoka na Accelelator mtoni mpaka tairi ya mbele ikataka kuinuka.

PAAAH!! PAAH!!

Sikuwahi kusikia mlio wa risasi kwa ukaribu vilee, Niliishiwa nguvu, nikapoteza Controll, mimi na yule jamaa tukaenda chini na pikipiki yetu 😭.

Nitakuja kuimalizia hapa hapa wakuu, Tutafute pesa za halali, Lakini pia Hawa polisi tusiwachukulie poaa mazee, Nilinyooshwa.

Imeendelea post no323.
 
Inaendelea.........


Baada ya kwenda chini nikasikia sauti ikisema, Tulieni hivyo hivyo, Mimi nikajiambia liwalo na liwe, Nikafyatuka haraka haraka kwa kasi kuelekea upande wa porini, Daaaah!! Nikafanikiwa aisee.


Nikaanza kuona matumaini, mbali na maumivu ya kuanguka na pikipiki yaani nilikimbia siku ile nadhani HUSSEIN BOLT hajajua tu kwamba kuna mtaalami zaidi yake huku mtaani.


Nilikimbia napita chaka kwa chaka, nilifika sehemu moja nikaona ile mioto ya kuchoma shamba ndio unamalizikia malizikia, nikawaza kitu, nikavua koti, nikazitoa hela mfukoni mwa lile koti, nikaichukua simu yangu nikaiweka kwenye mfuko niliotoa pesa, kisha nikalitupia pale kwenye moto.


Kooti likapamba moto kama dakika mbili hivii PUUUUUH!! Nikajihakikishia ile ni simu imeshasambaratika.


Nikaendelea kutembea mwendo wa haraka sio mbio tena, sababu nilishajihakikishia niko sehemu salama, Mfukoni nilikua na Cash Laki1 na Elfu70, Nikatembea mpaka Igawa mjini kwa kupita chaka tu chaka, Ni parefu aisee, yaani kwa pikipiki tu nikiichapa Accelerator mtoni ni dakika24 kutoka Igawa mjini mpaka hapo chaka.


Igawa guest zilikua zinahesabika kipindi hicho, kwa haraka ni zisizozidi 8, Hivyo wazo la kwenda guest lilikua ni hatari kwangu, kama wangeamua kusaka Rum hadi Rum huenda ningedakwa.


Igawa bhana mimi nilikua na kademu pale, kalizalishwa na mhuni tu fundi ujenzi wa mbeya - infact alikatelekeza, Huyu mwanamke anaitwa Beatrice, alikua anauza mgahawa mmoja maarufu maarufu pale stand, Nilikadanganya mimi ni Mchuuzi wa mpunga.


Kalikua kamepangisha chumba nyuma ya kiwanda cha ku-pack mpunga pale, nikaona huko ndiko usalama wangu ulipo.


NGO! NGO! NGO!, Naniiiii..?


Ibn hapa, Mbona usiku sana, Saa8 kasoro hii, We nifungulie mama angu tutaongea. Nilikua nakahonga sana haka kamdada hivyo Ilikua ngumu kunikazia, Nikaingia. Mbona kama unachechemea, Mbona umechafuka hivyo, Usiku huu unatoka wapi?, Mbona sielewi jomoni...!! 😆.


Mimi ni mkimya na hapa nikawa sijui hata cha kujibu, nimekaa tu pembezoni mwa kitanda, kalikua kamepanga room1 that time.


Nikamwambia kwa utaratibu, Mama angu naomba nipumzike, Kilakitu ntakwambia asubuhi, Akaniambia sawa ila utoe hyoTrouser mana ni chafu sana before hujapanda kitandani, nikaitoa kisha nikalala upande wa pili kabisa huko, Nkawaacha ye na mwanae wamelala upande mwingine.


NB: Hii ndiyo siku pekee mimi Ibn Unuq kulala na mwanamke bila kufanya Chohote, Ndiyo siku ya kwanza na ya Mwisho. Wamakonde utawasikia wanakuuliza "We kuweza kwani?".


Asubuhi kulipokucha mjadala mzito kati ya Simba na Yanga ukaanzishwa, ikanibidi nibuni uongo, nikamdanganya nilipata ajali na pikipiki porini nikaanguka, nikapoteza fahamu, Nilipozinduka baada ya masaa kadhaa, nikawasha chombo haiwaki, nakaamua niipaki kichakani.


Polee baba angu? Mbona hukuniambia sasa jana ili nikusindikize zahanati. Nyooo..!! Ili niingie kirahisi mikononi mwa mamwela- niliwaza.


Nikamwambia mimi mbona niko sawa tu, kwanza ngoja niiwahi kabla hakujapambazuka vizuri, isije ikaibiwa, Niikokote hadi kijiweni kwako then niende zahanati [Navyozungumzia zahanati wanaoishi kijijini wanaelewa], nakumbuka nilijidai natoa Elfu20 nimpe, akakataa, nilifanya kusudi, nilijua tu atakataa.


Akili ikawaza au nikirudi tena mbeya nikachukue pesa nikimbilie Dar? maana ghetto nilikua nina akiba kama milioni 3 na laki mbili na elfu40, Nikasema yes Good plan!!


Nikadandia roli la mizigo mpaka mbeya - ningeweza kupanda basi sema mimi ni mtata tu. Nilifika Mbeya nikataka kupanda daladala nirudi ghettoni kufuata pesa, mmmh!! Nikawazaaaaaaaah!! nikaogopa huenda ile Pikipiki itanikamatisha, nikapata wazo la kwenda Machimbo - kyela, Hata sikufiria mara mbil, nikajiambia hizo pesa potelea mbali - kuliko kukamatwa. haraka haraka nikapanda gari ndogo zinazoenda Kyela direct.


Nilifanikiwa kufika chimbo.
Aisee Maisha ya chimbo acheni nyie, Huku nilinunua kiswaswadu kidogo nikasajili na laini mpya, Nilikaa chimbo miezi miwili tu umbo la mazoezi liliyeyuka mithili ya Theruji ya mlima kilimanjaro, Aisee laifu linichapa sana yaani hapa nilie kabisa 😭.


Sikumoja nilimsikia jamaa mmoja anajinadi kwamba bila uchawi hupati mali- na nikimuangalia jamaa anaokota mawe kweli kweli, nikajiambia liwalo na liwe, nikamfuata yule jamaa, nikamwambia nautaka huo uchawi, Huyu jamaa akaniambia, unauhakika nikamwambia Yaah!!, Akasema mganga wake yuko katumba, kama niko serious hata nauli atanilipia, nikamuuliza, hii Sura yangu wewe unaiona ni kama vile inachekesha au? 😂.


Eti wakuu hii sura inachekesha hii?
👇👇View attachment 3179387


Bhasi kweli tukafunga safari baada ya siku2 kupita, Tukaelekea kwa huyo mtaalamu, Akilini mwangu nikiwa nimejawa na Shauku ya kupata walau Milioni 50 nihamie Dar [Nilikua napenda kweli nirudi zangu kuishi hapo Dar moja kwa moja].


Siku ya nyuma yake kabla nilitembeza sululu pale chimbo kwa hasira ili nipate pesa ya kwenda kwa mganga. Nakumbuka siku ile nilipata Gram 2.4, nikaiuza, matumizi ya hovyo ya hapa na pale nikabakiwa kama na Laki1 na sitini hivi. Mimi Ibn Unuq ilikua fanya ufanyavyo, lazima nipate pesa ya kununulia Kijiti na Mbunye kilasiku. Bora pesa niipate hata kwa kupora tu sio nikose hivyo vitu viwili na tena bora nilale njaa ila sio nilale na Arostoo 😂.


Tulifika kwa mganga, nikaingia ndani nikimwacha yule jamaa nje, Nikamsimulia mganga mkasa wote - sikufikiri hata kwamba labda pengine nina deal na mtu anayenitafuta? Bhasi yule mganga "Mzee Mfwinyi" akaniuliza je, anipe dawa ya kuokota mawe chimbo au Tufute kesi? Sema kweli msomaji wewe hapa ungechagua nini? 😜


Vyoteee..!! Nikamjibu, ila nataka nirudi kwanza Mbeya baada ya hapo nitakuja tena kuchukua dawa ya chimbo. Akaniambia kwa sauti ya kukoroma "Iwe Munyamulume" yaani "Wewe ni jasiri", Akasema atanifanyia dawa ya vyote kwa pamoja. Akasema nikamtafutie kuku nyeusi ambayo haijaanza kutaga na Mayai Viza mawili- nkashtukaa, Navitoa wapi sasa? Nkamuuliza.

Mfwinyi akaniambia "Iwe Munyamulume, wengile tukupata", Sio kila kitu niwatafsirie bhana. Nikajiambia Liwalo na liwe, Tukatoka na yule jamaa kwenda kuvisaka.


Aisee wakuu duniani hapa kuna vitu vinashangaza sana. Hamuwezi amini kuna maduka mjini humu wanauza mayai viza, maji ya kuoshea maiti, Nazi mbovu na vingine vingi vya ajabu, Hata mimi nilishangaa. Halafu wauzaji maranyingi ni wale Jamaa wa Itikadi kali - sio hawa wakawaida, Unamkuta ameshika ile Lozari yao - nikumbusheni jina limenitoka, halafu kama anaihesabia kwa utaratibu sana kama wale Ma-master wa kichina wa Kung-fu. Sasa jichanganye kumchokonoa jamaa wa mtindo huu - Utaimba Kasongooo yeeyeee 🎵🎵, Nikavinunua.


Usiku majira ya saa6 hivi, Tukaelekea makaburini na mganga, Nikaambiwa nivue nguo zote, nibakie uchi wa mnyama, nilale juu ya kaburi kifudi fudi, aaaah nikagoma Aisee, naijua hiyo 😂.


Wakuu ni hivi mimi ni mgumu sana nikabakia na Bukta [Ni zile ambazo zilikua na Chupi ya V ndani, nyeupe, Ina matobo hivi - watoto wa 2000 tulieni 😆, nyie mmezikuta boxer] - akasema sawa hakitaharibika kitu, nikalala kifudifudi akaniambia nifumbe macho - nikafumba ila akili yote kwenye bukta - Yaani nikawa makini mno, kama nikihisi Bukta inashushwa tu, Nichomoke ndukiiii 🏃🏿‍♂️‍➡️,,,,,,,,


Akaongea maneno fulani kisha akasema nifumbue macho, akamshika yule kuku mithili anataka kunyofoa kichwa, akamng'ata shingo kwa meno ya mbela hadi vikatengana, daaah!! Kama ni kiongozi ilifaa aitwe Gadaffi kabisa, Unajua Mdomo wake baada ya kumng'ata yule kuku ukawa kama ule wa Art the crown yule jamaa wa kwenye Terrifier III - Nani kaicheki hii movie?


Akawa ananinyunyizia ile damu inayoruka ruka huku anaimba imba "Kasongoo yeeyee..." Huu ni mfano tu msije mkasema hii story ni Chai, wimbo wenyewe ulikua wa lugha isiyoeleweka, nakumbuka tu neno - "Ndaba".


Akaniambia niamke pale, nichukue yai moja moja nisemee yote nayotaka Yafutwe kuhusu ile kesi kisha nibamizie pale juu ya kaburi kila yai moja. Haikuishia hapo tukarudi kilingeni, huko nikatembezewa namba 11 karibu sehemu zote za mwili - rudia tena kusoma, nimesema karibu sehemu zote, sio sehemu zote za mwili, Maana waafrika mnavyojua kufukua makaburi, Heri yetu sisi wakenya 😆.


Baada ya pale nikasema sasa Ibn Unuq umepikwa umepikika, Rudi mbeya kawaonyeshe sasa. Bhasi asubuhi baada ya lile zoezi, nikachemshiwa maji yenye dawa na ndundami nikaenda kuyaoga, Nikaiweka ile elf15 kilingeni, nikaagana na mganga, nikamwambia jamaa yangu, mimi naenda mbeya mara moja kusalimia home, Then ndiyo nirudi kukimbiza chimbo, jamaa akasema hata yeye ana mission Mbeya ila atalala kwa demu wake Soweto.


Tukafika mbeya, tukaachana, mimi nikarudi zangu ghetto nikijiamini kwamba mimi ni Invisible.


Nilifika Ghetto majirani wananiuliza ulipotelea wapi, nikawaambia machimbo, kama kawaida mimi sio Muongeaji sana bhasi nikawa nafocus kuvunja kufuli la gheto maana nilipoteza funguo, Nikaingia, nikapitiliza kufunua kwanza godoro, Waoooh pesa zangu zote bado zipo - ilikua jumla Milioni3 na laki mbili na elfu40 nilizokusanya kwenye Mission Impossible.


Arostoooooo!! Usiniache na arostoooo!! 🎶
Baby, baby huuuuuuuu!! 🎶
Arostoooo usiniache na arosto🎶
Mamaa ma-Ex wangu nawadiss ......
.🎶


Ilikua ni sauti kubwa ya mziki toka kwenye spika za ghettoni, Nina mda mrefu sikusikiliza Hiphop, nilikua kwenye moment fulani ya raha vibaya mno nikawa nabadilisha badilisha tu ngoma huku nimejilaza kitandani.


Ibn - kwanini usiende dukani kununua chuma nyingine kama ile boxer- used, halafu tokea kijiweni waambie tu uliamua kuhamia kupiga mishe kyela sasa ndiyo umerudi, watachoongea au kulaumu chochote don't care, Wewe ndo Unju mwenyewe mbishi.


Haraka nikaamka, nikaenda kupanda daladala hadi Mwanjelwa kwa Big boy Motorcycle, Kilichonishangaza miezi mitatu tu ya mimi kutoka mbeya narudi Boxer BM150 zilikua zimetapakaa karibu kila sehemu mbeya mjini.


Milioni 1 na laki 7 bei ya mwisho- Ni Bigboy mwenyewe alikua ameniambia hii bei, Tulianzia milioni mbili kamili, Chuma ilikua bado mpya tu, Hii chuma niliilipia sababu ilikua inaendana vile vile na ile ya mwanzo, bhasi nikarudi zangu ghetto nikaweka Card ya pikipiki, nikapitia Lake oil pale nitatia Full Tank.


Break ya kwanza mtaa wa Forest kwa Bimkubwa, Huko Walinilaumu zaidi kwa kuwasusa bila kuwatembelea na kutopatikana, Unajua Ibn Unuq sio mtu wa kujitetea tetea, nikaomba msamaha yakaisha, Nilianza kuamini dawa inafanya kazi, mbona Bi- mdashi hajaongelea lolote kuhusu uhalifu.


Nikawaeleza kama nilivyojipanga kule ghetto ya kwamba nilihamia Kyela na pikipiki yangu, kule mambo yamekaza nimerudi, wakaelewa somo, nikamkatia Bi-mkubwa laki2- zikaanguka dua za kutosha palee, nikapiga zangu ndizi za kuchemsha na maziwa nikatembea zangu, nikarudi ghetto, nikamgongea jirani- "Jirani eeh! nilipoteza simu naomba nisaidie namba ya mwenye nyumba", akanipa.


Nilivyoongea na mwenye nyumba nikagundua pia hakuna jipya kuhusu ule msala mana alilaumu tu kwamba sipatikani, nikamwambia vilevile nilikua kyela, tukaagana nae.


Unajua nilikua nimelipa kodi ya nyumba miezi 6 na hapa nikawa bado nna miezi miwili ya juu, hivyo nikawa ni kama vile namsalimia tu, Nikajisemea moyoni Mganga ametisha.


Nikaingia soko la mwanjelwa, kuna pisi yangu ilikua inauza Macarpet, duka la Mkinga mmoja hivi anapesa chafu mbaya mbovu - tukapiga story nyingi za uongo, nikatoka hapo nikapitia sokoni upande wanaouza viatu kwa Rasi ngoda, nikanunua Travorta moja makini la kuendeshea pikipiki, huwezi amini lile Travorta, kuna jamaa nilimuuziaga bado analitumia mpaka leo, Hii sio chai, Liko kama hili hapa 😆👇View attachment 3179398


Nilipanga kwasasa iwe kazi kazi, saa11 nikajihimu kijiwe, nilikua mtu wa kwanza kufika, nikasogeza sogeza kama mtu mbili tatu hivi, Kidogo akaja jamaa naye bodaboda ila sura ngeni akaanza kunilolosa, umelipia hela ya hiki kijiwe_sebenza man!!, Nikamwambia dogo kwenu hakuna wakubwa? Akashuka akanifuata, Namimi nikashuka chap - Nilimchukua na hiyo ndonga apo juu, nikamwambia - Dogo sisi ndiyo waasisi wa kijiwe, Kwanza lete pesa ya mchango wa kijiwe.



Bahati nzuri akatokea mwanangu Lugano, akaamulia, Tukapeana tano za kuzidi maloloso ya kupigana kiutani, akaniuliza nilikua wapi nikampanga vile vile yaani kama kawa, kilichomfanya aamini ni kuniona na ile boxer. Hata yule jamaa niliyemlolosa akavutiwa na jinsi nilivyotaniana ki-fair na Lugano, Lugano akamwambia mimi na huyu mwamba ndio tulianzisha hiki kijiwe, inabidi jamaa nayeye umuandalie posho yake, Nikamwambia dogo niandalie tu Fifty, akasema sawa bro.


Siku hiyo kijiweni nililoloswa sana sababu umbo langu la kibabe lilipotea na Ile ndoga niliyoivaa waliicheka sana kama wewe ulivyoicheka 😆.


Nikapiga kazi wiki, mwezi, miezi miwili, hapa nilishaanza kwenda na Gym. Gym zenyewe ni zile za mtaani za ndoo kwa Mwanngu Chuma "Mbeya boy" - yule jamaa Freestyler, wale wafuatiliaji wa 10 za maangamizi mnamuelewa vizuri kazi yake.


Siku moja nimetoka zangu Loleza nikawa nimepata mchongo wa kupeleka box la viberiti na katoni ya sabuni kwa mpemba mmoja hivi.


Wakati wa kurudi nikaiona mark X nyeusi imepaki njiani, ikapigwa honi Ishara ya boda Njoooo!!, Nikavuka naendesha mdogo mdogo mpaka kwenye kioo cha gari, Kioo kikashushwa aiseee ni Mboka, Yule jamaa tuliyeanguka wote na pikipiki, mawazo yangu yote jamaa yuko jela, nikapanga gear namba1 kabisa, Jamaa akaniambia - usalama wako upo kwangu, ninajua unapoishi, kijiweni kwako hadi home kwa Mama ako, Chukua namba badae tuonane, Nikawa sina budi.


Nikakubali ila nilijiapiza sitamtafuta, ikapita siku mbili jamaa akaamua kuja pale pale kijiweni tena kwa mguu tu, akaniita ishara ya abiria mnavyoitaga boda kwa Ishara 🤞. Oyaah Ibn Unuq yule jamaa niliekwambia anakuulizia jana ndo yule pale, nikamfuata. Akaniambia dogo mbona hukunicheki, nakupa siku mbili ukishindwa kunicheki utanitambua mimi ni nani, Nilikukimbiza siku ile ukanipotea, Nikagundua kumbe jamaa nayeye alifanikiwa kukimbia.


Usiku nikamuandikia sms ndefu ya kutoa sababu za kwanini sitaki kuendelea kuwa naye, jamaa akanitumia sms fupi sana ya kikatili "Umechagua kifo", kuna mijitu mikatili aisee, Sasa msala si haupo, anikaushie tu - nilijiwazia kwa hasira sana. Aaah bwana eeeenh... liwalo na liwe bhanaa, nkaongea kwa sauti, ila nilikuwa nina wasiwasi na mashaka bado.


Nakumbuka ilikua jumanne-zikapita siku mbili Jumatano, Alhamisi, ijumaa hiyo tayari, eeh bhana eeeh!! sitakuja kuisahau ile Ijumaa.


Ninapokaa ni kitambo kidogo hadi kijiweni na sio makazi ya watu wengi, kama nilivyowaambia mimi napenda utulivu, ikawa inanilazimu niitembeze pikipiki kwa kasi kama dakika 15 hivi hadi kufika nane nane stand kijiweni, Aisee kuna gari nyeupe, Sijui ni Carina au MarkII ilikua inakuja mbele yangu kwa kasi nikajua wahuni tu wa mbeya, Aisee iliponikaribia nikakuta imaninyookea, ilinichota Mzima mzima nikapaa juu kama Super Hero, Nilikua BlackAdam kwa muda. Kumbuka namimi nilikua kibati - nikatua upande wa nyuma ya ile gari.



Nikashtuka tu nipo kitanda cha hospitali, Nimefungwa pingu mkono mmoja, nikawa nimeduwaa tu pale kwenye kitanda, sielewi elewi. Tena kuna Maaskari wawili wamesimama pembeni, Nikakaa kimya natafakari, Askari mmoja akatoka, mara namuona anarudi na Nurse, Nikamuuliza yule nurse nna mda gani akaniambia leo siku ya 4- akaniambia unajisikiaje kwasasa - nikajaribu kujitikisa nikaweza, nikasema niko vizuri, Nikamuuliza hawa maaskari je?


Askari mmoja akaniambia usiwe na wasiwasi upo chini ya mikono salama, bado nikawa nawaza, kidogo Bi-mdashi naye akaingia wodini pamoja dogo langu la kike, Toto la kinyakyusa.


Wakanifariji fariji, mama akasema raia mwema walichukua simu wakaona sms imeandikwa "DOGO NILIKWAMBIA UKIANZA KUFANYA KAZI NA SISI HAKUNA KURUDI NYUMA, TUNAKUMALIZA". Waka ripoti polisi, Nikajua sasa kumbe ndiyo maana nalindwa, nikajisemea kimoyomoyo sasa Liwalo na liwe.


Bahati nzuri sikuumia sana, unajua MarkII ama Ama Carina, bonet yake iko chini sana, Inapogongana na pikipiki ambayo ipo kwenye mwendo, Dereva ndiye utayeruka utaiacha pikipiki, Sasa Kuumia kutategemea jinsi ulivyotua, Upande wangu, Nashukuru nilitua vizuri.


Baada ya wiki nikaruhusiwa na nilikua naweza hata kutembea vizuri tu, Ila pingu mkononi, kituoni moja.


Nilianza kuhojiwa, kuhusu ile SMS, nikaulizwa ni nani niliokua nashirikiana nao? Na nilikua nafanya nao nini? Nikawa naleta majibu yaliyopinda pinda-Tumpeleke special room huyu. Hii mijamaa hata haijali kama sijapona vizuri daaah!! Sawa tu mazee 😭.


Siwezi waambia nilichofanywa humo- vitu vingine ni afadhali ibakie siri, Ukikamatwa ukajionee mwenyewe huko huko. Jamani polisi wanajua kupiga aisee. Yaani ubishi wote uliisha nikahadithia Full story A-Z.

Oya msije mkaona kama vile mimi ni mchumba tu, Onhoo!! Mtaingia siku kwenye 18- polisi sio poa nyie, Mi nashangaaga mnavyowachukulia chukulia poa, shauri yenu.


Nikasimamishwa mahakamani, nikasomewa makosa yangu:


1. Utapeli wa pesa za mawakala wakubwa kwa kutumia Hacking, Ransomware na Malware.
-
Mtu wa IT mwenye ujuzi anaweza kuvunja mifumo ya usalama ya tovuti au akaunti za mawakala wa mtandao na kupata taarifa nyeti, kama nywila au taarifa za kifedha.


2. Kuhatarisha usalama wa watu wangu wa karibu ikiwemo wazazi, ndugu na jamaa kwa kushirikiana na vikundi hatari.

3.Utakatishaji fedha, Yaani hii kesi hata mimi nilishangaa kivipi tena, Ila serikali duuh?


Iko hivi Sisi tulikua hatuvamii na kuua, Tunakuja kwako kama Internet service providers, au wawakilishi toka mitandao tofauti ya simu na vitambulisho FAKE kama ID za jf, Zikipatikana data zako [Taharifa za msingi], zinatumwa kwa wale IT wa kule porini, Wale ndiyo wanajua jinsi ya kuiba pesa yako kutumia hizo data, Pesa ikishaibwa inaingizwa bank kwenye akaunti tofauti tofauti, Mfano milioni10 inaweza ikagawanywa mara 5.


Kila Mtu anapewa kadi yake ya kupokelea pesa, pesa ikiingia inatakuwa aende ATM, akaitoe chap, ili kwamba dili likibumburuka ile akaunti ya bank inafutwa na wale IT chap.


Wale IT walikua na uwezo wa ku create Fake bank akaunti za matawi yote, Walikua na uwezo wa kutengeneza ID ya kampuni yeyote, Laini ilitakiwa ziwe nyingi sababu kila Mission ikikamilika mnasajiliwa line mpya zile zilizotumika mnazitupa.


Sasa mimi na yule jamaa ndiyo tukawa collectors wa pesa, Yaani pesa inatakiwa ifike kwenye ile Cruiser kwa mfumo wa Cash 💵.


Bhasi tena Mimi Ibn Unuq Nikasomewa Kifungo cha Miaka 50 jela na faini ya milioni 25.


Naiandika hadithi hii kwa uchungu nikiwa nyuma ya nondo, Kile kikosi changu chote tulikamatwa mpaka wale ma-IT. Wawili niko nao jela moja, wengine sijui walipelekwa wapi, saa nyingine walishapoteza maisha kasoro yule jamaa aliyenigonga "MBOKA" sijui atakua wapi kwasasa.


Mpaka sasa hivi ninavyoandika imekatika miaka10 bado nipo jela, japo mazoezi sijaacha na wala sijutii lolote sababu - nimestahili "What goes arround Comes arround".


Nawashauri ndugu zangu tufuate sheria, Tuishi kwa kutafuta vilivyo halali, jela kubaya sana, Mkusikiage tu.


MWISHO.

____________________________


Wakuu Introduction kwenye chapta one ni sahihi kabisa na ile picha ni ya kwangu, ila Chai ilianzia pale nilipochukua pikipiki ya Daywaka.


Ukweli mwingine ni bro JIMMY, ni kweli kabisa alinifundisha kuendesha pikipiki wakati nimerudi mbeya baada ya kumaliza chuo, Ila ndiyo sikuchukua hiyo pikipikipi ya mkataba kama nilivyoendelea kusimulia bali nilikaa Mbeya wiki3 tu kusaidia kazi za pale home Then nikarudi zangu Dar-es-salaam kuanza biashara ndogo ndogo.


Sasa hivi kabiashara kamekua kidogo -natumia nguvu ya watu wengine, Tunasaidiana kuendesha miradi yangu [Nimewekeza zaidi kwenye biashara ya mbao na kilimo].


Kwakuwa kazi wanafanya vijana unakuta ninakua na muda mwingi wa kupumzika, And as long as napenda kuwa peke yangu- peke yangu hua najitahidi Ili muda usipotee. Hivyo naangaliaga nifanye nini ili nisave time, Sometimes nasafiri mikoa tofauti kuangalia fursa za kilimo, sometimes nasoma vitabu tofauti tofauti, sometimes ndiyo hivyo tena Mazoezi.


Sometimes hua najitahidi hivyohivyo hata kama sipendi kuchangamana naingage kwenye michezo - Football & Tennis, Muda mwingi nautumia JF pia.


Mfano Sasa hivi niko Kifanya - Njombe huku, nimekuja kukata miti ya mbao na hapa nimetulia zangu kwenye chumba nilichopanga, Huku nina kazi ya miezi mitatu ya Kushusha msitu, Ila makazi rasmi Dodoma.


Niko nashusha Uzi, Ngoja Niwaibie siri kidogo, Nimeshaandika hadithi nyingi sana kipindi niko chuo yote hii sababu ya kuwa nakua peke yangu- peke yangu, nikawa namuuzia Hafidhi Jr Ikhram kwa wanaomjua, Alipeta sana Enzi zake huko facebook [Kabla sijajiondoa huko na Kufuta akaunti yangu].


Ibn Unuq ana tabia ya kuchange kulingana na watu na mazingira, Mijadala ya utani utani - Ana switch, Mijadala serious - Ana switch, Ila ikivukwa mipaka anakuchana , ana kuignore.


Siku nikitulia nitawaletea mkasa wa kusisimua, kuna kipindi Niliwahi kuchukua pesa za moto.


Watagg na wengine, wavunje mbavu na huu mkasa.


LENGO NI KUKUMBUSHIA UJUZI WANGU WA KUANDIKA STORRY ZIZIZOCHOSHA KUSOMA.
Hii story kuna wana hapo mbeya ndo zilikuwa mambo zao mmoja alipigwa juju akaweuka hadi sasa, kuna waliokuwa wanajenga lodge mitaa fulani baada ya dili kubumbuluka walitimka wote hadi sasa awajaludi . Kwa mbeya hii story ina ukweli kwa kiasi chake
 
Hii story kuna wana hapo mbeya ndo zilikuwa mambo zao mmoja alipigwa juju akaweuka hadi sasa, kuna waliokuwa wanajenga lodge mitaa fulani baada ya dili kubumbuluka walitimka wote hadi sasa awajaludi . Kwa mbeya hii story ina ukweli kwa kiasi chake
Wewe unaona mbali kaka!! 👊🏾
 
Back
Top Bottom