mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Kuna miaka nilikuwa mkoa fulani katika kupambana na maisha, nikapanga room mi na mwamba mmoja tuliyetoka nae mjini, huyu mwamba ikifika usiku mnene ananiamsha nakunionyesha watu au mtu ambaye simuoni, nikadhani anakuwa anaota, tukiamka ndio ananiambia kuwa jana usiku huyu mama wa nyumba ya jirani alikuja kutuwangia uchi, nikimuuliza kajuaje akadai ana dawa za kupaka machoni.
Siku moja nikamuomba kupaka zile dawa jioni halafu tukaenda kwenye harusi moja huko kijijini, nilichokiona sitasahau, watu walikuwa wanacheza ngoma uchi, mara wanatumia mafuvu kunywa pombe, kumbe zile dawa zinafanya kazi, kilichonifanya nikamatwe na kupelekwa milembe ni baada ya kuona kundi la fisi linakuja kila nikipiga kelele watu wanashangaa hao fisi wako wapi?
Jamaa mmoja akasema funga kamba pekeka Milembe, njiani wale fisi wakadandia pick up nikazidisha kelele, kilichoniokoa ni yule mwamba kuja kufuta zile dawa machoni mwangu.