Nilivyopelekwa milembe wakidhani mi kichaa kumbe ni mzima

Nilivyopelekwa milembe wakidhani mi kichaa kumbe ni mzima

Nilikuwa chumbani kwangu mara nikamiuona mtu (kivuli chenye umbo la mtu) nikaanza kupiga kelele baba mtuu ,mzee katoka nduki hadi chumbani kwangu akauliza yuko wapi huyo mtu nikaonyesha alipo mzee wangu bila uoga akasogea hadi pale ....

Akanigeukia huku ananishanga "mtu gani si nguo hii ??? " 😆😆😆 kumbe ilikuwa nguo niliitupa kwenye baiskel sasa ikajichora umbo la mtu plus uoga nikawa naiona Kama incheza
 
Kuna miaka nilikuwa mkoa fulani katika kupambana na maisha,nikapanga room mi na mwamba mmoja tuliyetoka nae mjini,huyu mwamba ikifika usiku mnene ananiamsha nakunionyesha watu au mtu ambaye simuoni,nikadhani anakuwa anaota,tukiamka ndio ananiambia kuwa jana usiku huyu mama wa nyumba ya jirani alikuja kutuwangia uchi,nikimuuliza kajuaje akadai ana dawa za kupaka machoni,siku moja nikamuomba kupaka zile dawa jioni alafu tukaenda kwenye harusi moja huko kijijini,nilichokiona sitasahau,watu walikuwa wanacheza ngoma uchi,mara wanatumia mafuvu kunywa pombe,kumbe zile dawa zinafanya kazi,kilichonifanya nikamatwe na kupelekwa milembe ni baada ya kuona kundi la fisi linakuja kila nikipiga kelele watu wanashangaa hao fisi wako wapi,jamaa mmoja akasema funga kamba pekeka milembe,njiani wale fisi wakadandia pick up nikazidisha kelele,kilichoniokoa ni yule mwamba kuja kufuta zile dawa machoni mwangu
Alkasuus mujaarab hii

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Wewe ulikuwa wa kutiwa vibao tu akili ikae sawa, Mirembe huwa hawapelekwi watu wenye wenge la kuona sijui fisi...
 
😂😂 hujamalizia uzi mkuu...

vp ulifanikiwa kuingia mirembe?? au safari iliishia njian
 
Sio kwamba hizo dawa ndio zilikuletea maruwe ruwe, hakukua na hvyo vitu ulivyoviona?😁
 
Kuna miaka nilikuwa mkoa fulani katika kupambana na maisha, nikapanga room mi na mwamba mmoja tuliyetoka nae mjini, huyu mwamba ikifika usiku mnene ananiamsha nakunionyesha watu au mtu ambaye simuoni, nikadhani anakuwa anaota, tukiamka ndio ananiambia kuwa jana usiku huyu mama wa nyumba ya jirani alikuja kutuwangia uchi, nikimuuliza kajuaje akadai ana dawa za kupaka machoni.

Siku moja nikamuomba kupaka zile dawa jioni halafu tukaenda kwenye harusi moja huko kijijini, nilichokiona sitasahau, watu walikuwa wanacheza ngoma uchi, mara wanatumia mafuvu kunywa pombe, kumbe zile dawa zinafanya kazi, kilichonifanya nikamatwe na kupelekwa milembe ni baada ya kuona kundi la fisi linakuja kila nikipiga kelele watu wanashangaa hao fisi wako wapi?

Jamaa mmoja akasema funga kamba pekeka Milembe, njiani wale fisi wakadandia pick up nikazidisha kelele, kilichoniokoa ni yule mwamba kuja kufuta zile dawa machoni mwangu.
Duniani kuna mambo!
 
Back
Top Bottom