Katika jamii nyingi za kiafrika kuna kodi inaitwa Black Tax, Ukisha onekana una kipato simu zinaanza kuita, yaani tayari ushavikwa jukumu la kusaidia ndugu wa familia, ndugu wa baba, ndugu wa mama hadi wa mke.
Katika vitu ambavyo ningependa kuvijua tangu mwanzoni ni hivi
Nitazungumzia zaidi point ya tatu UWAJIBIKAJI NA UWAZI WA MATOKEO
Tatizo sio kutoa msaada bali ni kwamba waafrika wengi tunasahau kitu muhimu sana kinachoitwa UWAJIBIKAJI.
Asili ya binadamu inaonyesha kuwa kila inapokosekana uwajibikaji, unyonyaji huwa mkubwa na nidhamu hupungua. Na ndivyo ilivyo hata kwa watanzania wanaoishi Marekani na Ulaya wanapotuma pesa nyumbani, Wanarudi likizo hakuna kilichoendelea, Nchi yetu inapewa misaada mingi kwa miaka mingi lakini inaishia kuchezewa na viongozi kwasababu hakuna UWAJIBIKAJI.
Mara nyingi, nimewaambia wanafamilia na Ndugu wa baba / mama / mke kwamba wanaponiomba msaada wasinipe tu makadirio ya matumizi yao bali kuwe na uwajibikaji na matokeo nayoweza kuyafuatilia au kuyaona,
Mwanzoni waliniita mbahili / Kauzu, Nami nilikaza sikutoa chochote nilipoona msaada wa mwisho hauna uwajibikaji wala matokeo.
Nilikuwa natoa pesa lakini ndugu hawakuwahi kunipa matokeo, nidhamu yao ya pesa ilikuwa ndogo sana, mtu umempa pesa ya mtaji anafungua duka kwa kusua sua baada ya mda chalii, mtu unamlipia ada wala hakupi updates, unampa mtu pesa ya kulima inaishia kwenye pombe za kienyeji, n.k.
Baada ya visa vingi nimekuwa nikisema wazi kabisa kuwa ikiwa sitapata matokeo ya pesa zangu, sitatoa pesa. Nafanya kazi kwa bidii sana, siwezi kutoa pesa kwa watu ambao ni wazima wenye afya lakini hawapo tayari kuwajibika na kunipa access ya matokeo ya pesa niliyowapa, yaani kwao kupokea pesa inakuwa kama njia ya kuishi.
Haijalishi hali ya umasikini, ikiwa uwajibikaji na matokeo havipo, kuna uwezekano mkubwa sana pesa zitatumika vibaya. Siwezi tena kutoa pesa kwa ajili ya mtaji wa biashara bila masharti ya uwajibikaji na kweli kwa msimamo niliojenga watu huwa wanajua namaanisha nachosema.
Unataka pesa kwa ajili ya biashara? Nipe business plan, Nionyeshe umedhamiria kuwajibika, furaha yangu nione unajitegemea, sihitahi hata senti yako.
Unataka Nikusomeshe chuo ? Nionyeshe una uhitaji wa elimu, niwe updated na matokeo yako hata kama sio mazuri tujue namna ya kuyaboresha au uende veta ujifunze ujuzi, Kumsomesha mtu chuo miaka mitatu ni takriban milioni 10, Chagua kozi ambayo angalau kuna matangazo ya ajira mara kwa mara au utaweza kujiajiri baada ya kuhitimu, siwezi kuchoma milioni 10 kukusomesha kozi ambayo hata wahitimu wanajuta kuichagua.
Unataka kulima ? Niambie shamba lipo wapi nikakukodie, nishirikishe kwenye matokeo.
Misimamo yangu leo hii haijaleta matokeo makubwa sana ila kwa kidogo nilichotoa kwa kipato changu cha kawaida naweza kujivunia
Kuna ndugu alikuwa kahitimu chuo hana kazi, nilimsaidia mtaji kidogo mwanzoni na kunionesha ana kiu, nikamuongezea zaidi, kwa sasa nafurahi kumuona tunawashiana taa barabarani
Ndugu wa mke waliokuja kumsalimia na kuishia kukaa miezi niliwatafutia sehemu ya kujifunzia kazi, mwanzoni nilipingwa nanyanyasa wageni lakini leo hii wana shughuli zao zinazowaingizia vipato na moja kaoa tayari
Mwengine kamaliza chuo mwaka jana, kwa sasa kajishikiza kwenye uteller wa benki, si haba kwa kuanzia
Pesa siyo za bure; kila wakati zina gharama kwa mtu. Kwa hivyo, kabla ya kumsaidia mtu yeyote, daima nasisitiza nia yao ya kuwajibika na kuwepo kwa uwazi wa matokeo. Ikiwa baada ya muda sioni sifa hizi, pesa zangu hukauka na hazirudi tena.
Ninatoa msamaha tu kwa masuala yanayohusiana na afya, isipokuwa yale yanayosababishwa na mtu mwenyewe, kama vile wajomba walevi wanaojiletea matatizo ya kiafya kwa kunywa kupita kiasi bila nia ya kuacha

- Usije kutaja kipato chako halisi, pendelea kutaja kipato kinachobaki baada ya kodi, matumizi, shughuli za uwekezaji, n.k. wengi ukiwaambia unapata kiasi flani, huchukulia ni kiasi kitachoweza kumudu misaada.
- Kupaumbele cha misaada kiwe kusaidia watu wajifunze kujitegemea mfano kutoa mtaji, kukodi shamba, kulipia ada, peleka veta, n.k. Saidia kufundisha kuvua samaki sio kuwapa samaki
- Hakikisha pesa unayotoa kuna UWAJIBIKAJI NA UWAZI WA MATOKEO