Nilivyoweza kujinasua kwenye gharika la ndugu omba omba, Nilionekana mbahili lakini wanaanza kunielewa, pesa yangu siwezi kuitoa bila uwajibikaji

Nilivyoweza kujinasua kwenye gharika la ndugu omba omba, Nilionekana mbahili lakini wanaanza kunielewa, pesa yangu siwezi kuitoa bila uwajibikaji

Yes , watu hawaelewi hili jambo .

Ndo maana ni vizuri MTU ukampatia mbinu za kujimpambania yeye Kama yeye . mfano kumtafutia kibarua , n.k

Maana hamna hela ambayo utampatia MTU na akapiga hatua . wachache ndo wanaweza .
Mkuu sasa kama mtu hana qualification za kujiajiri inakuaje. Kuna mmoja nimempatia 7 mls lakn biashara yake hata kuzalisha 3000 kwa siku imekuwa changamoto... Wakati mwingine mkuu labda nipe mawazo
 
Mkuu sasa kama mtu hana qualification za kujiajiri inakuaje. Kuna mmoja nimempatia 7 mls lakn biashara yake hata kuzalisha 3000 kwa siku imekuwa changamoto... Wakati mwingine mkuu labda nipe mawazo

Unapotaka kumsapoti mtu hasa ndugu zetu hawa .

Anza umpime uone anaweza nini ukimuona hana nidhamu ya hela usimpatie Biashara , muingize katika Kazi za kuajiriwa hizo zitamfaa .

Hata Kama hajasoma unaweza ukawa na project ukamuweka Kama kibarua Ila yeye asiwe msimamizi wa moja Kwa moja.

Tofauti na hapo itakuwa ngumu. Na wale ndugu ambao umri sio mkubwa Sana at least wasomeshe wapate ujuzi wa mikono Kama kuchomelea , ufundi bomba n.k

Usimpatie MTU hela ambaye unajua kabisa nidhamu yake ya hela ni ndogo
 
Hizi za kuwaweka ndugu kwenye biashara zetu hapo mtagombana. Kuna mmoja nilimweka kwenye huduma za kifrdha mpesa, tigo pesa na miamala ya kibenki. Laiti nisingekuwa mimi sikai na kinyongo moyoni hata leo tusingekuwa tunazungumza mkuu.
Yani mimi napambana sana lakini nashindwa kusonga coz 80% ya mapato yangu yanaishia kwa ndugu aisee
 
Pole sana mkuu hilo jambo lako linahitaji maombi

Maana 80% maana yake sio mchezo
 
Mkuu sio rahisi. Mimi naweza kukwambia asilimia 80% ya mapayo yangu huishia kwa ndugu lakini hakuna ambaye hata amepiga hatua ya kujitegemea kasoro mmoja tu.
Ni jambo linaniap stress sana and almost wote ni over 28
Duh ni wakiume?
 
Katika jamii nyingi za kiafrika kuna kodi inaitwa Black Tax, Ukisha onekana una kipato simu zinaanza kuita, yaani tayari ushavikwa jukumu la kusaidia ndugu wa familia, ndugu wa baba, ndugu wa mama hadi wa mke.

Katika vitu ambavyo ningependa kuvijua tangu mwanzoni ni hivi
  • Usije kutaja kipato chako halisi, pendelea kutaja kipato kinachobaki baada ya kodi, matumizi, shughuli za uwekezaji, n.k. wengi ukiwaambia unapata kiasi flani, huchukulia ni kiasi kitachoweza kumudu misaada.
  • Kupaumbele cha misaada kiwe kusaidia watu wajifunze kujitegemea mfano kutoa mtaji, kukodi shamba, kulipia ada, peleka veta, n.k. Saidia kufundisha kuvua samaki sio kuwapa samaki
  • Hakikisha pesa unayotoa kuna UWAJIBIKAJI NA UWAZI WA MATOKEO

Nitazungumzia zaidi point ya tatu UWAJIBIKAJI NA UWAZI WA MATOKEO

Tatizo sio kutoa msaada bali ni kwamba waafrika wengi tunasahau kitu muhimu sana kinachoitwa UWAJIBIKAJI.

Asili ya binadamu inaonyesha kuwa kila inapokosekana uwajibikaji, unyonyaji huwa mkubwa. Na ndivyo ilivyo hata kwa watanzania wanaoishi Marekani na Ulaya wanapotuma pesa nyumbani, Wanarudi likizo hakuna kilichoendelea, Ncho yetu inapewa misaada mingi kwa miaka mingi lakini inaishia kuchezewa na viongozi kwasababu hakuna UWAJIBIKAJI.

Mara nyingi, nimewaambia wanafamilia na Ndugu wa baba / mama / mke kwamba wanaponiomba msaada wasinipe tu makadirio ya matumizi yao bali kuwe na uwajibikaji na matokeo nayoweza kuyafuatilia au kuyaona,

Mwanzoni waliniita mbahili / Kauzu, Nami nilikaza sikutoa chochote nilipoona msaada wa mwisho hauna uwajibikaji wala matokeo.

Nilikuwa nalipia ada za shule lakini ndugu hawakuwahi kunipa matokeo ya masomo, nakuja kugundua baadae kwamba mtu haendi hata shuleni, matokeo ni mabovu, n.k.

Baada ya visa vingi nimekuwa nikisema wazi kabisa kuwa ikiwa sitapata matokeo ya pesa zangu, sitatoa pesa. Nafanya kazi kwa bidii sana, siwezi kutoa pesa kwa watu ambao ni wazima wenye afya lakini hawapo tayari kuwajibika na kunipa access ya matokeo ya pesa niliyowapa, yaani kwao kupokea pesa inakuwa kama njia ya kuishi.

Haijalishi hali ya umasikini, ikiwa uwajibikaji na matokeo havipo, kuna uwezekano mkubwa sana pesa zitatumika vibaya. Siwezi tena kutoa pesa kwa ajili ya mtaji wa biashara bila masharti ya uwajibikaji na kweli kwa msimamo niliojenga watu huwa wanajua namaanisha nachosema.

Unataka pesa kwa ajili ya biashara? Nipe business plan, Nionyeshe umedhamiria kuwajibika, furaha yangu nione unajitegemea, sihitahi hata senti yako.

Unataka Nikusomeshe ? Nionyeshe una uhitaji wa elimu, niwe updated na matokeo yako hata kama sio mazuri tujue namna ya kuyaboresha.

Unataka kulima ? Niambie shamba lipo wapi nikakukodie, nishirikishe kwenye matokeo.

Misimamo yangu leo hii haijaleta matokeo makubwa sana ila naweza kujivunia

Kuna ndugu alikuwa kahitimu chuo hana kazi, nilimsaidia mtaji kidogo mwanzoni na kunionesha ana kiu, nikamuongezea zaidi, kwa sasa nafurahi kumuona tunawashiana taa barabarani

Ndugu wa mke waliokuja kumsalimia na kuishia kukaa miezi niliwatafutia sehemu ya kujifunzia kazi, mwanzoni nilipingwa nanyanyasa wageni lakini leo hii wana shughuli zao zinazowaingizia vipato na moja kaoa tayari

Mwengine kamaliza chuo kwa gpa bomba, kwa sasa kajishikiza kwenye uteller wa benki, nafurahi namna anavyopambana

Pesa siyo za bure; kila wakati zina gharama kwa mtu. Kwa hivyo, kabla ya kumsaidia mtu yeyote, daima nasisitiza nia yao ya kuwajibika na kuwepo kwa uwazi wa matokeo. Ikiwa baada ya muda sioni sifa hizi, pesa zangu hukauka na hazirudi tena.

Ninatoa msamaha tu kwa masuala yanayohusiana na afya, isipokuwa yale yanayosababishwa na mtu mwenyewe, kama vile wajomba walevi wanaojiletea matatizo ya kiafya kwa kunywa kupita kiasi bila nia ya kuacha
Wewe hata nchi unafaa kupewa👏👏👏👏
 
Katika jamii nyingi za kiafrika kuna kodi inaitwa Black Tax, Ukisha onekana una kipato simu zinaanza kuita, yaani tayari ushavikwa jukumu la kusaidia ndugu wa familia, ndugu wa baba, ndugu wa mama hadi wa mke.
 
Africa usipokuwa makini utagombana mpaka na wazazi kwenye suala la pesa ndio maana matajiri wengi Tanzania hawapatani na familia zao.
 
Tatizo lenu kubwa watoa mitaji ni kua mnatoa mitaji ila hamtaki kuwajibika kwayo.

Yaani unampa mtu 1M unataka eti ajiongeze kukupa updates, kama ni ndugu yako na unapenda aendelee basi muulize kafikia wapi, kama unaona hajafikia criteria zako basi muulize shida nini na umshauri means za kutoboa. Sasa ninyi mnatoa hata 1m tu bila maelekezo as long as ndgu kakuomba ili mwisho wa mwaka uje kumlaumu kua ulishampa 1M na hajaifanyia ipasavyo, kama wahaya wengi wafanyavyo.
 
Africa usipokuwa makini utagombana mpaka na wazazi kwenye suala la pesa ndio maana matajiri wengi Tanzania hawapatani na familia zao.
Ndivyo ilivyo, upo mjini ukisema nijenge walau nyumba ndogo ili nipumzike Kodi utasikia kwanini usianze wanajua mkewe kamshawishi shida tupu
 
Kama kujitafuta kwako mpaka unajipata ndugu hawakushiriki una haki ya kuwakataa lakini kama viatu vya shule kanunia mjomba,uniform kanunia bamdogo,kaka alikulipia ada lazima uwajibike kwao ....otherwise funga mdomo wako.
 
Back
Top Bottom