Nilivyoweza kujinasua kwenye gharika la ndugu omba omba, Nilionekana mbahili lakini wanaanza kunielewa, pesa yangu siwezi kuitoa bila uwajibikaji

Sina utajiri wowote, hali ya kiuchumi ya kawaida, ni kwamba kwa tamaduni zetu ni ngumu kukwepa black tax, Nilichoongeza ni uwajibikaji.
 
Wasaideni watu kama Mungu kakupa fursa ya kufanya hivo...

Katika vitu najivunia ni kua na moyo wa kutoa sana msaada kwa watu hata nisiowajua... Hata humu JF nimeshasaidia watu wengi tu kupata vibarua na hata watujuani na sijataka tujuane wengine hadi hulazimisha kunipa zawadi ila hua mara nyingi nakataa ni mmoja tu niwewahi kuchukua shukurani yake..

Kuna kipindi nilikua nimepigika sana Mungu akanifungulia milango nikapata mchongo.. kama kawaida simu kutoka kwa ndugu na jamaa zilikua nyingi na Mimi nilikua nawasaidia bila kujiuliza mara mbili...

Nakumbuka wakati wa changamoto baada ya kupoteza kazi mke wangu alikua anakaribia kuzaa Sina hili wa lile nikampigia rafiki mmoja ambaye niliwahi kumpa chaka mahala.. huwezi amini jamaa baada ya kumweleza shida zangu alinitumia milioni Moja na nusu sio mkopo.!

Kwahiyo usifikiri wewe umeyamaliza maisha na kuwaona wengine wajinga kwenye maisha Kuna kupanda na kushuka...

BEN MWAITEGE - SAFARI BADO
 
Wasaidien ndugu zenu acheni roho mbaya

Unakuta mtu mmoja umejilimbikizia uchumi mwingi sana alafu ndugu zako wote masikin mafukara wa kutupwa

Hata ikitokea umekufa hakuna hata ndugu yako mmoja mwenye uwezo wa kununulia hata jeneza la laki mbili
This is a strawman argument fallacy.

Jifunze kusoma kwa ufahamu na kujadili kimantiki si kubishana kwa ushabiki kihisia.

Mtoa mada hajapinga kusaidia ndugu, ameongelea misingi ya kuongeza ufanisi na kupunguza kusaidiana kusiko na tija ambako kutamfunga katika umasikini msaidia na msaidiwa.

Huelewi wapi?
 
Bhebhe nzunya kinehe

Christmas 🎄 elelo
 
Wewe una sifa? YEye hana yes wewe vipi?
 
Nendeni PM wakuu, naona uzi ushabadilika kuwa wa kilugha 😂
Mkuu,

Kama Muislamu akipewa "Asalaam Aleikum" ilivyokuwa vibaya sana kukataa kuirudishia "Aleikum Salaam" na sisi Wasukuma mtu akikusalimia au kukuongelesha Kisukuma kama unakijua ni kitu kibaya sana kutomrudishia Kisukuma.

Nimeelewa hilo unalolisema ndiyo maana sijaendeleza mazungumzo.

Wewe ndiye unayaendeleza sasa.
 
🤝
 
Wasaidien ndugu zenu acheni roho mbaya

Unakuta mtu mmoja umejilimbikizia uchumi mwingi sana alafu ndugu zako wote masikin mafukara wa kutupwa

Hata ikitokea umekufa hakuna hata ndugu yako mmoja mwenye uwezo wa kununulia hata jeneza la laki mbili
Mkuu sio rahisi. Mimi naweza kukwambia asilimia 80% ya mapayo yangu huishia kwa ndugu lakini hakuna ambaye hata amepiga hatua ya kujitegemea kasoro mmoja tu.
Ni jambo linaniap stress sana and almost wote ni over 28
 
NINYI VIUMBE BINADAMU MNA MAPUNGUFU MAKUBWA SANA

MMEPEWA HEWA YA BURE NA BABA YENU WALA HAMLIPII LAKINI NINYI KUWASAIDIA NDUGU ZENU MNAWAPIGIA MAHESABU

HAKIKA MNA LAANA NDANI YENU, ITAWATESA SANA

HAKUNA BINADAMU MKAMILIFU PASIPO WENZAKE, KWENYE HALI YA MATATIZO WATAKAOWASAIDIA NI WATU WENGINE KWAMAANA KUWA WAKATI HUO NINYI HAMTAWEZA KUJISAIDIA WENYEWE
 
Mkuu sio rahisi. Mimi naweza kukwambia asilimia 80% ya mapayo yangu huishia kwa ndugu lakini hakuna ambaye hata amepiga hatua ya kujitegemea kasoro mmoja tu.
Ni jambo linaniap stress sana and almost wote ni over 28

Yes , watu hawaelewi hili jambo .

Ndo maana ni vizuri MTU ukampatia mbinu za kujimpambania yeye Kama yeye . mfano kumtafutia kibarua , n.k

Maana hamna hela ambayo utampatia MTU na akapiga hatua . wachache ndo wanaweza .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…