Nilivyoweza kujinasua kwenye gharika la ndugu omba omba, Nilionekana mbahili lakini wanaanza kunielewa, pesa yangu siwezi kuitoa bila uwajibikaji

Yes , watu hawaelewi hili jambo .

Ndo maana ni vizuri MTU ukampatia mbinu za kujimpambania yeye Kama yeye . mfano kumtafutia kibarua , n.k

Maana hamna hela ambayo utampatia MTU na akapiga hatua . wachache ndo wanaweza .
Mkuu sasa kama mtu hana qualification za kujiajiri inakuaje. Kuna mmoja nimempatia 7 mls lakn biashara yake hata kuzalisha 3000 kwa siku imekuwa changamoto... Wakati mwingine mkuu labda nipe mawazo
 
Mkuu sasa kama mtu hana qualification za kujiajiri inakuaje. Kuna mmoja nimempatia 7 mls lakn biashara yake hata kuzalisha 3000 kwa siku imekuwa changamoto... Wakati mwingine mkuu labda nipe mawazo


Unapotaka kumsapoti mtu hasa ndugu zetu hawa .

Anza umpime uone anaweza nini ukimuona hana nidhamu ya hela usimpatie Biashara , muingize katika Kazi za kuajiriwa hizo zitamfaa .


Hata Kama hajasoma unaweza ukawa na project ukamuweka Kama kibarua Ila yeye asiwe msimamizi wa moja Kwa moja.


Tofauti na hapo itakuwa ngumu. Na wale ndugu ambao umri sio mkubwa Sana at least wasomeshe wapate ujuzi wa mikono Kama kuchomelea , ufundi bomba n.k


Usimpatie MTU hela ambaye unajua kabisa nidhamu yake ya hela ni ndogo
 
Hizi za kuwaweka ndugu kwenye biashara zetu hapo mtagombana. Kuna mmoja nilimweka kwenye huduma za kifrdha mpesa, tigo pesa na miamala ya kibenki. Laiti nisingekuwa mimi sikai na kinyongo moyoni hata leo tusingekuwa tunazungumza mkuu.
Yani mimi napambana sana lakini nashindwa kusonga coz 80% ya mapato yangu yanaishia kwa ndugu aisee
 

Pole sana mkuu hilo jambo lako linahitaji maombi

Maana 80% maana yake sio mchezo
 
Mkuu sio rahisi. Mimi naweza kukwambia asilimia 80% ya mapayo yangu huishia kwa ndugu lakini hakuna ambaye hata amepiga hatua ya kujitegemea kasoro mmoja tu.
Ni jambo linaniap stress sana and almost wote ni over 28
Duh ni wakiume?
 
Wewe hata nchi unafaa kupewa👏👏👏👏
 
Katika jamii nyingi za kiafrika kuna kodi inaitwa Black Tax, Ukisha onekana una kipato simu zinaanza kuita, yaani tayari ushavikwa jukumu la kusaidia ndugu wa familia, ndugu wa baba, ndugu wa mama hadi wa mke.
 
Africa usipokuwa makini utagombana mpaka na wazazi kwenye suala la pesa ndio maana matajiri wengi Tanzania hawapatani na familia zao.
 
Tatizo lenu kubwa watoa mitaji ni kua mnatoa mitaji ila hamtaki kuwajibika kwayo.

Yaani unampa mtu 1M unataka eti ajiongeze kukupa updates, kama ni ndugu yako na unapenda aendelee basi muulize kafikia wapi, kama unaona hajafikia criteria zako basi muulize shida nini na umshauri means za kutoboa. Sasa ninyi mnatoa hata 1m tu bila maelekezo as long as ndgu kakuomba ili mwisho wa mwaka uje kumlaumu kua ulishampa 1M na hajaifanyia ipasavyo, kama wahaya wengi wafanyavyo.
 
Africa usipokuwa makini utagombana mpaka na wazazi kwenye suala la pesa ndio maana matajiri wengi Tanzania hawapatani na familia zao.
Ndivyo ilivyo, upo mjini ukisema nijenge walau nyumba ndogo ili nipumzike Kodi utasikia kwanini usianze wanajua mkewe kamshawishi shida tupu
 
Kama kujitafuta kwako mpaka unajipata ndugu hawakushiriki una haki ya kuwakataa lakini kama viatu vya shule kanunia mjomba,uniform kanunia bamdogo,kaka alikulipia ada lazima uwajibike kwao ....otherwise funga mdomo wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…