T-Bagwell
JF-Expert Member
- Apr 6, 2017
- 1,243
- 2,378
Habarini wana jukwaa.
Mwanzoni mwa mwaka jana (December 2024) wazazi wangu walinishauri tutume wawakilishi waende nyumbani kwa wazazi wa mchumba wangu kwaajili ya utambulisho.
Japokua Binti nilishaanza kuishi naye kwa zaidi ya miezi mitatu, ilihali tulishakaa kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka minne.
Niliwataarifu wazazi kwamba wasubirie kwanza mpaka nitakapoweka mambo sawa ndipo nitawaambia ili tuanze taratibu zote mpaka NDOA.
Binafsi mimi sio mfuasi wa DINI kwahiyo swala la ndoa nilipanga kufunga naye ndoa ya KIMAHAKAMA (Japokua hili sikuwashirikisha wazazi kwasababu ni wafuasi sana wa Dini) na pia sikupanga tarehe, mwezi au mwaka (Nilitegemea akishajifungua ndipo nitaanza kuweka taratibu za tarehe na mwezi wa tukio hilo)
Wazazi walikazania sana hilo swala pasipo kunisikiliza, ikafika mpaka hatua wakasema kama unahofia gharama basi sisi tutagharamia…. Ikabidi niwe mpole.
Wakapanga tarehe, wakapanga watu wa kwenda kisha wakanitaarifu nikatoa baadhi ya fedha kwaajili ya ku sapoti shughuli kisha watu wakaenda.
Walipewa tarehe ya mwisho wa mwaka ndipo wapeleke baadhi ya mahitaji mengine/fedha kiandaliwe chakula kwa pamoja ili ndugu zake na wakwangu waweze kufahamiana.
(KULIKUA NA CHANGAMOTO ZA HAPA NA PALE KUTOKANA NA KUTOKUFIKA KWA TAARIFA KUTOKANA NA CHANGAMOTO YA FAMILIA YAO)
Tulijadiliana na wazazi na mwisho wa mwaka ulishindikana kutokana na ratiba zilizokuwepo kwa upande wa ukoo wangu mwisho wa mwaka.
Juzi kabla ya Christmas aliniambia ameitwa kwao na baba yake kwaajili ya kikao, nikamkatalia akalalamika mpaka kufikia stage ya kulia.
Tarehe 28 walipiga simu kwetu kudai kwamba wanamhitaji binti yao kwaajili ya mazungumzo, wazazi wakanipigia nikawambia hawezi safiri mwenyewe kwasababu pia ni MJAMZITO na kama week mbili zilizopita aliumwa na kulazwa mpaka mimba ikatishia kutosha, akahudumiwa na kushauriwa apate muda wa kutosha wa kupumzika.
Baba yake akataka namba yangu azungumze na mimi nikamwambia binti asimpe, baadae nikawasiliana na wazazi wangu nikaona isiwe shida, jioni yake nilimwambia awasiliane na rafiki yake kisha nitawapeleka… kweli alifanya hivyo na rafiki yake alikubali.
Jioni ilifika nikawapeleka japokua sikuwafikisha nyumbani kwao kabisa, nikawakodishia usafiri mwingine then mimi nikaendelea na safari ya kuelekea migombani. (KILIMANJARO)
(HII SAFARI YA KWENDA KWETU ILIKUA NIMEPENGA KWENDA NAE ILI PIA AKAJUMUIKE NA NDUGU ZANGU)
Mwaka mpya ukafika na safari yangu ya kurudi ilikaribia, nikampigia simu usiku wa tarehe moja kumuuliza kama kesho yake tarehe mbili asubuhi atakua tayari ili nimpitie turudi wote nyumbani akaniambia kuna maongezi wanamalizia then yeye atakuja jioni yake/kesho yake asubuhi tarehe 2 nikaona sio shida kwasababu bado kuna ndugu zangu bado walikuwepo migombani so ingekua rahisi kumpa lift kupunguza changamoto za public transport lakini haikua hivyo kutokana na sababu alizoleta za hapa na pale
Leo asubuhi nimeamka najiandaa na harakati za siku napokea simu nyumbani kwamba upande wa mwanamke wamekaa na wametupa tarehe 15/01 kwamba ndio tarehe ya hilo tukio kwahiyo tunapaswa tutume kiasi cha fedha kwaajili ya maandalizi ya hiyo siku.
Kila nikiangalia nafasi ya hiyo tarehe kwa upande wangu na wazazi wangu inakosekana, lakini pia January ni mwezi mgumu karibia kwa kila mtu.
Nawaza ku abort mission lakini in a good way, nachomokaje kwenye hili wakuu… kwasababu tokea mwanzo nilikua namkataza mwenzangu asiende nikitegemea yote haya lazima yatatokea.
Lakini pia wazazi wangu wamechangia yote haya kwasababu nilishawaonya tokea mwanzo lakini walikataa kunisikiliza.