Niliwaonya Simba kuhusu ulinzi wa CEO Barbara mkapuuza, ameshambuliwa Z'bar

Niliwaonya Simba kuhusu ulinzi wa CEO Barbara mkapuuza, ameshambuliwa Z'bar

sioni connection yoyote ya Babra kuitwa pisi na swala la yeye kusumbuliwa hapo Zenji.

By the way unazungumziaje kipigo cha paka mwizi tulichowatembezea jana??
Screen Shot 2021-01-14 at 11.41.04 AM.png
 
INABIDI HANSPOPE ATAFUTIWE CHEO HAPO SIMBA WAHUSIKA WA SASA HIVI WAKO SO SOFT YAANI WALAINI KAMA MLENDA mnashindwa hata kumlinda CEO wenu anayedhalilishwa kutwa mitandaoni na ma redioni via makanjanja yaliyo kwenye pay roll?
 
hamna connection yoyote hapo mzee.
By the way unazungumziaje kipigo cha paka mwizi tulichowatembezea jana??
una kichwa kigumu sana bro ,tukio limetokea juzi kabla ya mechi halafu mbona unahaha sana kwani waliomshambulia ni wa deportivo la utopolo?siku ya december 30 nilipoonya haya yatatokea ya CEO kudhalilishwa ulinikebehi sana sasa yametokea unajaribu kuandika pumba zako
 
maoni yako hayo ndugu....kina kaduguda wananiudhi sana ,vita hii ya sasa siyo ya kawaida wakishindwa kufatilia hili suala wahusika wakamatwe nitawadharau sana
hamna vita yoyote hapa,
jana tumeshaua paka mwizi, jikiteni kwenye kuandaa timu.
 
Baada ya kina Francis Mhando wa Efm kumfanyia dhihaka Barbra na kumuita pisi kali chombo ya fundi wakihusisha maneno ya mtandaoni kuhusu mkude kusimamishwa kwamba alimtongoza nilianzisha uzi hapa na kulaumu sana wako walionisapoti wako waliodhihaki kama kawaida maana kwa Ta nzania mwanamke ni chombo cha starehe tena wako hadi wanawake walionicheka hapa jamvini na kuona naongea pumba.

Mwishoni nilimaliza ule uzi kuwaomba Simba wampe ulinzi barbara nikasema kuna siku atashikwa makalio na manyonyo hadharani, haya yametokea huko zanzibar sasa subirini tu siku wachambuzi wa utopolo watamuita kahaba malaya wakiwa hewani ndipo mtaamka sasa.

=======


Bosi Simba adai kushambuliwa Z’bar​


Thursday January 14 2021


bosi simbapic

Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez

Summary

Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez juzi usiku alifanyiwa fujo katika Uwanja wa Amani mjini hapa, muda mfupi baada ya timu hiyo kumaliza kufanya mazoezi uwanjani hapo.
Advertisement

By Mwanahiba Richard
More by this Author

Unguja. Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez juzi usiku alifanyiwa fujo katika Uwanja wa Amani mjini hapa, muda mfupi baada ya timu hiyo kumaliza kufanya mazoezi uwanjani hapo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Barbara alisema alifanyiwa fujo wakati akiswali swala ya Ishah saa mbili usiku katika uwanja huo, baada ya timu kuondoka.

“Wakati naswali walikuja watu wakaanza kunivuta, kunipiga na kuvuta mtandio wangu. Waliniumiza sana,” alisema mtendaji huyo aliyehusisha tukio hilo na mchezo wa fainali kati ya Simba na Yanga uliochezwa jana usiku.

Alisema baada ya tukio hilo aliripoti katika Kituo cha Polisi Ng’ambo alikofunguliwa jalada lenye namba NGB/RB 247/2021, ambapo watuhumiwa kadhaa walikamatwa na kuwekwa ndani usiku huohuo. Gazeti hili lilifika katika kituo hicho ambapo polisi walikiri kupokea malalamiko na kufungulia jalada la shambulio la mwili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadhi Juma Haji alisema hana taarifa juu ya tukio hilo.

Chanzo: Mwananchi
Anajua maana ya kushambuliwa Sana? Maana kwemye match alikuwepo
Yeye angesema alidhalilishwa maana kushikwa tako sio kushambuliwa
 
fungu limetoka kubwa sana ku demonise simba kwa kila hali kwenye media za makanjanja mmekula hela lakini kuweni na mipaka MTUNZIENI BARBRA HESHIMA YAKE KAMA MWANAMKE MSOMI, msitengeneze mazingira ya nchi hii kwamba Mwanamke ni malaya na hawezi kushika cheo kikubwa bila kulalwa.
Kuna msemo kwamba watu wanakuchukulia kwa jinsi unavyojichukulia.

Simba na Yanga zimeamua kuendesha taasisi zao kihuni, hivyo hata hao watangazaji watazichukulia kihuni hivyo hivyo.

Nimezungumzia recruitment criteria ya CEO hapo, ilikuwa ya kihuni.

Tukija kwenye tatizo la Mkude, unapotoa press release ya utovu wa nidhamu kwenye sports, unakuwa obliged kutaja kosa husika kwa uma. Otherwise angepewa adhabu kimya kimya.

Kutotaja kosa unatengeneza mazingira ya uma kujaza kosa wao wenyewe.

Acheni kujiendesha kihuni ili mpewe heshima stahili.
Hivi nafasi ya CEO aliipataje?

Kazi ilitangazwa?

Qualifications zilikuwa zipi?

Kuna applicants wengine aliopambana nao?

Unadhani selection yake iliangalia nini ukilinganisha na interviewees wengine (kama walikuwepo)?

Ukiyajibu hayo maswali, utaelewa kwamba hiyo nafasi kaipata kwa sababu ya yeye kuwa na ukaribu na Fundi.

Simba walikuwa very unprofessional kwenye recruitment ya hiyo post ya CEO, na haya ndiyo matokeo yake.
 
Akipata wadada makini mithili ya wale ya Hayati Muamar Gaddafi, itakuwa poa sana
 
sitak kuamin kwamba CEO tena mwanamke anakosa ulinzi tena ktk maeneo ya mchanganyiko kama uwanjan
 
aachee ushezi huyooo, ina maana hajui msikiti ulipo?, nani alimwambia anzeee kubinua binua vi -makalio yakee au alikuwa anawatega wa-zenji? mwache apate alicho kuwa anakitafuta
 
😅 Au siyo, unataka Mkuu njaakalihatari ateuliwe awe a personal bodyguard wa Madam CEO.

Kazi ya kulinda pisi kali kama ile, haitachukua muda kabla ya mlinzi naye kusimamishwa kazi kwa utovu wa nidhamu.
hahahahahaha sijui hata kurusha teke lakini kutokana na jinsi nilivyo na njaa itabidi tu nichukue hiyo kazi au hata wakinipa kazi ya kukusanya mapaka meusi ya kutupeleka robo fainali ya CAF poa tu
 
Culture yetu bado hovyo sana aisee

Bado miaka hii,kuna gang motivated violence against women?

I still wonder

Halafu imetokea Zbar wanaposema kuna dini na maadili makali sana?

Dini ni matatizo sana

Logically hainiingii kichwani, kwamba watu wamkute anasali waanze kumvuta vuta?

Tena Zanzibar?

Sijui, inaweza kuwa kweli au kuna habari inatengenezwa.
 
aachee ushezi huyooo, ina maana hajui msikiti ulipo?, nani alimwambia anzeee kubinua binua vi -makalio yakee au alikuwa anawatega wa-zenji? mwache apate alicho kuwa anakitafuta
waoooh just waooohhh hii comment inazidi kuipa nguvu hoja yangu natumai wahusika wa simba watakuwa serious this time
 
sijaingilia popote nimekumbusha uzi nilioweka tarehe 30 december mwaka jana nilwaambia simba wampe ulinzi huyu dada mambo yamebadilika sana huko maredioni kuna makanjanja yana chuki za waziwazi na simba
na huyu dada ana juhudi sana kuna kitu anataku kuki prove kuna watu hawapendi na ule mfumo dume ulio katika jamii na wengine kama kina kigogo 14 wenye chuki zao na Mo dewji mahasira yao yanamuangukia huyu dada
Ni dhahili una jambo lako na huyo CEO.
 
Ni dhahili una jambo lako na huyo CEO.
lipi tena mkuu nakubali determination yake na mimi ni shabiki wa simba na vilevile naishi kwenye jamiii ya kitanzania yenye mfumo dume iliyojaa ma pervets yanyooona wanawake kama pisi kali ambao hatta wakibakwa utasikia kwa nini ulivaa suruali ya kubana ukawatamanisha
 
Back
Top Bottom