Niliyetaka kumuoa kanidanganya kuwa mama yake amelazwa ICU nitume hela ya mchango

Mkiambiwa ndoa ni utapeli mnaona si kweli. Ona sasa unataka kuowa tapeli hana tofauti na wale wa tuma kwa namba hii.
 
Kusinguzia kifo au ugonjwa sio poa
 
Kuna sifa nyingi umezitaja kumhusu naona anakufaa. Kosa moja halifuti mazuri yote labda ukimkuta na jamaa hapo kimbia usigeuke nyuma. Swala kuoa au kutoa ni uamuzi binafsi.
 
Imagine jamaa angeitoa hyo hela huyo binti angezoea alafu ange muona jamaa ni zwazwa ndio angepigwa hela na angegongewa waziwazi
 
Nyamaza usimtafute, atachagua mwenyewe anataka kuja au lah
 
Usimuache akaenda kukopa au akapata shida ... Mapenzi ni uaminifu na uwazi.
 
Wanawake wengi saivi wanapitia kipindi kigumu sana wanaume wanatumia falsafa ya No Reforms No Money.

Sema uncle ukiangalia kwa umakini huyo ni wife material hajawa mbobevu kwenye tasnia ya utapeli ndo maana kadanganya kizembee sana
 
Uongo ni tabia joh, kua mwingine akidanganya kidogo tu hujifeel guilty, sasa mtu asingizie mama yake mzazi ni mgonjwa huyo si muongo pro.

Binti hana mbinu za kumchomoa jamaa hela, unaambiwa kila mwanaume anahonga ila ndio ujanja, utundu na maarifa ya binti yatumike kumchomoa jamaa kibunda, binti hana maarifa, uongo wa kizamani sana huo.
 
Ya Kibingwa Sana Hiyo Na Umetimiza Maandiko Kutoka Katika Kitabu Kitakatifu Cha Biblia,,(1 Petro 3:7).
 
Huyo ukimuoa tegemea kukuingiza matatizoni.

Ndio wale unasikia "kapandishwa kizimbani kwa kosa la kujipatia fedha kwa udanganyifu"
 
Mtoa mada kama hii thread yako sio chai, kulingana na mazuri ya huyo binti ulioyasema, mm nakushauri msamehe tu huyo binti, hamna alie perfect, hata ww haupo perfect, ila duh na huo uongo alokwambia, heri angedanganya kua anaomba umuoengezee hela, anunue shuka jipya au kitenge, au nguo.

Ila hawa madem mizinga Yao nahisi saa ingine si umaskini, ni matumizi ya tamaa, wadada wengi wanapenda kununua vitu vingi ambavyo si vya lazma kwao, wakati kipato Chao kidogo, mwishowe wanaingia kwenye madeni na kuwa wapiga vizinga mdukuzi Melancholic
 
Yaani wewe chifu umemaliza kila kitu. Mwenye macho haambiwi tazama. Mwamba ni mgumu kutoa senti, unaona kabisa yeye ameeleza jinsi anavyonufaika kwa binti kujitoa kwake kumuwekea mazingira vizuri. Lakini hajaonesha fadhila yoyote anayomfanyia, na hajamuoa. Akimuacha atakuwa amemsaidia sana
 
Mtoa mada uyo demu muongo achana nae,ipo siku atakuambia kasafiri kikazi kumbe anakatikiaa kwa jamaa wake boda bodaa.
Alafu uyo hana tofauti na wale wa tuma hela kwa namba hii!
Kama ameweza kudanganya mama yake yupo ICU karibu na kifo huyo hashindwi chochote.
 
Nakazia hapa👿
 
Kwanini huwa mnasubiri mpaka muombwe hela?

Umempa sifa zote za mwanamke ila hela humpi daaa
50k kama huna mpe hata nusu basi

Kwenda kwao ilikuwa upajue kitambo sana na kujitambulisha
Hapo ndio wengi mnafeli
Haya umejitambulisha kwa mama mkwe au nae uliwahi kumuona mitaani
 
Cha muhimu hapo ni wewe kuacha ubahili, kisha umuoe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…