Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Miaka 9 iliyopita mlikua mnatumia njia gani kupigiana video call? Na mlikua mnatumia njia gani kutumiana picha usiku?WanaJF kwema?
Miaka tisa iliyopita nikiwa job kwangu alipita mdada mmoja wa makamo ila kanizidi miaka kadhaa, mi nikamuomba namba baada ya kusalimiana na akanipatia tukaanza kuchat na kuwasiliana sana mana ye hakuwa akiishi maeneo ya karibu na mimi.
Tuliendelea kuchat kwa muda tuu na alinambia hana mahusiano yoyote na kwa kipindi kile niliamini mana tulipigiana video calls na kutumiana picha hadi usiku wa manane. Kwakifupi tukiingia kwenye penzi na kama kawaida ya penzi jipya lilianza kwa moto sana na kila mmoja alizidi kupata matamanio ya kukutana na mwenzake ili adhiirishe aliyojionea kwenye zile picha tulizotumiana na yale aliyoambiwa na mwenzake.
Siku zikaenda na hatimaye tulikutana kwa mara ya kwanza na nakumbuka ilikuwa Hotel moja Tanga, tulipiga stori kidogo lakini kwakuwa lengo halikuwa stori haikutuchukua muda mwingi tukajikuta tunachezeana na hatimaye kila mmoja akajikuta anamfaidi mwenzake.
Kiukweli tulijikuta kwenye penzi zito na lilienda hadi mwaka mwenzangu akapata ujauzito. Kwakuwa nilikuwa nafanya naye sana sikuwa na nguvu ya kukataa, nikakubali ile mimba. Lakini nakumbuka kipindi akiwa mjamzito ndo alinifungukia ukweli kuwa alikuwa na mume na alimpa talaka mbili na pia wana mtoto mmoja wa kike.
Ulipita muda na akajifungua mtoto wa kiume lakini nilimuona yule mtoto baada ya miezi sita kwa madai ya kwamba mume wake anamfuatilia na amefungua kesi hivyo mimi sitakiwi kuonekana kule kwakuwa jumba bovu linaweza niangukia. Nilimuelewa na nilitii.
Sasa baada ya miaka kadhaa sipo tena kwenye mahusiano na yule mdada na mtoto amekuwa mkubwa sana na nyumbani kwa wazazi wangu hawajawahi muona na wanatamani sana kumuona ila tatizo ni mama yake mtoto anaogopa kuniachia mtoto kwa sababu mbili, moja ni kuwa naweza nikapotea kabisa na mtoto nayeye asimuone tena, na ya pili ambayo nahisi ni kubwa anamuogopa yule mume wake kwakuwa walivyokuja kuachanishwa na mahakama yule mtoto alikuwa ni sehemu ya watoto waliopata wakiwa pamoja na mume wake na ata jina walimbadilisha akaanza tumia jina la yule aliyekuwa mume wake japo yule mwanaume anajua kila kitu.
Mpaka sasa huyu dada hataki kuniachia mwanangu nikae naye au nimsomeshe ila nikitaka kuongea naye anapewa simu na mtoto anajua kama mimi ndo baba yake. Na ata yule aliyekuwa mume wake anajua kuwa mtoto ni wa kwangu ila anataka kunikomoa kutokana na cheo na kitendo chake kwakuwa anahisi mi ndo nilisababisha ndoa yake kufunjika.
Naomba msaada wanaJF, nifanye nini ili nimpate mwanangu mana nampenda sana na ata yeye ananipenda na ananihitaji sana, amekuwa akiniambia hivyo kila nikiongea naye.
Utaomba mpimweDNAWatanielewa? Mana yule aliyekuwaga mume wake walipopita mahakamani alimlazimisha huyu mwanamke wamfanye yule mtoto kama sehemu yao ya familia hadi walimbadilisha jina
Kwahiyo nifanyeje ndugu yanguSasa hujiulizi kinachofanya aogope,huyo Mwanamke alikuongopea toka mwanzo wa mahusiano bado unaamini kila anacho kuambia.
Kuwa mwangalifu kuna watu wengi wapo wameuwawa kwa ajili ya mapenzi hasa kwenye mambo kama hayo.wewe uliingilia ndoa ya watu halafu bado unaendelea na ujinga.
Mama yake anapata shinikizo na hofu toka kwa mume wake ndo mana hayupo tayarikuwa mpole. kwa nguvu huyo mtoto hutampata na hata ukimpata atakuzingua katika malezi. Mwache mtoto akae na mama yake.
otherwise, ongea kwa upole na mama yake akuelewe na mweleze malengo ya wewe kutaka kukaa na mtoto wa miaka tisa ni yapi maana kama ni malezi umechelewa. Mimi nina watoto wangu watatu niliowapata nje, moja kabla sijaoa na wawili nilikengeuka nikiwa ndani lakini wote niliwachukua, wa kwanza akiwa na miaka 7, wa akiwa na miaka minne na wa tatu akiwa na miaka mitatu. Wote niliwachukua kwa kukabidhiwa na mama zao tena kwa upendo na mahusiano mazuri na wanawasalimia watoto wao kwa uhuru.
Ndio