Niliyezaa naye hataki kunipa mtoto wangu, nifanyaje?

WanaJF kwema?

Miaka tisa iliyopita nikiwa job kwangu alipita mdada mmoja wa makamo ila kanizidi miaka kadhaa, mi nikamuomba namba baada ya kusalimiana na akanipatia tukaanza kuchat na kuwasiliana sana mana ye hakuwa akiishi maeneo ya karibu na mimi.

Tuliendelea kuchat kwa muda tuu na alinambia hana mahusiano yoyote na kwa kipindi kile niliamini mana tulipigiana video calls na kutumiana picha hadi usiku wa manane. Kwakifupi tukiingia kwenye penzi na kama kawaida ya penzi jipya lilianza kwa moto sana na kila mmoja alizidi kupata matamanio ya kukutana na mwenzake ili adhiirishe aliyojionea kwenye zile picha tulizotumiana na yale aliyoambiwa na mwenzake.

Siku zikaenda na hatimaye tulikutana kwa mara ya kwanza na nakumbuka ilikuwa Hotel moja Tanga, tulipiga stori kidogo lakini kwakuwa lengo halikuwa stori haikutuchukua muda mwingi tukajikuta tunachezeana na hatimaye kila mmoja akajikuta anamfaidi mwenzake.

Kiukweli tulijikuta kwenye penzi zito na lilienda hadi mwaka mwenzangu akapata ujauzito. Kwakuwa nilikuwa nafanya naye sana sikuwa na nguvu ya kukataa, nikakubali ile mimba. Lakini nakumbuka kipindi akiwa mjamzito ndo alinifungukia ukweli kuwa alikuwa na mume na alimpa talaka mbili na pia wana mtoto mmoja wa kike.

Ulipita muda na akajifungua mtoto wa kiume lakini nilimuona yule mtoto baada ya miezi sita kwa madai ya kwamba mume wake anamfuatilia na amefungua kesi hivyo mimi sitakiwi kuonekana kule kwakuwa jumba bovu linaweza niangukia. Nilimuelewa na nilitii.

Sasa baada ya miaka kadhaa sipo tena kwenye mahusiano na yule mdada na mtoto amekuwa mkubwa sana na nyumbani kwa wazazi wangu hawajawahi muona na wanatamani sana kumuona ila tatizo ni mama yake mtoto anaogopa kuniachia mtoto kwa sababu mbili, moja ni kuwa naweza nikapotea kabisa na mtoto nayeye asimuone tena, na ya pili ambayo nahisi ni kubwa anamuogopa yule mume wake kwakuwa walivyokuja kuachanishwa na mahakama yule mtoto alikuwa ni sehemu ya watoto waliopata wakiwa pamoja na mume wake na ata jina walimbadilisha akaanza tumia jina la yule aliyekuwa mume wake japo yule mwanaume anajua kila kitu.

Mpaka sasa huyu dada hataki kuniachia mwanangu nikae naye au nimsomeshe ila nikitaka kuongea naye anapewa simu na mtoto anajua kama mimi ndo baba yake. Na ata yule aliyekuwa mume wake anajua kuwa mtoto ni wa kwangu ila anataka kunikomoa kutokana na cheo na kitendo chake kwakuwa anahisi mi ndo nilisababisha ndoa yake kufunjika.

Naomba msaada wanaJF, nifanye nini ili nimpate mwanangu mana nampenda sana na ata yeye ananipenda na ananihitaji sana, amekuwa akiniambia hivyo kila nikiongea naye.
Ukisikia mtu kasomea digrii ya ufugaji badala ya kufuga samaki anaishia kufuga ndevu ndio wewe mkuu.
 
Mi nadhani unahitaji kufanya uchunguzi bunafsi,naona kuna vitu bado hujavijua unaendelea kudanganywa
 
Mtoto sio wako, labda km unatafuta matatizo yasiyo ya msingi.
Kaa mbali na Mke wa mtu, mxxxxxiiiiieeeew
 
Mwanaume hagombei Mtoto
Kama Mwanamke amezuia huyo Mtoto.
Pili, kama toto lenyewe limekukataa.

Zaa wengine
 
Kwahiyo nifanyeje ndugu yangu
Kama Mama wa mtoto hataki kukupa ushirikiano wwe potezea,nakuhaidi kuna siku atakuja kukutafuta,kama siyo yeye basi mtoto wako atakutafuta mwenyewe, ila kama kweli ni Damu yako itakuja tu,na ikija wwe ipokee bila kinyongo! Kumbuka wakati tunapanga,na Mungu nae anapanga! Mi haya yalisha nitokea,lakini namshukuru Mungu baada ya miaka kadhaa nimerejeshewa Kijana wangu copyright, naamini rangi yangu ndiyo iliniokoa,maana mtu na mkewe wote weupe,lakini wametoa kitu Black kama mkaa!! Ila siku zote bado namuhusia kijana wangu,pamoja na mateso yote aliyoyapata bado anatakiwa kumuheshimu Baba yake mlezi!!
 
Mi nadhani unahitaji kufanya uchunguzi bunafsi,naona kuna vitu bado hujavijua unaendelea kudanganywa
Ni kweli pia niligundua Hilo ndo mana nimekuja kuomba ushauri ili nijue pakuanzia
 
WanaJF kwema?

Miaka tisa iliyopita nikiwa job kwangu alipita mdada mmoja wa makamo ila kanizidi miaka kadhaa, mi nikamuomba namba baada ya kusalimiana na akanipatia tukaanza kuchat na kuwasiliana sana mana ye hakuwa akiishi maeneo ya karibu na mimi.

Tuliendelea kuchat kwa muda tuu na alinambia hana mahusiano yoyote na kwa kipindi kile niliamini mana tulipigiana video calls na kutumiana picha hadi usiku wa manane. Kwakifupi tukiingia kwenye penzi na kama kawaida ya penzi jipya lilianza kwa moto sana na kila mmoja alizidi kupata matamanio ya kukutana na mwenzake ili adhiirishe aliyojionea kwenye zile picha tulizotumiana na yale aliyoambiwa na mwenzake.

Siku zikaenda na hatimaye tulikutana kwa mara ya kwanza na nakumbuka ilikuwa Hotel moja Tanga, tulipiga stori kidogo lakini kwakuwa lengo halikuwa stori haikutuchukua muda mwingi tukajikuta tunachezeana na hatimaye kila mmoja akajikuta anamfaidi mwenzake.

Kiukweli tulijikuta kwenye penzi zito na lilienda hadi mwaka mwenzangu akapata ujauzito. Kwakuwa nilikuwa nafanya naye sana sikuwa na nguvu ya kukataa, nikakubali ile mimba. Lakini nakumbuka kipindi akiwa mjamzito ndo alinifungukia ukweli kuwa alikuwa na mume na alimpa talaka mbili na pia wana mtoto mmoja wa kike.

Ulipita muda na akajifungua mtoto wa kiume lakini nilimuona yule mtoto baada ya miezi sita kwa madai ya kwamba mume wake anamfuatilia na amefungua kesi hivyo mimi sitakiwi kuonekana kule kwakuwa jumba bovu linaweza niangukia. Nilimuelewa na nilitii.

Sasa baada ya miaka kadhaa sipo tena kwenye mahusiano na yule mdada na mtoto amekuwa mkubwa sana na nyumbani kwa wazazi wangu hawajawahi muona na wanatamani sana kumuona ila tatizo ni mama yake mtoto anaogopa kuniachia mtoto kwa sababu mbili, moja ni kuwa naweza nikapotea kabisa na mtoto nayeye asimuone tena, na ya pili ambayo nahisi ni kubwa anamuogopa yule mume wake kwakuwa walivyokuja kuachanishwa na mahakama yule mtoto alikuwa ni sehemu ya watoto waliopata wakiwa pamoja na mume wake na ata jina walimbadilisha akaanza tumia jina la yule aliyekuwa mume wake japo yule mwanaume anajua kila kitu.

Mpaka sasa huyu dada hataki kuniachia mwanangu nikae naye au nimsomeshe ila nikitaka kuongea naye anapewa simu na mtoto anajua kama mimi ndo baba yake. Na ata yule aliyekuwa mume wake anajua kuwa mtoto ni wa kwangu ila anataka kunikomoa kutokana na cheo na kitendo chake kwakuwa anahisi mi ndo nilisababisha ndoa yake kufunjika.

Naomba msaada wanaJF, nifanye nini ili nimpate mwanangu mana nampenda sana na ata yeye ananipenda na ananihitaji sana, amekuwa akiniambia hivyo kila nikiongea naye.
Zaa na mwingine
 
Kama Mama wa mtoto hataki kukupa ushirikiano wwe potezea,nakuhaidi kuna siku atakuja kukutafuta,kama siyo yeye basi mtoto wako atakutafuta mwenyewe, ila kama kweli ni Damu yako itakuja tu,na ikija wwe ipokee bila kinyongo! Kumbuka wakati tunapanga,na Mungu nae anapanga! Mi haya yalisha nitokea,lakini namshukuru Mungu baada ya miaka kadhaa nimerejeshewa Kijana wangu copyright, naamini rangi yangu ndiyo iliniokoa,maana mtu na mkewe wote weupe,lakini wametoa kitu Black kama mkaa!! Ila siku zote bado namuhusia kijana wangu,pamoja na mateso yote aliyoyapata bado anatakiwa kumuheshimu Baba yake mlezi!!
Pole na hongera sana ndugu.
Natamani iwe hivyo ata kwangu mkuu lakini naumia kuona jina kabadilishiwa na kupewa lingne sasa ata akija kurudi kwangu baadae vipi jina notaweza kumbadilisha akiwa mkubwa?
 
Back
Top Bottom