Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Finishing ni gharama sana. Ndio maana amesema hivyo. Hakuna kuteleza kwenye finishing ndio maana boma zenye bati zipo nyingi watu wamezitelekeza [emoji28][emoji28][emoji28]
Kupaua ndio stage ngumu kwasababu utahitaji mbao na mabati kwa wakati mmoja nyumba ya kawaida vyumba vitatu ni 4m na kuendelea. Hicho mnachosema finishing ni stages kadhaa ambazo nyingine unaweza kufanya ukiwa ndani ya Boma kwa hela za reja reja.
 
upo sahihi mkuu ila nawaza kipato cha laki 5 unabalancije mahesabu na kama uko na familia au upo singo?
 
Fundisho zuri sana mkuu👍
 
Nilianza ujenzi nikiwa 24 nikamaliza nikiwa 27 aisee nilikuwa napenda nyumba kubwa....nikajenga vyumba vya kujiachia....sebule kubwa ....ila kwa sasa natamani nyumba ndogo
 
Weka picha ya mjengo tuone
 
Mkuu, kwa kipato chako cha 500,000 hadi 550,000

Ulifanikishaje? Tushirikishe huu muujiza.

Hujasema kama upo na chanzo kingine cha mapato.
 
Kupaua ndio stage ngumu kwasababu utahitaji mbao na mabati kwa wakati mmoja nyumba ya kawaida vyumba vitatu ni 4m na kuendelea. Hicho mnachosema finishing ni stages kadhaa ambazo nyingine unaweza kufanya ukiwa ndani ya Boma kwa hela za reja reja.
Kutoa hela kwa mkupuo kweli inauma. Lakin ya kidogo kidogo ndio inakuaga nyingi mwisho wa siku.
 
Hongera Sana kwa hatua umezipiga jemedari.
Leo nilikuwa kuangalia bei za material huko nje hakufai aisee.
Nondo 16mm ni 52-54000/=
Nondo 10mm ni 26000/=
Cement 20000 Hadi 21000
 
Nyumba iko wapi, onyesha picha isijekuwa ni Banda la mbuzi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]maninaaaa umenifanyaa nichekee mpk nionee hchi kibanda changu cjui nikiuzee nilee helaa ,mbinguni ntakutaa nyumba km ww

Usiuze mkuu, ila kiwe cha mwisho kujenga...[emoji23][emoji23]
 
Ntaongeza yafuatayo

1.Kwa maisha ya sasa hakuna haja ya kujenga nyumba kubwa (ya vyumba vingi) maximum nyumba kubwa isizidi 3 bedroom kama ni nyumba ya kwanza jenga 2 bedroom na zote ziwe self contained.

2.Wengi wamenunua viwanja lakini wanaogopa kuanza kujenga sababu wengi hatuna stable income ,jenga nyumba kwa phase(hatua ) msingi,pandisha nyumba,lenta,kupaua,fremu za milango,grill ,plasta,wirering,plumbing etc.Jiwekee target phase moja ndani ya kipindi fulani.Jitahidi kila phase isitumie muda mrefu

3.Usimsikilize sana fundi kwenye kufanya estimation ya vifaa/materials ,mafundi wengi ni wazuri kujenga lakini hawawezi kufanya estimation unaweza kununua extra bati hata 10.Akikwambia mifuko 10 nunua 7 kwanza ikiisha ndio uongeze

Mengine mengi yameshaelezwa
 
Sasa unaogopa nini,hao ndio watatoa taharifa humu siku ukifa ili tukutumie pole huko mbinguni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…