Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Chemba walijenga kila moja 40,000, zilikua 8, nimepigwa ?
 
Hongera,nyumba yako inaukubwa gani ?
Ni kubwa kiasi, Sebule peke yake ni mita 5 kwa 5, master ni 4 kwa 5, kitu ambacho nilikibana ni jiko peke yake napo ni kwasababu nilifanya mabadiliko ya ramani baada ya kuwa nimeshajenga msingi
 
Mkuu nilipofanya plumbing nilikua nishanunua tenk na kujenga mnara hivyo ghrama zilihusisha pia vifaa vya tenk kama nilivyosema, ni nyumba ya kwanza, vifaa vingi nilikua sivijui, hivyo yawezekana upigaji pia umehusika katika hilo, si unajua mafundi
Kama ilihusisha hadi mfumo wa kusafirisha majitaka hadi kwenye Shimo basi hiyo gharama ni sawa tu hasa ukizingatia kujumlisha na gharama za kuunganisha mfumo wa maji kutoka kwenye tank hadi ndani
 
Tunauza mbao kwa bei za jumla
2*4 fut 12=4400
2*4treated fut 12=4800
1*6 fut 12 = 4400
1*8 fut 12= 8500
1*8 ya fisherboard=9500
1*10=13500
1*10 ya fisherboard= 15000
2*2treated fut 12=2500
2*2 fut 12=2300
2*4treated fut 18=9500
2*6 fut 12=8500
2*6treated fut 18=16000
2*2treated fut 18=5000
2*3 fut 12=3500
1*4 fut 18=4000
1*4 fut 12=2500
Tunafanya delivery popote ulipo kwa Dar-es-salaam ,tunapatikana kwa namba hizi hapa 0759630751,
0654830416,
0687371138
vile vile huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu ..
Ofisi zetu ziko Mbuyuni -Bagamoyo road
 
Kunakauli inakatisha tamaa, gharama za kupaua/za bati, zinanitoa damu...ila hapa naona kuwa ukipaua ndio unaanza ujenzi...wtf!!!si bora niache
Kuna nyumba ina vyumba vinne(viwili master), dinning , sebule kubwa store, nk. Ilikuwa imekamilika kila kitu hadi kupauliwa na grill zilikuwepo tayari ila nikawa nimepangisha familia kama tatu hivi wakati naendelea na mengine maana nyumba ipo Mwanza na mimi shughuli zangu nyimgi ni Dar.

Juzi nikawaza kufanyia finishing, yani nifunge wiring ya maana, rangi, gypsum board, Tiles na mfumo wa maji,milango na madirisha ya alminium hiwezi amini hivyo tu imekatika 19M na bado inadai kuwekewa palvings na kumalizia sehemu sehemu. Wakati huo nilienda na budget ya 12M nikiamini itamaliza vitu , vifaa vimepanda bei hatari ila ndohivyo swala la finishing huwa halitaki viporo ukilianzisha kwahiyo nikajilazimisha tu.

Ujenzi ni finishing mkuu, nyumba kama ina milango 10 tu ukitaka ile mizuri million zinakutoka,vitasa tu 70k-200k kimoja.[emoji28][emoji28].

Kama unajenga boma tu na kupaua fanya, ila kama mpunga ni wa mawazo litageuka pagare tu.

SIKUTISHI
 
Ni kweli. Hata floor mwingine anaweka tiles mwingine sakafu ya kawaida.
Nimefanya finishing mwaka huu January, tile hazishikiki sokoni yaani zimepanda ghafla sana.
Box moja la 50*50 ni 48K na vinakaa 7 tu.
 
Ndani ya miaka 3 unaweza Jenga hadi kupaua.Hizo pesa nyingi Sana tena unajibana unasevu 250,000 kwa mwezi,hapo una familia .
Ukisave 250K kwa mwaka mzima haifiki hata 3M ambayo ni hela ya Cement tu, kujenga nyumba kubwa mpaka finishing kwa income ya 500K tena ukiwa na familia eti kwa miaka mitatu ni ngumu sana. Labda uijenge kuanzia kijana uje kuimaliza ukikaribia kustaafu na hala uwe na displine kubwa sana.

Narudia tena ni ngumu sana, unless uwe unafugwa sehemu na hauna familia.
 
Ni kubwa kiasi, Sebule peke yake ni mita 5 kwa 5, master ni 4 kwa 5, kitu ambacho nilikibana ni jiko peke yake napo ni kwasababu nilifanya mabadiliko ya ramani baada ya kuwa nimeshajenga msingi
Ulitumia bati za kampuni gani?
 
Sio inauma mkuu, bali ni ngumu kupata pesa nyingi kwa mkupuo kwa tulio wengi. Shida ndipo inapoanzia na ndio maana kwa tulio wengi sehemu ngumu kuliko zote kwenye ujenzi ni kupaua, the rest is easy hata kama total cost itakuja kuwa kubwa
Unamaanisha muda wa kupaua ni lazima uwe na hela yote ya mbao na mabati hapo hapo? Kwamba huwez nunua kidogo kidogo vikikamilika ndio upaue?
 
Unamaanisha muda wa kupaua ni lazima uwe na hela yote ya mbao na mabati hapo hapo? Kwamba huwez nunua kidogo kidogo vikikamilika ndio upaue?
Ni hivi kupaua hata ukiamua kununua mwaka mzima huwezi kufanya nusu,itabidi uwe na vifaa vyote ndio upaue, wakati finsihing nyingine kama tile unaweza kufanya chumba kwa chumba au nusu chumba, madirisha unaweza ukaweka aluminium chumba kimoja baada ya kingine,gypsum unaweza usiweke ukakaa tu hadi utakapoamua etc.
 
Unamaanisha muda wa kupaua ni lazima uwe na hela yote ya mbao na mabati hapo hapo? Kwamba huwez nunua kidogo kidogo vikikamilika ndio upaue?
Namaanisha siku ya kufanya hiyo kazi lazima ifanyike kwa wakati mmoja, kuanzia kupiga mbao hadi Bati. Huwezi piga mbao ukasubiri miezi sita ndio upige Bati. Hata materials huwezi wekeza dukani zikakaa mwaka mzima, risk yake ni kubwa lazima kuwe na timeframe ambayo ni reasonable. Sasa hapo ndio panapoleta shida, hata fundi lazima uwe na hela yao yote maana watafanya kazi zote ndani ya wiki moja itakuwa imekamilika kabisa. Factors zote hizo ndio zinazoleta ugumu katika hatua ya kupaua
 
Ni hivi kupaua hata ukiamua kununua mwaka mzima huwezi kufanya nusu,itabidi uwe na vifaa vyote ndio upaue, wakati finsihing nyingine kama tile unaweza kufanya chumba kwa chumba au nusu chumba, madirisha unaweza ukaweka aluminium chumba kimoja baada ya kingine,gypsum unaweza usiweke ukakaa tu hadi utakapoamua etc.
Exactly, hii ndio point kuu, ndio maana tunasema ukipaua tayari una nyumba
 
Back
Top Bottom