Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Natamani ningefanya hivyo ila nilishajibu hapo nyuma, kuna watu wakiiona nyumba watagundua ID yangu, kifupi ni nyumba ya vyumba vitatu, kimoja masta, sitting room imeunganika na dinning room, public toilet na jiko, nyumba ina urefu wa mita 9 na upana wa mita 11
Mkuu kama hutojali ,waweza tusaidia karaman tuone..🙏
 
Nilianza ujenzi nikiwa 24 nikamaliza nikiwa 27 aisee nilikuwa napenda nyumba kubwa....nikajenga vyumba vya kujiachia....sebule kubwa ....ila kwa sasa natamani nyumba ndogo

Anzisha familia nyumba hautaiona kubwa tena
 
Ndani ya miaka 3 unaweza Jenga hadi kupaua.Hizo pesa nyingi Sana tena unajibana unasevu 250,000 kwa mwezi,hapo una familia .
Ukisevu 250K kwa mwezi, kwa miaka 3 ni only 9 Million. Haitoshi hata msingi wa nyumba ya vyumba 3 na makolombwezo mengine. Labda uwe na chanzo kingine cha pesa. Ila kwa laki tano na nusu kwa mwezi, ukitoa matumizi ya mwezi. Hata miaka 9 bado utakuwa unajenga. Mimi naona kujenga kutegemea mshahara pekee ni ngumu sana, labda mshahara uwe mamilioni kwa mwezi
 
Mengine yote rahisi,kigumu kwenye ujenzi ni kuweka hela ipatikane Mara 1 ya kununua kiwanja.
Hata mimi kwenye ujenzi, hapo kwenye kupata kiwanja na kupaua ndio palikuwa pagumu zaidi, maana huwezi kufanya nusu nusu. Hatua zinazofuata naamini ni nyepesi kuliko zote kwasababu naweza kufanya nusu nusu, labda kwenye Magrili ya madirisha hapo hapo panahitaji kumaliza yote kwa mara moja
 
Gharama za kupaua zinakua kubwa sababu zinahotajika kwa mara moja, kwa mfano mimi kupaua pekee nimetumia milion 7, hapo ni hela ya fundi bati na mbao. Ila baada ya kupaua, plumbing phase one ime cost 2M, frame za milango mti wa mpili laki tisa, wiring phase one, laki saba, grill 1.5 M, bado mambo yanaendelea
Mkuu plumbing phase one mbona imetumia pesa nyingi sana? Imejumuisha mfumo wa majitaka na ujenzi wa Chemba au?
 
Ndio mkuu...kulaua ndio gharama kubwa kuliko any other stage. Ukimaliza kupaua nyumba imeisha hiyo...tia kashata madirishani mengine unafanya ukiwa humo ndani
Huu ndio ukweli, ni kweli finishing ni very expensive kutegemea na finishing ya aina gani mtu unataka, lkn ni ukweli kuwa nyumba ukishaezeka basi umemaliza ujenzi, hatua zilizobaki utajipimia mwenyewe kulingana na msuli wako. Kupaua ndio hatua ngumu kuliko zote kwakuwa inakutaka uifanye kwa mara moja na vifaa vyake ni vya gharama kubwa sana
 
Kupaua ndio stage ngumu kwasababu utahitaji mbao na mabati kwa wakati mmoja nyumba ya kawaida vyumba vitatu ni 4m na kuendelea. Hicho mnachosema finishing ni stages kadhaa ambazo nyingine unaweza kufanya ukiwa ndani ya Boma kwa hela za reja reja.
Mimi vyumba vitatu kupaua tu na blandaring bati geji 30 migongo mipana imenipiga 12M
 
Huu ndio ukweli, ni kweli finishing ni very expensive kutegemea na finishing ya aina gani mtu unataka, lkn ni ukweli kuwa nyumba ukishaezeka basi umemaliza ujenzi, hatua zilizobaki utajipimia mwenyewe kulingana na msuli wako. Kupaua ndio hatua ngumu kuliko zote kwakuwa inakutaka uifanye kwa mara moja na vifaa vyake ni vya gharama kubwa sana
Yanateketea mahela hapo kwenye kupaua balaaa.
Sasa olewe wako ulogae ujenge ghorofa hela zinavyo teketea kwenye kumwaga slab unaweza anza kulia. Mifuko ya cement inamezwa na concrete mixer kama lina pepo vile🤣🤣🤣🤣
 
Kutoa hela kwa mkupuo kweli inauma. Lakin ya kidogo kidogo ndio inakuaga nyingi mwisho wa siku.
Sio inauma mkuu, bali ni ngumu kupata pesa nyingi kwa mkupuo kwa tulio wengi. Shida ndipo inapoanzia na ndio maana kwa tulio wengi sehemu ngumu kuliko zote kwenye ujenzi ni kupaua, the rest is easy hata kama total cost itakuja kuwa kubwa
 
Yanateketea mahela hapo kwenye kupaua balaaa.
Sasa olewe wako ulogae ujenge ghorofa hela zinavyo teketea kwenye kumwaga slab unaweza anza kulia. Mifuko ya cement inamezwa na concrete mixer kama lina pepo vile[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Siwezi jiroga kujenga ghorofa kama hata nyumba ya kwanza ya kuishi sina! Kujenga ghorofa hela zinateketea halafu huoni hata hatua uliyopiga
 
Ukisevu 250K kwa mwezi, kwa miaka 3 ni only 9 Million. Haitoshi hata msingi wa nyumba ya vyumba 3 na makolombwezo mengine. Labda uwe na chanzo kingine cha pesa. Ila kwa laki tano na nusu kwa mwezi, ukitoa matumizi ya mwezi. Hata miaka 9 bado utakuwa unajenga. Mimi naona kujenga kutegemea mshahara pekee ni ngumu sana, labda mshahara uwe mamilioni kwa mwezi
Tatizo la UJENZI ukiwasikiliza watu, kila pesa utakayokuwa nayo utaambiwa HAITOSHI.

UJENZI ungekuwa gharama hivyo, went nyumba wangekuwa wachache mnooooo.
 
Mkuu plumbing phase one mbona imetumia pesa nyingi sana? Imejumuisha mfumo wa majitaka na ujenzi wa Chemba au?
Mkuu nilipofanya plumbing nilikua nishanunua tenk na kujenga mnara hivyo ghrama zilihusisha pia vifaa vya tenk kama nilivyosema, ni nyumba ya kwanza, vifaa vingi nilikua sivijui, hivyo yawezekana upigaji pia umehusika katika hilo, si unajua mafundi
 
Back
Top Bottom