Leo nimemtembelea ndugu hospitali ya Taifa Muhimbili. Gharama alizonieleza imebidi nione haja ya Serikali yetu kufanya Jambo katika hili.
Wacha gharama za usafiri wa mgonjwa na wauguzi kutoka wilayani, bado kuna gharama za malazi na matibabu. Na gharama za matibabu nilivyoziona, mwananchi wa hali ya chini lazima msiba utazikwa na manispaa.
Naiomba serikali kuliangalia kwa mapana yake na nashauri iweke ruziku katika hosipitali za rufaa zote nchini ili kushusha gharama hizo.
Kwakweli hali ni mbaya.