Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Sasa wewe katika kufanya uchunguzi wako huo ulitegemea familia za hao panyaroad wakwambie walikuwa ni wezi? Acha kwanza polisi wafanye kazi yao la sivyo hao vibaka mtawapa nguvu ya kurudi upya maana wanatetewa, huu sio muda muafaka wa kuongea haya.
Ndiyo. Tukae kimya kama tulivyokaa kimya wakati panyarodi wanapeta mtaani hadi kufunga mitaa. Tuache Polisi wapepetane nao hadi kieleweke -daadek.
 
Aisee nakwambiaje? Hao panyarodi wanavuna walichopanda. Walikuwa na muda wa kujirekebisha/kuacha ukorofi wao(Hawakuliona hilo), walikuwa na muda wa kutoroka ilipoanzishwa Operesheni(Hawakuliona hilo), walikuwa na muda wa kujisalimisha kwenye vyombo/polisi etc(Hawakujiongeza hata kidogo).Lakini wapi. Walikaza shingo, Sikio la kufa halisikii dawa na kusikia kwa kenge ni damu masikioni. Eti mtu anadai tupoteze muda kwenda mahakamani na longolongo kibao.Mbona paya rodi atashinda kesi kwani hajakamatwa na kithibiti. Spidi waliyoanza nayo ndio spidi hiyohiyo watamaliza nayo.
 

Ni wapumbavu peke Yao ambao kama kawaida yao si ajabu kusikia wakishangilia wasikiapo fulani kafa.

Watu hao wamekuwa wakiruka ruka kushangilia waitwao panya road kuuwawa bila kujali ni kweli panya road au la.

Kwa tuhuma hizi dhidi ya polisi uchunguzi huru ni muhimu.

Ni dhahiri kuwa wengi wasio na hatia wanauwawa.

Kama Serengeti tusishangae kusikia maandamano ya kubumba na pongezi badala ya watu kuwajibishwa.
 
Umepiga nyundo kwenye msumari haswaaaa!!!.

Watz ni mambumbu sana ktk masuala ya Sheria na haki. Hebu fikiria mwanao kwa chuki tu mtaani kwako katajwa ni pants rodi, anachukuliwa na kwenda kupgwa rusasi. Urajisikuaje.
Mwanao anasoma chuo,au Yuko shule anatajwa vp ni panya road?
 
Kumbe panya road wanatumiwa na wanasiasa fulani kuvuruga amani ya nchi? Maana panya road wakiachiwa, wananchi wanalalamika, panya road wakikamatwa na kushughulikiwa wengine wanapiga kelele haki zao za binadamu zimekiukwa. Nani yuko nyuma ya panya road? Ukitaka kujibu hilo swali jiulize nani anafaidika na panya road.
 
Kaka Nondo, hongera kwa kujaribu kujenga hoja. Ila hii 'story' yako inakosa kitu muhimu. Haija balance.

1. Una facts za ulichokiandika au ulisimuliwa ulipotembelea 'location?'
2. Kwa mfano, una uhakika hiyo reasonable force ilitumika katika mazingira unayoamini?Maana umeitafsiri reasonable force kirahisi na siyo kulingana na nature ya tukio. Vipi kama mtuhumiwa alitaka kumuua askari na askari alikuwa katika POINT OF NO RETURN? #Twende taratibu. Usalama wa raia na mali zao ni muhimu. Tuzuie uhalifu.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Polisi fanyeni kazi inatakiwa huyu nondo na moka zake za tandika atembelee familia 200 tatu tu anatujazia ibara za katiba na kiingereza kingi hapa
 
Reactions: EEX
Marehemu J. Nyerere wakati wa uhai wake kipindi Iddi A. Dadaa liyekuwa rais wa Uganda, Iddi Amin alianzisha chokochoko ; mara apige mabomu, mara atukane,mara atoe vitisho n.k. Ikafika mahali mwl. Nyerere akajikuta amefikia POINT OF NO RETURN na akaamuru huyu Jamaa Nduli achapwe. Mara paap! Mataifa wakaanza kumpigia kelele oh. unavunja haki za kibinadamu. Mwl.aliwajibu kwamba Nduli alipokuwa anatutendea visivyo nyie mlikaa kimya hata tulipopiga kelele hamkutoa walau tamko lolote. Sasa nyamazeni .... Ni sawa na hii ya panya rodi.Raia waathirika walipiga kelele sana dhidi ya vitendo vya panya rodi lakini hakuna aliyekemea- watu walikaa kimya kana kwamba panya rodi wameshindikana.Sasa panya rodi wanaadabishwa tayari chap wanajitokeza wenye kuijua sheria na maneno mengi.
Ingefaa ukimya uliokuwepo uendelee wakati ni zamu ya Serikali nayo kuonesha kwamba ipo tena ipo hai.
 
Nimekuelewa mno. Sahihi.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Wakati Watu wanauwawa na panya road sikuona Uzi wako mtoa mada
 
Shangailieni tuu huo ujinga, next time special operation ikiwahusu kwa sababu wakuu hawajapendezwa na maoni yenu au matendo yenu msije humu kulalamika, mtu anakamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi hana bunduki wala silaha yeyote then anaishia kuwa maiti na wengi wenu humu mnaona sawa tuu na kuunga mkono, wote akili zenu zimeruka na madhara ya kuishi manchi ya kimaskini yasiyofuata haki na wote hamna tofauti na hao panya road, muongezewe tozo tuu maana hamna akili
 
Kama ndivyo hivyo ,basi sheria zibadilishwe ili Polisi wawe wakikamata wanaua ,na haya mambo ya kukamata na kupeleleza, kushtaki mahakamani yaishe .Kama mnaona sheria ni Butu basi mzibadili . Unawezaje kumpiga Risasi Mtuhumiwa? Huku Chombo Cha kuthibitisha uhalifu wako ni Mahakama?
 
Mambo yaende kisheria sio nguvu, Sheria zirekebishwe kutoa adhabu kali kwa uhalifu. Sio mabavu yatumike...
Yes, kama kuna watuhumiwa wamekamatwa sheria ifuatwe wapelekwe kushtakiwa mahakamani kwa mujibu wa sheria sio kupiga Risasi. Tusitee watuhumiwa kuuwawa ni hatari Sana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…