Tuelezeke mkuu.Ni rahisi, pia nimegundua unaweza kuunda huo ubao mwenyewe na sio lazima kununua au kuagiza. Ila kuna maneno ya kusema wakati wa kuanza zoezi la kuita Spirit husika
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuelezeke mkuu.Ni rahisi, pia nimegundua unaweza kuunda huo ubao mwenyewe na sio lazima kununua au kuagiza. Ila kuna maneno ya kusema wakati wa kuanza zoezi la kuita Spirit husika
Mkuu karibu, pia zipo njia nyingi za kucheza na hao viumbe sio hiyo moja tuMkuu nakuja PM unipe maelezo.
Nataka kujaribu na napenda kinyama kucheza na hivyo viumbe🤭🤭🤭.
tupe ABCNi rahisi, pia nimegundua unaweza kuunda huo ubao mwenyewe na sio lazima kununua au kuagiza. Ila kuna maneno ya kusema wakati wa kuanza zoezi la kuita Spirit husika
Ili kutimiza utafiti ni lazima kupitia changamoto kadhaa, nilijua ni hatari lakini sikusita kujaribuwee jifanye mtafiti tu professor kidevu!!!,,,ipo siku litakukuta jambo!!
Mjasiliamali naona unajaribu kuwashawishi raia uwaagizie vibao vya oujia board kupitia AmazonHabari za wakati huu wana jukwaa
Duniani hatupo pekeyetu, vipo viumbe au roho ambazo kwa macho hatuwezi kuziona, zipo katika dimension nyingine, lakini ipo namna tunaweza kuwasiliana au kutengeneza ukaribu nao.
Swala hili halina uhusiano wowote na imani yangu bali ni jambo ambalo niliona katika baadhi ya harakati na tafiti zangu binafsi, kujaribu na kudadisi mambo mapya ni moja ya hulka na tabia yangu.
OUJIA board ni nini?
View attachment 3045441
Ni kipande au ubao ulio undwa kwa mbao na kuandikwa kwa mpangilio wa herufi na namba ambazo hutumika kuita au kufanya mawasiliano na roho za giza. Upande wa kushoto kuna neno YES na upande wa kulia NO, upande wa chini lipo neno linalo someka GOOD BYE.
Ubao huu huambatana na kitufe au kipande kidogo cha mbao ambacho huitwa planchettes, hii hutumika kama pointer, kimbao hicho huwa na umbo la kopa na kishimo kidogo katikati yake.
Matumizi ya vitu hivi viwili yana lengo la kutafuta au kuita roho ambazo zipo karibu yetu katika mazingira tuliyopo kwa wakati huo kwa kuzungusha kipande kidogo juu ya ubao wa OUJiA board.
Baada ya kufuatilia kwa ukaribu mchezo huu na kugundua una uhalisia na kuleta matokeo, ndipo na mimi nikaona ni vyema kujaribu na kujua ni nini hasa hutokea au huonekana.
Nilikuwa na rafiki ambaye anajihusisha na uagizaji wa bidhaa katika soko la Amazon, ndipo nikamuomba tufanye order ya OUJIA board, nilifanikiwa kuipata bidhaa ikiwa katika hali nzuri kama yalivyokuwa matarajio yangu.
Nilikaa nayo kwa muda mrefu pasipo kujaribu kuitumia, sababu ni bado nilikuwa najifunza kwa kutazama videos ili nijue njia sahihi ya kutumia ubao huo. Japo katika video hizo niliona matukio ya kutisha lakini bado niliamini naweza kufanya kwa usahihi bila kupata au kuona madhara yoyote.
Mnamo tarehe 24/ 11/2022, baada ya kurejea nyumbani Mida ya saa tatu usiku, ndipo nikatoa ubao ule na kuutazama kwa dakika kadhaa, nikaona hii ndyo siku sahihi ya kufanya majaribio.
Nikauchukua ubao na kuuweka chini, nikawasha mishumaa mitatu na kuiweka pande tofauti yani mbele, nyuma na pembezoni mwa ubao. Nikatia nia na kufungua zoezi kwa kutamka maneno maalum. Hofu ilinijaa lakini sikusita kwani tayari nilikuwa na kusudi la kujaribu.
Nilianza kuzungusha kipande kidogo cha mbao katika herufi na namba zilizoandikwa katika OUJIA board, sikuona wala kusika chochote. Nikajaribu tena kwa mara nyingine huku nikiuliza kwa sauti "Is there any presence of spirits? " Am I alone? "
Nilichagua kutumia Lugha ya kingereza kwa kuhofia labda kiswahili kinaweza sababisha nikaita vigagura au vibwengo vya kiswahili. Wakati bado nazungusha kipande cha mbao (pointer) juu ya ubao, ndipo nikahisi kuna sauti nasikia bila kujua zinatoka wapi.
Nilihisi labda ni woga tu niliokuwa nao, niligeuka nyuma na sikuona kitu, lakini bado nilihisi sauti na upepo kutokea upande wa nyuma. mkono wangu uliokua juu ya ubao ukaanza kusogea bila idhini yangu, hapo nikajua tayari nimepata ugeni.
Nikauliza "what is your name"? Mkono ukasogeza ile pointer mpaka kwenye herufi "J", nikauliza "how old are you" pointer ikajisogeza yenyewe wakati nimeishika mapaka kwenye namba 34.
Nikauliza "do you wish to harm or attack me" pointer ikasogea Mpaka upande ulio andikwa NO. Bado nikawa nahisi upepo au hewa kali inatokea upande wa nyuma nilipokuwa nimekaa, lakini nikigeuka sioni kitu.
Uoga ulinizidi kwani ilikuwa ni usiku sana na nilikuwa pekeyangu, nikaamua nisitishe zoezi na kumalizia mchezo.
Kwa utaratibu wa mchezo huu, baada ya kutosheka na maongezi na Spirit husika, unapaswa kusogeza pointer katika maneno yaliyo andikwa Good bye ili kuruhusu roho hiyo kuondoka na kumaliza game, lakini nilishindwa kufanya hivyo kwani mkono ulikuwa hauwezi kabisa kusogeza kile kibao.
Nikatoa mkono na kuacha ile pointer, ajabu ni kwamba ilianza kuzunguka yenyewe na kurejea kwenye herufi 'J' kisha namba 34. Ubao niliuweka chini kabisa hivyo usidhani kwamba labda ulikuwa kwenye meza na chini kuna sumaku au kitu kingine. Ni kweli kabisa niliona pointer inazunguka yenyewe juu ya ubao pasipo kuguswa na mtu.
Niliogopa sana na nilifanikiwa kutoka nje haraka. Siku ile sijarudi nyumbani kabisa na nikaenda kulala kwa rafiki. Nilipo rejea asubuhi nikachukua ubao ule na nikautupa, ila badae niliurejea na kuuchoma moto kabisa.
Nadhani nilikosea sheria au taratibu za mchezo, pia niligundua sio jambo sahihi kutafuta mawasiliano au ukaribu na roho za giza. Kuanzia siku hiyo mpaka leo, nikilala kwenye chumba changu naota lakini sikumbuki ndoto yoyote, tofauti na sehemu nyingine. Nahisi bado kuna tatzo ndani ya chumba changu, itabidi nihame nijaribu sehemu nyingine.
Hili tukio ni la kweli na nilikutana nalo wala sio hadithi au story ya kutunga, kama yupo atakaye hitaji kujaribu, nipo tayari kumpa maelekezo lakini atambue kwamba ni mchezo hatari sana na sio vyema kuufanya ukiwa pekeyako.
Shukran kwa kusoma andiko hili, karibu share maoni au experience yako kuhusu OUJIA board.
View attachment 3045421
_______________________
#BM
Mkuu nilivyo utupa ubao, nikasoma sehemu nikaona napaswa kuuchoma moto kabisa, lakini bado nahisi sijamaliza kazi.Kosa kubwa!
Kwanza kwa kucheza mchezo huu hatari kabisa na pili.
Kwa kutokusema Goodbye kwa ile roho ya kuzimu uliyokuwa unazungumza nayo! Ulifanya kosa kutupa Uija Board bila kuaga huyo mgeni kwa hiyo haendi anabaki na wewe mpaka uje utumie njia za kumdhibiti huyo roho na anaweza kuita wenzake wengi tu wakakutesa sana. Maadamau unajua jina lake na jinsi alivyokuja basi itakuwa rahisi kumtoa.
Hiyo roho kama unavyosema unajisikia kwamba kuna mauzauza hapo chumbani ni kweli na hata kama ukihama hapo bado utakuwa na shida kwani hiyo roho haipo hapo chumbani, ipo ndani yako, katika mwili wako.
Ni somo refu, au labda siku niandae uzi maalum kwaajili ya mafunzo na taratibu za kufuata kucheza na ubao huutupe ABC
Niache nijaribu kwanza mkuu mi jasiri 😹😹Utauponza kivivi hivi
Saivi siwezi kununua tena, najua namna ya kutengeneza mwenyeweNunua ubao mwingine ujaribu tena
Aaaah video au picha ya wale khudam achana nayo.Maana ni side effect yao walipokujaNataka nijue na ile mijini ya kipemba uliyonisimulia, halafu video hujatuma.!!
Dadavua mkuu mimi nataka niviite vibwengo na vigagu wa kiswahiliNi rahisi, pia nimegundua unaweza kuunda huo ubao mwenyewe na sio lazima kununua au kuagiza. Ila kuna maneno ya kusema wakati wa kuanza zoezi la kuita Spirit husika
Utanijuza utakayokutana nayo 🚶🚶Niache nijaribu kwanza mkuu mi jasiri 😹😹
Hujakoma 😹😹😹Mkuu nakuja PM unipe maelezo.
Nataka kujaribu na napenda kinyama kucheza na hivyo viumbe🤭🤭🤭.
Aaaaah kumbe na ww ni mtaalamu 😂😂😂😂Hujakoma 😹😹😹
Hamna 😂😂😂😂kuna raha we hujui tu.Hujakoma 😹😹😹
Si ungeongea tu kibongo ingekuj mizimu ya babu yako,huenda ingekupa mchongoNilichagua kutumia Lugha ya kingereza kwa kuhofia labda kiswahili kinaweza sababisha nikaita vigagura au vibwengo vya kiswahili.
Tena ashukuru aliita wazungu wastaarabu, angeita vibwengo vya kiswahili ss hivi angekuwa anaokota makopo 😹😹Kosa kubwa!
Kwanza kwa kucheza mchezo huu hatari kabisa na pili.
Kwa kutokusema Goodbye kwa ile roho ya kuzimu uliyokuwa unazungumza nayo! Ulifanya kosa kutupa Uija Board bila kuaga huyo mgeni kwa hiyo haendi anabaki na wewe mpaka uje utumie njia za kumdhibiti huyo roho na anaweza kuita wenzake wengi tu wakakutesa sana. Maadamau unajua jina lake na jinsi alivyokuja basi itakuwa rahisi kumtoa.
Hiyo roho kama unavyosema unajisikia kwamba kuna mauzauza hapo chumbani ni kweli na hata kama ukihama hapo bado utakuwa na shida kwani hiyo roho haipo hapo chumbani, ipo ndani yako, katika mwili wako.
Aiseee sio poaSi ungeongea tu kibongo ingekuj mizimu ya babu yako,huenda ingekupa mchongo