Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
- Thread starter
- #81
Mkuu ni wewe tu na maamuzi yako, ila uwe makini kwani wapo walio ingiwa na mapepo na hayajatoka kabisaMkuu mbona kama vile umenishawishi nami nitest nione mambo yakoje
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu ni wewe tu na maamuzi yako, ila uwe makini kwani wapo walio ingiwa na mapepo na hayajatoka kabisaMkuu mbona kama vile umenishawishi nami nitest nione mambo yakoje
Ungepiga kiluga au kiswahili au maSharti haya ruhusuHabari za wakati huu wana jukwaa
Duniani hatupo pekeyetu, vipo viumbe au roho ambazo kwa macho hatuwezi kuziona, zipo katika dimension nyingine, lakini ipo namna tunaweza kuwasiliana au kutengeneza ukaribu nao.
Swala hili halina uhusiano wowote na imani yangu bali ni jambo ambalo niliona katika baadhi ya harakati na tafiti zangu binafsi, kujaribu na kudadisi mambo mapya ni moja ya hulka na tabia yangu.
OUJIA board ni nini?
View attachment 3045441
Ni kipande au ubao ulio undwa kwa mbao na kuandikwa kwa mpangilio wa herufi na namba ambazo hutumika kuita au kufanya mawasiliano na roho za giza. Upande wa kushoto kuna neno YES na upande wa kulia NO, upande wa chini lipo neno linalo someka GOOD BYE.
Ubao huu huambatana na kitufe au kipande kidogo cha mbao ambacho huitwa planchettes, hii hutumika kama pointer, kimbao hicho huwa na umbo la kopa na kishimo kidogo katikati yake.
Matumizi ya vitu hivi viwili yana lengo la kutafuta au kuita roho ambazo zipo karibu yetu katika mazingira tuliyopo kwa wakati huo kwa kuzungusha kipande kidogo juu ya ubao wa OUJiA board.
Baada ya kufuatilia kwa ukaribu mchezo huu na kugundua una uhalisia na kuleta matokeo, ndipo na mimi nikaona ni vyema kujaribu na kujua ni nini hasa hutokea au huonekana.
Nilikuwa na rafiki ambaye anajihusisha na uagizaji wa bidhaa katika soko la Amazon, ndipo nikamuomba tufanye order ya OUJIA board, nilifanikiwa kuipata bidhaa ikiwa katika hali nzuri kama yalivyokuwa matarajio yangu.
Nilikaa nayo kwa muda mrefu pasipo kujaribu kuitumia, sababu ni bado nilikuwa najifunza kwa kutazama videos ili nijue njia sahihi ya kutumia ubao huo. Japo katika video hizo niliona matukio ya kutisha lakini bado niliamini naweza kufanya kwa usahihi bila kupata au kuona madhara yoyote.
Mnamo tarehe 24/ 11/2022, baada ya kurejea nyumbani Mida ya saa tatu usiku, ndipo nikatoa ubao ule na kuutazama kwa dakika kadhaa, nikaona hii ndyo siku sahihi ya kufanya majaribio.
Nikauchukua ubao na kuuweka chini, nikawasha mishumaa mitatu na kuiweka pande tofauti yani mbele, nyuma na pembezoni mwa ubao. Nikatia nia na kufungua zoezi kwa kutamka maneno maalum. Hofu ilinijaa lakini sikusita kwani tayari nilikuwa na kusudi la kujaribu.
Nilianza kuzungusha kipande kidogo cha mbao katika herufi na namba zilizoandikwa katika OUJIA board, sikuona wala kusika chochote. Nikajaribu tena kwa mara nyingine huku nikiuliza kwa sauti "Is there any presence of spirits? " Am I alone? "
Nilichagua kutumia Lugha ya kingereza kwa kuhofia labda kiswahili kinaweza sababisha nikaita vigagura au vibwengo vya kiswahili. Wakati bado nazungusha kipande cha mbao (pointer) juu ya ubao, ndipo nikahisi kuna sauti nasikia bila kujua zinatoka wapi.
Nilihisi labda ni woga tu niliokuwa nao, niligeuka nyuma na sikuona kitu, lakini bado nilihisi sauti na upepo kutokea upande wa nyuma. mkono wangu uliokua juu ya ubao ukaanza kusogea bila idhini yangu, hapo nikajua tayari nimepata ugeni.
Nikauliza "what is your name"? Mkono ukasogeza ile pointer mpaka kwenye herufi "J", nikauliza "how old are you" pointer ikajisogeza yenyewe wakati nimeishika mapaka kwenye namba 34.
Nikauliza "do you wish to harm or attack me" pointer ikasogea Mpaka upande ulio andikwa NO. Bado nikawa nahisi upepo au hewa kali inatokea upande wa nyuma nilipokuwa nimekaa, lakini nikigeuka sioni kitu.
Uoga ulinizidi kwani ilikuwa ni usiku sana na nilikuwa pekeyangu, nikaamua nisitishe zoezi na kumalizia mchezo.
Kwa utaratibu wa mchezo huu, baada ya kutosheka na maongezi na Spirit husika, unapaswa kusogeza pointer katika maneno yaliyo andikwa Good bye ili kuruhusu roho hiyo kuondoka na kumaliza game, lakini nilishindwa kufanya hivyo kwani mkono ulikuwa hauwezi kabisa kusogeza kile kibao.
Nikatoa mkono na kuacha ile pointer, ajabu ni kwamba ilianza kuzunguka yenyewe na kurejea kwenye herufi 'J' kisha namba 34. Ubao niliuweka chini kabisa hivyo usidhani kwamba labda ulikuwa kwenye meza na chini kuna sumaku au kitu kingine. Ni kweli kabisa niliona pointer inazunguka yenyewe juu ya ubao pasipo kuguswa na mtu.
Niliogopa sana na nilifanikiwa kutoka nje haraka. Siku ile sijarudi nyumbani kabisa na nikaenda kulala kwa rafiki. Nilipo rejea asubuhi nikachukua ubao ule na nikautupa, ila badae niliurejea na kuuchoma moto kabisa.
Nadhani nilikosea sheria au taratibu za mchezo, pia niligundua sio jambo sahihi kutafuta mawasiliano au ukaribu na roho za giza. Kuanzia siku hiyo mpaka leo, nikilala kwenye chumba changu naota lakini sikumbuki ndoto yoyote, tofauti na sehemu nyingine. Nahisi bado kuna tatzo ndani ya chumba changu, itabidi nihame nijaribu sehemu nyingine.
Hili tukio ni la kweli na nilikutana nalo wala sio hadithi au story ya kutunga, kama yupo atakaye hitaji kujaribu, nipo tayari kumpa maelekezo lakini atambue kwamba ni mchezo hatari sana na sio vyema kuufanya ukiwa pekeyako.
Shukran kwa kusoma andiko hili, karibu share maoni au experience yako kuhusu OUJIA board.
View attachment 3045421
_______________________
#BM
Ndiyo, ila kuna rangi ya kuchorea inauzwa kwenye maduka ya dawa asiliUtanitengenezea bure?
Yanaruhusu, ila nilihofia tu mizimu yetu maana haichelewi kutaka damuUngepiga kiluga au kiswahili au maSharti haya ruhusu
Siku nikikosa cha kutafiti na ruka na hii maana kwenye utafiti unapaswa utake riskMkuu ni wewe tu na maamuzi yako, ila uwe makini kwani wapo walio ingiwa na mapepo na hayajatoka kabisa
Limeisha tengeneza pesa ya rangi nakupa, kikubwa nione hivyo vibwengoNdiyo, ila kuna rangi ya kuchorea inauzwa kwenye maduka ya dawa asili
Halafu sio mbali ni mwaka huu tu mwanzoni.😹😹😹 Kwani walikufanyaje mbona husemi??
Jina lako na mwenendo wako vinashabianaMkuu mbona kama vile umenishawishi nami nitest nione mambo yakoje
Asitie neno kwanza, Afanye hilo jaribio then ndio aje kutia nenoHapa Kiranga lazima utie neno lako mkuu
Wewe sema tunazitafuta.Ndiyo, ila kuna rangi ya kuchorea inauzwa kwenye maduka ya dawa asili
Wewe ulichemka sana na bado umechemka, ile roho bado ipo na itakutafuta popote uwapo.Nilipata hofu sana mkuu, niliamua nimuache auende kwani nilihisi yupo na ananipuliza kwa upepo mkali
Hio tunaiita fursa ya kuverify the presence of witch crafts 😁😁Jina lako na mwenendo wako vinashabiana
Umeshaona fursa hiyo 😃
Mkuu saivi nasali sana, naamini hiyo ndiyo njia sahihi ya kujilinda na kuepukana na mabaya yoteWewe ulichemka sana na bado umechemka, ile roho bado ipo na itakutafuta popote uwapo.
Uliwaita majini ya kike na upwiru wako, wamekuja kukuonyesha show unawafukuza 😹😹😹Halafu sio mbali ni mwaka huu tu mwanzoni.
Yule ndugu yangu alinifundisha kusoma qassam maana si unajua Wapemba kwa kusoma dini!?
Akanifundisha kama nne ambazo unawaita wafuatao;
-Aswaarul kabiir.
-Arruuhaniyyah.
-Maimanah.
-Hamamah.
Mie nilisoma ya arruhaaniyyah hawa huwa ni wa kiroho mara nyingi huja kwa kivuli,mpaka wakuzoee ndio huja kwa sura kabisa.
Kusoma kwake unatakiwa usome usiku katika giza ukiwa umewasha mshumaa wa kijani,mwekundu na njano,uwe na kitezo chenye moto uwe na ubani zuhra,jawi/uvumba na Zafarani.
Urefu wa hiyo azma ni kama karatasi moja,unasoma kwa idadi ya namba tasa.1,5,7 ila ukitaka wake haraka soma mara 71.
Mie nikasoma mara 71 halafu nikapitiwa usingizi.
Wakati wa alfajiri ile adhana inaadhiniwa nilishikwa mguu nikavutwa nikaamka.
Katika meza yangu ya vitabu vya dini niliona kivuli kinasoma vitabu vyangu wallahi kwa sauti.
Nilishtuka AISEE.
Sikuisoma tena.
Sasa kipindi nimeenda Morogoro kufuatilia ishu zangu nikawa nimelala nanenane pale mnadani kwa jamaa zangu.
Usiku nimelala ghafla nilishtuka nikaona wadada weupee wawili.
Mmoja kabla kama sista mavazi meupe mengine Meusi.
Sasa kila nikupige kelele wenzangu hawasikii,yule mweusi alivyotaka kuja nikamzuia kwa ishara ya mkono akasimama yule mweupe mbishi kila nikipunga mkono kumzuia anakuja,akalala kifuani kwangu akabusu mikono yangu,akanipapasa mapaja halafu akanitizamaa akasema kwaheri ila nitarudi tena.
Ghafla niliinuka juu nikarudi tena chini kwa nguvu nikapoteza fahamu.
Tunaamka asubuhi tunakuta maji mekundu usawa wa kizingiti cha mlango yana harufu kali ya marashi kama misk/musk halafu kila niliposhikwa na yule kiumbe PEUPEEE kama gypsum AISEE.
Ilichukua kama siku 5 mpaka ile rangi nyeupe kutoka nilivaa kanzu na gloves wiki nzima.
Mkuu sio jambo dogo kama unavyo dhania, mimi nilitumia karibia mwaka mzima kusoma na kudadisi namna ya utumiaji wa hiyo kitu.Wewe sema tunazitafuta.
Usiongee nusu nusu mdau toa full DESA hilo tulisome.
Tayari nimesha achana na hiyo kitu, saivi nafanya tafiti nyingineSisi tuliwahi kuucheza miaka ya 2006 huko, nadhani nitakupa dodosa na sheria zake soon, ukitaka kuacha, siyo kukimbia na kuchoma moto.