Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
- Thread starter
- #61
Maelezo niliyo andika yanaweza kukupa mwanga wa kuanzia, ila ni lazima uwe na ubao kwanzaDadavua mkuu mimi nataka niviite vibwengo na vigagu wa kiswahili
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maelezo niliyo andika yanaweza kukupa mwanga wa kuanzia, ila ni lazima uwe na ubao kwanzaDadavua mkuu mimi nataka niviite vibwengo na vigagu wa kiswahili
Tuelekeze namna ya kuunda mwenyewe huo ubao.Saivi siwezi kununua tena, najua namna ya kutengeneza mwenyewe
Tatzo mizimu ya kibongo haina ustaarabu na inaweza kusema niipe damu za kukuSi ungeongea tu kibongo ingekuj mizimu ya babu yako,huenda ingekupa mchongo
😹😹😹 Kwani walikufanyaje mbona husemi??Aaaah video au picha ya wale khudam achana nayo.Maana ni side effect yao walipokuja
Ngojea tujaribu hili hapa halafu tuone inatiki🤭🤭🤭.
😹😹😹Utanijuza utakayokutana nayo 🚶🚶
Ouija board ni moja ya hizo wanaita "portals" au malango ya kukutana na roho za giza. Inaonekana kama kamchezo poa tu ila ni strategy ya Giza ya kuwapata watu. Pamoja na kuchoma kibao kitu ambacho kimsingi kinaashiria kuachana na mchezo huo, ujue kuwa yule uliyemwita hujafanya taratibu zake kisheria za kumrudisha alipotoka. Kuna kitu unapaswa kufanya uwe huru.Mkuu nilivyo utupa ubao, nikasoma sehemu nikaona napaswa kuuchoma moto kabisa, lakini bado nahisi sijamaliza kazi.
Ila nitahama na kujaribu sehemu nyingine nione kama bado mauzauza yataendelea
Hapana ndio nataka nijifunze 😹😹😹Aaaaah kumbe na ww ni mtaalamu 😂😂😂😂
Sasa mbona huleti maujuzi hayo na sie tupate hiyo raha? 😹😹😹Hamna 😂😂😂😂kuna raha we hujui tu.
Kama unavyo uona katika picha, ni ubao wa mbao halisi ya mti, na kuna rangi maalum kwaajili ya kuandikia hayo maandishi. Unaweza uka copy kutoka kwenye picha ya mfano.Tuelekeze namna ya kuunda mwenyewe huo ubao.
Umeongea kikomavu mno.Njia yoyote ambayo haimkufuru Mungu waweza kutumia ilimradi ufanikiwe the bad thing is to die broke while there's a lot of ways to make money.
Oyaaaa ko kimeumana kwa huyo mtoa mada aisee 😂😂😂🙌🙌Ouija board ni moja ya hizo wanaita "portals" au malango ya kukutana na roho za giza. Inaonekana kama kamchezo poa tu ila ni strategy ya Giza ya kuwapata watu. Pamoja na kuchoma kibao kitu ambacho kimsingi kinaashiria kuachana na mchezo huo, ujue kuwa yule uliyemwita hujafanya taratibu zake kisheria za kumrudisha alipotoka. Kuna kitu unapaswa kufanya uwe huru.
Niekekeze jinsi ya kuutengeneza si umesema unajua haina haja ya kuagiza AmazonMaelezo niliyo andika yanaweza kukupa mwanga wa kuanzia, ila ni lazima uwe na ubao kwanza
Nipo huru, lakini sina imani tu na chumba changu.Nimesha jaribu mambo mengine ya kutisha zaidi kuliko hilo, pia kwa sasa nimeacha na nimezidisha maombi na salaPamoja na kuchoma kibao kitu ambacho kimsingi kinaashiria kuachana na mchezo huo, ujue kuwa yule uliyemwita hujafanya taratibu zake kisheria za kumrudisha alipotoka. Kuna kitu unapaswa kufanya uwe huru.
You are on good track endelea.Nipo huru, lakini sina imani tu na chumba changu.Nimesha jaribu mambo mengine ya kutisha zaidi kuliko hilo, pia kwa sasa nimeacha na nimezidisha maombi na sala
Kuna movie niliangalia inaitwa Jumanji nayo iko km hiyo anayoelezea mtoa mada.!!Ouija board ni moja ya hizo wanaita "portals" au malango ya kukutana na roho za giza. Inaonekana kama kamchezo poa tu ila ni strategy ya Giza ya kuwapata watu. Pamoja na kuchoma kibao kitu ambacho kimsingi kinaashiria kuachana na mchezo huo, ujue kuwa yule uliyemwita hujafanya taratibu zake kisheria za kumrudisha alipotoka. Kuna kitu unapaswa kufanya uwe huru.
Kukuelekeza kwa maandishi sidhani kama itatosha, labda unipe oda nitengeneze nikupeNiekekeze jinsi ya kuutengeneza si umesema unajua haina haja ya kuagiza Amazon
Mkuu mbona hakuna dalili za kulogana hapaUchaguzi umekaribia msimu wa kulogana umeanza.
Mkuu mbona kama vile umenishawishi nami nitest nione mambo yakojeHabari za wakati huu wana jukwaa
Duniani hatupo pekeyetu, vipo viumbe au roho ambazo kwa macho hatuwezi kuziona, zipo katika dimension nyingine, lakini ipo namna tunaweza kuwasiliana au kutengeneza ukaribu nao.
Swala hili halina uhusiano wowote na imani yangu bali ni jambo ambalo niliona katika baadhi ya harakati na tafiti zangu binafsi, kujaribu na kudadisi mambo mapya ni moja ya hulka na tabia yangu.
OUJIA board ni nini?
View attachment 3045441
Ni kipande au ubao ulio undwa kwa mbao na kuandikwa kwa mpangilio wa herufi na namba ambazo hutumika kuita au kufanya mawasiliano na roho za giza. Upande wa kushoto kuna neno YES na upande wa kulia NO, upande wa chini lipo neno linalo someka GOOD BYE.
Ubao huu huambatana na kitufe au kipande kidogo cha mbao ambacho huitwa planchettes, hii hutumika kama pointer, kimbao hicho huwa na umbo la kopa na kishimo kidogo katikati yake.
Matumizi ya vitu hivi viwili yana lengo la kutafuta au kuita roho ambazo zipo karibu yetu katika mazingira tuliyopo kwa wakati huo kwa kuzungusha kipande kidogo juu ya ubao wa OUJiA board.
Baada ya kufuatilia kwa ukaribu mchezo huu na kugundua una uhalisia na kuleta matokeo, ndipo na mimi nikaona ni vyema kujaribu na kujua ni nini hasa hutokea au huonekana.
Nilikuwa na rafiki ambaye anajihusisha na uagizaji wa bidhaa katika soko la Amazon, ndipo nikamuomba tufanye order ya OUJIA board, nilifanikiwa kuipata bidhaa ikiwa katika hali nzuri kama yalivyokuwa matarajio yangu.
Nilikaa nayo kwa muda mrefu pasipo kujaribu kuitumia, sababu ni bado nilikuwa najifunza kwa kutazama videos ili nijue njia sahihi ya kutumia ubao huo. Japo katika video hizo niliona matukio ya kutisha lakini bado niliamini naweza kufanya kwa usahihi bila kupata au kuona madhara yoyote.
Mnamo tarehe 24/ 11/2022, baada ya kurejea nyumbani Mida ya saa tatu usiku, ndipo nikatoa ubao ule na kuutazama kwa dakika kadhaa, nikaona hii ndyo siku sahihi ya kufanya majaribio.
Nikauchukua ubao na kuuweka chini, nikawasha mishumaa mitatu na kuiweka pande tofauti yani mbele, nyuma na pembezoni mwa ubao. Nikatia nia na kufungua zoezi kwa kutamka maneno maalum. Hofu ilinijaa lakini sikusita kwani tayari nilikuwa na kusudi la kujaribu.
Nilianza kuzungusha kipande kidogo cha mbao katika herufi na namba zilizoandikwa katika OUJIA board, sikuona wala kusika chochote. Nikajaribu tena kwa mara nyingine huku nikiuliza kwa sauti "Is there any presence of spirits? " Am I alone? "
Nilichagua kutumia Lugha ya kingereza kwa kuhofia labda kiswahili kinaweza sababisha nikaita vigagura au vibwengo vya kiswahili. Wakati bado nazungusha kipande cha mbao (pointer) juu ya ubao, ndipo nikahisi kuna sauti nasikia bila kujua zinatoka wapi.
Nilihisi labda ni woga tu niliokuwa nao, niligeuka nyuma na sikuona kitu, lakini bado nilihisi sauti na upepo kutokea upande wa nyuma. mkono wangu uliokua juu ya ubao ukaanza kusogea bila idhini yangu, hapo nikajua tayari nimepata ugeni.
Nikauliza "what is your name"? Mkono ukasogeza ile pointer mpaka kwenye herufi "J", nikauliza "how old are you" pointer ikajisogeza yenyewe wakati nimeishika mapaka kwenye namba 34.
Nikauliza "do you wish to harm or attack me" pointer ikasogea Mpaka upande ulio andikwa NO. Bado nikawa nahisi upepo au hewa kali inatokea upande wa nyuma nilipokuwa nimekaa, lakini nikigeuka sioni kitu.
Uoga ulinizidi kwani ilikuwa ni usiku sana na nilikuwa pekeyangu, nikaamua nisitishe zoezi na kumalizia mchezo.
Kwa utaratibu wa mchezo huu, baada ya kutosheka na maongezi na Spirit husika, unapaswa kusogeza pointer katika maneno yaliyo andikwa Good bye ili kuruhusu roho hiyo kuondoka na kumaliza game, lakini nilishindwa kufanya hivyo kwani mkono ulikuwa hauwezi kabisa kusogeza kile kibao.
Nikatoa mkono na kuacha ile pointer, ajabu ni kwamba ilianza kuzunguka yenyewe na kurejea kwenye herufi 'J' kisha namba 34. Ubao niliuweka chini kabisa hivyo usidhani kwamba labda ulikuwa kwenye meza na chini kuna sumaku au kitu kingine. Ni kweli kabisa niliona pointer inazunguka yenyewe juu ya ubao pasipo kuguswa na mtu.
Niliogopa sana na nilifanikiwa kutoka nje haraka. Siku ile sijarudi nyumbani kabisa na nikaenda kulala kwa rafiki. Nilipo rejea asubuhi nikachukua ubao ule na nikautupa, ila badae niliurejea na kuuchoma moto kabisa.
Nadhani nilikosea sheria au taratibu za mchezo, pia niligundua sio jambo sahihi kutafuta mawasiliano au ukaribu na roho za giza. Kuanzia siku hiyo mpaka leo, nikilala kwenye chumba changu naota lakini sikumbuki ndoto yoyote, tofauti na sehemu nyingine. Nahisi bado kuna tatzo ndani ya chumba changu, itabidi nihame nijaribu sehemu nyingine.
Hili tukio ni la kweli na nilikutana nalo wala sio hadithi au story ya kutunga, kama yupo atakaye hitaji kujaribu, nipo tayari kumpa maelekezo lakini atambue kwamba ni mchezo hatari sana na sio vyema kuufanya ukiwa pekeyako.
Shukran kwa kusoma andiko hili, karibu share maoni au experience yako kuhusu OUJIA board.
View attachment 3045421
_______________________
#BM
Utanitengenezea bure?Kukuelekeza kwa maandishi sidhani kama itatosha, labda unipe oda nitengeneze nikupe