hermanthegreat
JF-Expert Member
- Mar 2, 2021
- 1,274
- 3,282
.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi ni OIJIA au OUIJA Board, ipi ni sahihi?Habari za wakati huu wana jukwaa
Duniani hatupo peke yetu, vipo viumbe au roho ambazo kwa macho hatuwezi kuziona, zipo katika dimension nyingine, lakini ipo namna tunaweza kuwasiliana au kutengeneza ukaribu nao.
Swala hili halina uhusiano wowote na imani yangu bali ni jambo ambalo niliona katika baadhi ya harakati na tafiti zangu binafsi, kujaribu na kudadisi mambo mapya ni moja ya hulka na tabia yangu.
OUJIA board ni nini?
View attachment 3045441
Ni kipande au ubao ulioundwa kwa mbao na kuandikwa kwa mpangilio wa herufi na namba ambazo hutumika kuita au kufanya mawasiliano na roho za giza. Upande wa kushoto kuna neno YES na upande wa kulia NO, upande wa chini lipo neno linalo someka GOOD BYE.
Ubao huu huambatana na kitufe au kipande kidogo cha mbao ambacho huitwa planchettes, hii hutumika kama pointer, kimbao hicho huwa na umbo la kopa na kishimo kidogo katikati yake.
Matumizi ya vitu hivi viwili yana lengo la kutafuta au kuita roho ambazo zipo karibu yetu katika mazingira tuliyopo kwa wakati huo kwa kuzungusha kipande kidogo juu ya ubao wa OUJiA board.
Baada ya kufuatilia kwa ukaribu mchezo huu na kugundua una uhalisia na kuleta matokeo, ndipo na mimi nikaona ni vyema kujaribu na kujua ni nini hasa hutokea au huonekana.
Nilikuwa na rafiki ambaye anajihusisha na uagizaji wa bidhaa katika soko la Amazon, ndipo nikamuomba tufanye order ya OUJIA board, nilifanikiwa kuipata bidhaa ikiwa katika hali nzuri kama yalivyokuwa matarajio yangu.
Nilikaa nayo kwa muda mrefu pasipo kujaribu kuitumia, sababu ni bado nilikuwa najifunza kwa kutazama videos ili nijue njia sahihi ya kutumia ubao huo. Japo katika video hizo niliona matukio ya kutisha lakini bado niliamini naweza kufanya kwa usahihi bila kupata au kuona madhara yoyote.
Mnamo tarehe 24/ 11/2022, baada ya kurejea nyumbani Mida ya saa tatu usiku, ndipo nikatoa ubao ule na kuutazama kwa dakika kadhaa, nikaona hii ndyo siku sahihi ya kufanya majaribio.
Nikauchukua ubao na kuuweka chini, nikawasha mishumaa mitatu na kuiweka pande tofauti yani mbele, nyuma na pembezoni mwa ubao. Nikatia nia na kufungua zoezi kwa kutamka maneno maalum. Hofu ilinijaa lakini sikusita kwani tayari nilikuwa na kusudi la kujaribu.
Nilianza kuzungusha kipande kidogo cha mbao katika herufi na namba zilizoandikwa katika OUJIA board, sikuona wala kusika chochote. Nikajaribu tena kwa mara nyingine huku nikiuliza kwa sauti "Is there any presence of spirits? " Am I alone? "
Nilichagua kutumia Lugha ya kingereza kwa kuhofia labda kiswahili kinaweza sababisha nikaita vigagura au vibwengo vya kiswahili. Wakati bado nazungusha kipande cha mbao (pointer) juu ya ubao, ndipo nikahisi kuna sauti nasikia bila kujua zinatoka wapi.
Nilihisi labda ni woga tu niliokuwa nao, niligeuka nyuma na sikuona kitu, lakini bado nilihisi sauti na upepo kutokea upande wa nyuma. mkono wangu uliokua juu ya ubao ukaanza kusogea bila idhini yangu, hapo nikajua tayari nimepata ugeni.
Nikauliza "what is your name"? Mkono ukasogeza ile pointer mpaka kwenye herufi "J", nikauliza "how old are you" pointer ikajisogeza yenyewe wakati nimeishika mpaka kwenye namba 34.
Nikauliza "do you wish to harm or attack me" pointer ikasogea Mpaka upande ulio andikwa NO. Bado nikawa nahisi upepo au hewa kali inatokea upande wa nyuma nilipokuwa nimekaa, lakini nikigeuka sioni kitu.
Uoga ulinizidi kwani ilikuwa ni usiku sana na nilikuwa pekeyangu, nikaamua nisitishe zoezi na kumalizia mchezo.
Kwa utaratibu wa mchezo huu, baada ya kutosheka na maongezi na Spirit husika, unapaswa kusogeza pointer katika maneno yaliyo andikwa Good bye ili kuruhusu roho hiyo kuondoka na kumaliza game, lakini nilishindwa kufanya hivyo kwani mkono ulikuwa hauwezi kabisa kusogeza kile kibao.
Nikatoa mkono na kuacha ile pointer, ajabu ni kwamba ilianza kuzunguka yenyewe na kurejea kwenye herufi 'J' kisha namba 34. Ubao niliuweka chini kabisa hivyo usidhani kwamba labda ulikuwa kwenye meza na chini kuna sumaku au kitu kingine. Ni kweli kabisa niliona pointer inazunguka yenyewe juu ya ubao pasipo kuguswa na mtu.
Niliogopa sana na nilifanikiwa kutoka nje haraka. Siku ile sijarudi nyumbani kabisa na nikaenda kulala kwa rafiki. Nilipo rejea asubuhi nikachukua ubao ule na nikautupa, ila badae niliurejea na kuuchoma moto kabisa.
Nadhani nilikosea sheria au taratibu za mchezo, pia niligundua sio jambo sahihi kutafuta mawasiliano au ukaribu na roho za giza. Kuanzia siku hiyo mpaka leo, nikilala kwenye chumba changu naota lakini sikumbuki ndoto yoyote, tofauti na sehemu nyingine. Nahisi bado kuna tatzo ndani ya chumba changu, itabidi nihame nijaribu sehemu nyingine.
Hili tukio ni la kweli na nilikutana nalo wala sio hadithi au story ya kutunga, kama yupo atakaye hitaji kujaribu, nipo tayari kumpa maelekezo lakini atambue kwamba ni mchezo hatari sana na sio vyema kuufanya ukiwa pekeyako.
Shukran kwa kusoma andiko hili, karibu share maoni au experience yako kuhusu OUJIA board.
View attachment 3045421
______________________
#BM
Nataka nihame kabisa hii nyumbaHicho chumba kiko "haunted". Ule mzimu bado haujaondoka kwa vile hukuuaga. Tahadhari kabla ya hatari.
OUJIAHivi ni OIJIA au OUIJA Board, ipi ni sahihi?
Mkuu ubao uliupata wapi au ulitengeneza mwenyewe?Hii Ouja ni hatari mm nilisummon akaja Roho mmoja tukawa tunaongea nikamuuliza una umri gani akaniambia miaka mia nne nikamuuliza naomba nikuulize historia ya miaka hiyo akanipa sharti mmoja akaniambia niende chooni nipake yale maji ya choo mwili mzima ndio atanisimulia nikamuambia hakuna njia nyingine akasema unaona uchafu nikamwambia siwezi akanisonya nikamcomand kwa sauti ya mamlaka ya juu ile sauti kali huku nikimwambia maneno yafuatayo ya kishetani Zay Zay Zay Laa Hassh alitoka baruti huyo kwa maaana hayo maneno yana nguvu alisema unataka kuniunguza wakati mm sio mbaya ni mtu poa akakimbia
Noma sana!Mkuu ubao uliupata wapi au ulitengeneza mwenyewe?
Sawa mkuu. Dm ipo wazi hakika.Leo usiku au asubuhi nakurushia qassam za kusoma.
Kwa Tanzania sidhani ila nina baba yangu mdogo yupo Nertheland ananipenda sana kila akija lazima aniletee zawadi hivyo nikawa vitu vingi au vitabu vingi ambavyo huku havipatikani huwa namuagiza ananileteaMkuu ubao uliupata wapi au ulitengeneza mwenyewe?
Sawa Mkuu, lakini huu mchezo sio salama kabisaKwa Tanzania sidhani ila nina baba yangu mdogo yupo Nertheland ananipenda sana kila akija lazima aniletee zawadi hivyo nikawa vitu vingi au vitabu vingi ambavyo huku havipatikani huwa namuagiza ananiletea
Kibwegu hana pa kukaa anaitwa getto ana kuja ndo alete pesa 😹😹Badala ungemtuma huyo kibwengu akazoe pesa akuletee wewe unacheza naye tu.
Unazitafuta nguvu za giza halafu unaogopa mwenyewe, ulizitafuuta za nini?Habari za wakati huu wana jukwaa
Duniani hatupo peke yetu, vipo viumbe au roho ambazo kwa macho hatuwezi kuziona, zipo katika dimension nyingine, lakini ipo namna tunaweza kuwasiliana au kutengeneza ukaribu nao.
Swala hili halina uhusiano wowote na imani yangu bali ni jambo ambalo niliona katika baadhi ya harakati na tafiti zangu binafsi, kujaribu na kudadisi mambo mapya ni moja ya hulka na tabia yangu.
OUJIA board ni nini?
View attachment 3045441
Ni kipande au ubao ulioundwa kwa mbao na kuandikwa kwa mpangilio wa herufi na namba ambazo hutumika kuita au kufanya mawasiliano na roho za giza. Upande wa kushoto kuna neno YES na upande wa kulia NO, upande wa chini lipo neno linalo someka GOOD BYE.
Ubao huu huambatana na kitufe au kipande kidogo cha mbao ambacho huitwa planchettes, hii hutumika kama pointer, kimbao hicho huwa na umbo la kopa na kishimo kidogo katikati yake.
Matumizi ya vitu hivi viwili yana lengo la kutafuta au kuita roho ambazo zipo karibu yetu katika mazingira tuliyopo kwa wakati huo kwa kuzungusha kipande kidogo juu ya ubao wa OUJiA board.
Baada ya kufuatilia kwa ukaribu mchezo huu na kugundua una uhalisia na kuleta matokeo, ndipo na mimi nikaona ni vyema kujaribu na kujua ni nini hasa hutokea au huonekana.
Nilikuwa na rafiki ambaye anajihusisha na uagizaji wa bidhaa katika soko la Amazon, ndipo nikamuomba tufanye order ya OUJIA board, nilifanikiwa kuipata bidhaa ikiwa katika hali nzuri kama yalivyokuwa matarajio yangu.
Nilikaa nayo kwa muda mrefu pasipo kujaribu kuitumia, sababu ni bado nilikuwa najifunza kwa kutazama videos ili nijue njia sahihi ya kutumia ubao huo. Japo katika video hizo niliona matukio ya kutisha lakini bado niliamini naweza kufanya kwa usahihi bila kupata au kuona madhara yoyote.
Mnamo tarehe 24/ 11/2022, baada ya kurejea nyumbani Mida ya saa tatu usiku, ndipo nikatoa ubao ule na kuutazama kwa dakika kadhaa, nikaona hii ndyo siku sahihi ya kufanya majaribio.
Nikauchukua ubao na kuuweka chini, nikawasha mishumaa mitatu na kuiweka pande tofauti yani mbele, nyuma na pembezoni mwa ubao. Nikatia nia na kufungua zoezi kwa kutamka maneno maalum. Hofu ilinijaa lakini sikusita kwani tayari nilikuwa na kusudi la kujaribu.
Nilianza kuzungusha kipande kidogo cha mbao katika herufi na namba zilizoandikwa katika OUJIA board, sikuona wala kusika chochote. Nikajaribu tena kwa mara nyingine huku nikiuliza kwa sauti "Is there any presence of spirits? " Am I alone? "
Nilichagua kutumia Lugha ya kingereza kwa kuhofia labda kiswahili kinaweza sababisha nikaita vigagura au vibwengo vya kiswahili. Wakati bado nazungusha kipande cha mbao (pointer) juu ya ubao, ndipo nikahisi kuna sauti nasikia bila kujua zinatoka wapi.
Nilihisi labda ni woga tu niliokuwa nao, niligeuka nyuma na sikuona kitu, lakini bado nilihisi sauti na upepo kutokea upande wa nyuma. mkono wangu uliokua juu ya ubao ukaanza kusogea bila idhini yangu, hapo nikajua tayari nimepata ugeni.
Nikauliza "what is your name"? Mkono ukasogeza ile pointer mpaka kwenye herufi "J", nikauliza "how old are you" pointer ikajisogeza yenyewe wakati nimeishika mpaka kwenye namba 34.
Nikauliza "do you wish to harm or attack me" pointer ikasogea Mpaka upande ulio andikwa NO. Bado nikawa nahisi upepo au hewa kali inatokea upande wa nyuma nilipokuwa nimekaa, lakini nikigeuka sioni kitu.
Uoga ulinizidi kwani ilikuwa ni usiku sana na nilikuwa pekeyangu, nikaamua nisitishe zoezi na kumalizia mchezo.
Kwa utaratibu wa mchezo huu, baada ya kutosheka na maongezi na Spirit husika, unapaswa kusogeza pointer katika maneno yaliyo andikwa Good bye ili kuruhusu roho hiyo kuondoka na kumaliza game, lakini nilishindwa kufanya hivyo kwani mkono ulikuwa hauwezi kabisa kusogeza kile kibao.
Nikatoa mkono na kuacha ile pointer, ajabu ni kwamba ilianza kuzunguka yenyewe na kurejea kwenye herufi 'J' kisha namba 34. Ubao niliuweka chini kabisa hivyo usidhani kwamba labda ulikuwa kwenye meza na chini kuna sumaku au kitu kingine. Ni kweli kabisa niliona pointer inazunguka yenyewe juu ya ubao pasipo kuguswa na mtu.
Niliogopa sana na nilifanikiwa kutoka nje haraka. Siku ile sijarudi nyumbani kabisa na nikaenda kulala kwa rafiki. Nilipo rejea asubuhi nikachukua ubao ule na nikautupa, ila badae niliurejea na kuuchoma moto kabisa.
Nadhani nilikosea sheria au taratibu za mchezo, pia niligundua sio jambo sahihi kutafuta mawasiliano au ukaribu na roho za giza. Kuanzia siku hiyo mpaka leo, nikilala kwenye chumba changu naota lakini sikumbuki ndoto yoyote, tofauti na sehemu nyingine. Nahisi bado kuna tatzo ndani ya chumba changu, itabidi nihame nijaribu sehemu nyingine.
Hili tukio ni la kweli na nilikutana nalo wala sio hadithi au story ya kutunga, kama yupo atakaye hitaji kujaribu, nipo tayari kumpa maelekezo lakini atambue kwamba ni mchezo hatari sana na sio vyema kuufanya ukiwa pekeyako.
Shukran kwa kusoma andiko hili, karibu share maoni au experience yako kuhusu OUJIA board.
View attachment 3045421
______________________
#BM
Kuogopa ni hali ya kawaida, Lengo lilitimia kwa kuona na kupata uhakika kama inawezekana au La...Unazitafuta nguvu za giza halafu unaogopa mwenyewe, ulizitafuuta za nini?
Hawa sio wa kuleta pesa, ukitaka pesa zipo njia nyingine za kufanya pamoja na kutoa kafara za damu ili wakija uwape.Badala ungemtuma huyo kibwengu akazoe pesa akuletee wewe unacheza naye tu.
Wanaotaka kafara ya damu ni wachafu.Hawa sio wa kuleta pesa, ukitaka pesa zipo njia nyingine za kufanya pamoja na kutoa kafara za damu ili wakija uwape.
Hakika nimelipataMwana kulitafuta
Wapo wachafu na hawataki damuWanaotaka kafara ya damu ni wachafu.
Wasafi huwa hawataki kitu.
Kwa hawa wanakuja kupiga misele tuHawa sio wa kuleta pesa, ukitaka pesa zipo njia nyingine za kufanya pamoja na kutoa kafara za damu ili wakija uwape.