Niliyoyaona baada ya kumiliki gari ya Mzungu

Hizo gari za mzungu ili ufaidi lazime uwe na uelewa mzuri wa magari.
Mwaka Jana Kuna Mzee tulikuwa naye Songea tunaingia vijijni yeye alikuwa anatumia BMW X3 hata alipokuwa akiambiwa gari hii hairudi Dar hajali.

Na yeye ni fundi pia anasema kwenye BMW Series X,hiyo X3 kwenye njia mbovu anaipeleka atakavyo na kweli alikuwa anatangulia mbele Sisi na GX100 Cresta.
Gari yake exhaust iliachia kwenye tuta na akitoa Kisha akaenda kurekebisha baada ya siku 2.

BMW X3 ina muungurumo mmoja wa kibabe Sana, kwenye milima mikali ukiwa nyuma yake na exhaust imetolewa.
 
Mjomba subiria hata Masika moja ipite kwanza. Gari haina hata mwaka unasema hujaona issues zaidi ya brake pads zilizoisha? 😂

Kiboko ya mjerumani ni mvua na madimbwi tu, utakuja kusimulia humu.
Hii inategemea, kama gari ni jipya au limetumika (umri). Mimi nina Mitsubishi Outlander (2016), tangu niinunue miaka mitano iliyopita sijaenda kwa fundi (haijahitaji matengenezo) isipokuwa regular service kila baada ya miezi sita. Of course mimi ni mzee, kwa mwaka ninaenda si zaidi ya kilomita elfu kumi. Ninyi vijana mna safari nyingi. Gari ni matunzo. Kama unaiendesha kama vile uko kwenye mashindano, wear and tear yake ipo juu na uwezekano wa kuharibika ni mkubwa kuliko yule anaye libembeleza gari lake kama mtoto
 
Sawa. Mzee mie nina damu inayochemka ligi za mchangani lazima zile.
 
Wengi wanazishindwa gari za mzungu.

Wananunua kwa sifa badae zinawashinda.

Mpaka sasa sidhani kama hizo VW tena za zamani zikose mafundi au spare. Labda ziwe za miaka ya sasa.
 
Mm naipenda sana Volkswagen beetle new model
 
Gari lilikuzidi uwezo kijana.

Gari kama Touran unawezaje inunua ushindwe kuihudumia?
Vanguard ungeiweza sasa?
hela ilikuwepo chief kwani niliagiza parts kibao toka SA ikiwemo gearbox,maana baadae ilikua inaruka gears halafu nasikia mlio kama mtu kapiga nyundo kwa engine.Ilinipuna karibia 6m plus 1.5m ya engine\gerbox ya carina +ufundi nk. Gari ya mjerumani ntanunua mpya sio used maana ni ugonjwa wa moyo.
 
very useful
 
Gari imekula hela mwisho ukaweka engine ya Toyota kuna mahali umekosea mkuu. Usingefika huko. Kitabu usipokielewa hukuandikiwa wewe. Hizo hizo used tunatumia karibu miaka 20 sasa. Mpya hata mimi naitamani.
 
Shikamoo babu..

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana ni gari lako specific ndo ilikuwa na shida na sio all european brands.
 

Mkuu bado familia inakuhitaji!! Gari hazihitaji mbio za sifa ,speed 250 ukipata ajali unachomoka kwenye kioo na kiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…