Niliyoyaona jana kwenye ATM ya NMB Gongolamboto yanatia aibu kwa watumishi

Huu uzi inabidi kuwa makini sana kwenye kuuchangia. Nina hoja 5;
1. Mimi kwa uzoefu wangu ni kwamba mishahara ya watumishi hasa wa serikali haitoshi. Nilishawahi kuwa mwalimu mwaka 2006 - 7. Tulianza na 118k na hadi naondoka ilikuwa 137k. Huu mshahara ulisababisha nile kiapo cha kuja kuwa mfanyabiashara. Nilikuwa peke yangu ila ilikuwa haitoshi.

2. Waalimu na watumishi wengi huwa wazito sana kujishughulisha na shughuli ndogo ndogo. Wakati niko mwalimu nilikua nafundisha tuition jumamosi na kujikusanyia tsh 200 kwa kila mtoto. Zile hela za jumamosi zilikuwa zikinisaidia sana. Wale waalimu wakongwe walikuwa wanaona kama vile kujishusha sana hivyo walikuwa hawajihangaishi na hizo 200 za weekend. Walikuwa wakisubiri likizo ndefu ndo wafundishe tuition.

3. Familia zetu ni chanzo kingine cha kudidimiza watumishi kwenye umaskini. Hapa Afrika ikishajulikana umepata ajira basi jua automatically kuna beneficiaries wa huo mshahara unaowajua na usiowajua. Yaani hata kama mshahara uwe tsh 100k utasumbuliwa tofauti na ukiwa mjasiriamali. Binafsi baada ya kuwa mjasiriamali nikawa sipokei simu za mizinga kwasababu ilionekana kama nishapotea kwa kuacha ajira.

4. Watumishi wengi ni kama vile wakishapata ajira ndo mwisho wa vitu vingine vyote na kujali mwonekano wake mbele ya jamii. Yaani atafanya kitu aende sawa na jamii inavyotaka. Kwa mfano jamii wakati inakupiga mzinga wa hela kwenye mshahara wako hapohapo itakusisitiza ununue kiwanja (plot), ukope gari, uoe/uolewe, upange nyumba kubwa na mambi mengine ambayo utakuta haziko kwenye plans. Nimeona watumishi wengi wakiishi maisha magumu sana kisa walianza kujenga kwa kujinyima sana plus mikopo.

5. Ujinga wa baadhi ya watumishi wenyewe unachangia. Ripoti za TAKUKURU zinaonyesha watumishi hasa waalimu ni wahanga wa utapeli. Najiuliza hawa waalimu si tumesoma nao chuo inakuwaje wanatapeliwa mara kwa mara utadhani sio wasomi? Watumishi muwe mnaji-update jinsi dunia inavyoenda.
 
Tuishi kulingana na vipato vyetu tusiendekeze tamaa maana PEPO LA TAMAA litakupeleka kwa PEPO LA MIKOPO na MADENI.
Kikubwa yatupasa kusali na kukemea katika jina la Yesu.
Ameen
 
Wengi ni walimu, wana akili sare, mi ni mwl pia huwa naenda baada ya wk!
 
Mchawi ni wahuni wa ccm! Stupid! Majizi mengi!
 
Hivi najiuliza kitu, ni kweli wengi huwa wanakopa na kuwekeza kadi za benki, sasa ikatokea nineunganisha simbanking na nikakopa nikaweka kadi mwisho wa siku mkopeshaji anabaki na kadi isiyo na msaada.

Wanafanyaje kuepuka kupigwa hawa wakopeshaji?
Mtz ana hata akili ya simbanking? Wachache!
 
We kwenu kama mashaallah mshukuru Mungu sisi wengine kwenye koo zetu ndo pekee tunaolipwa kupitia benki
 
Biashara zenye faida kubwa zinahitaji mtu kuwa na roho ngumu, vilevile na mbaya, na pia mtu kujilipua. Hakuna sehemu yoyote ile maskini anaye mtetezi wa kweli.

Sana sana atapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa ili kwa kitambo kifupi asahau matatizo yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana waalimu wanapopewa kuwa wasimamizi wa uchaguzi huwa wanatusaliti kwa ajili ya dhiki
 
Hivi najiuliza kitu, ni kweli wengi huwa wanakopa na kuwekeza kadi za benki, sasa ikatokea nineunganisha simbanking na nikakopa nikaweka kadi mwisho wa siku mkopeshaji anabaki na kadi isiyo na msaada.

Wanafanyaje kuepuka kupigwa hawa wakopeshaji?
Maisha yatakuwa magumu utaenda kopa wapi tena Ili mwezi ukutane
 
Mimi hata boom likitoka chuo nilikuw nasbr siku kadhaa kwa sababu akiba ilikuwepo.
Ile kujazana ni jau kubwa.
Ile mbaya sana hapa mabibo mabibo watu walikuwa tumepanga sasa vile mishemishe za hata vibaka wanajua madogo wamepata pesa ...Aisee zile phase za boom kila phase utasikia mwanachuo fulani kakabwa kaibiwa pesa unakuta mtu laki tano katoa yote na Wana sijui Kuna watu walikuwa wanauza ramani yaani watu walishavamiwa mpaka getto kutemeshwa pesa zote..Kuna mwana alikuja katwa kidole cha mguu mpaka akaonyesha pesa alikuwa anakaa mabibo karibu na manzese.

Watu walikuwa kama west life siku ya boom wanatembea makundi makundi huko ubongo wanajazana kweny mabar ukija manzese na sinza ndo usiseme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…