MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Huu uzi inabidi kuwa makini sana kwenye kuuchangia. Nina hoja 5;
1. Mimi kwa uzoefu wangu ni kwamba mishahara ya watumishi hasa wa serikali haitoshi. Nilishawahi kuwa mwalimu mwaka 2006 - 7. Tulianza na 118k na hadi naondoka ilikuwa 137k. Huu mshahara ulisababisha nile kiapo cha kuja kuwa mfanyabiashara. Nilikuwa peke yangu ila ilikuwa haitoshi.
2. Waalimu na watumishi wengi huwa wazito sana kujishughulisha na shughuli ndogo ndogo. Wakati niko mwalimu nilikua nafundisha tuition jumamosi na kujikusanyia tsh 200 kwa kila mtoto. Zile hela za jumamosi zilikuwa zikinisaidia sana. Wale waalimu wakongwe walikuwa wanaona kama vile kujishusha sana hivyo walikuwa hawajihangaishi na hizo 200 za weekend. Walikuwa wakisubiri likizo ndefu ndo wafundishe tuition.
3. Familia zetu ni chanzo kingine cha kudidimiza watumishi kwenye umaskini. Hapa Afrika ikishajulikana umepata ajira basi jua automatically kuna beneficiaries wa huo mshahara unaowajua na usiowajua. Yaani hata kama mshahara uwe tsh 100k utasumbuliwa tofauti na ukiwa mjasiriamali. Binafsi baada ya kuwa mjasiriamali nikawa sipokei simu za mizinga kwasababu ilionekana kama nishapotea kwa kuacha ajira.
4. Watumishi wengi ni kama vile wakishapata ajira ndo mwisho wa vitu vingine vyote na kujali mwonekano wake mbele ya jamii. Yaani atafanya kitu aende sawa na jamii inavyotaka. Kwa mfano jamii wakati inakupiga mzinga wa hela kwenye mshahara wako hapohapo itakusisitiza ununue kiwanja (plot), ukope gari, uoe/uolewe, upange nyumba kubwa na mambi mengine ambayo utakuta haziko kwenye plans. Nimeona watumishi wengi wakiishi maisha magumu sana kisa walianza kujenga kwa kujinyima sana plus mikopo.
5. Ujinga wa baadhi ya watumishi wenyewe unachangia. Ripoti za TAKUKURU zinaonyesha watumishi hasa waalimu ni wahanga wa utapeli. Najiuliza hawa waalimu si tumesoma nao chuo inakuwaje wanatapeliwa mara kwa mara utadhani sio wasomi? Watumishi muwe mnaji-update jinsi dunia inavyoenda.