Niliyoyaona jana kwenye ATM ya NMB Gongolamboto yanatia aibu kwa watumishi

Baada ya Samia kuwadanganya kuwa kaongeza 23% ya mashahara kumbe ni 2,3% nikimuona mtumishi kabeba bango kwenye mei mosi nitamuita ******!
 
wenye mawazo kama haya kina Nzie ya Mana, na Bugucha
ukweli ni kwamba serikari wala ccm haikupangii namna ya kuishi, usiendeshwe na utumishi wako serikalini kiasi cha kushindwa kujijenga, wewe ni mtanzania huru, feel free wherever.

naungana na Mwl.RCT Kusema kwamba; mtumishi binafsi ndie mwenye jukumu la kujitoa kwenye ufukara, wala sio serikali/ccm
 
Tungejua background ya baadhi ya hao watu na jinsi wanavyokomaa na extended families. Muda mwingine ni kufumba mdomo tu.

Mwingine akipata mshahara 80% unaishia kwenye starehe ni tofautina hawa wenzetu.

Wengi wao mnaowaona kwenye foleni hawajui starehe 90% ya mshahara unaushia kusolve matatizo ya familia. Na wengi wao ndio wale wametoka familia zetu hizi za kimasikini upande ya nyumbani wanamuangalia yeye na upande wa mke wanamuangalia yeye na ukiangalia mshahara wenyewe hauwezi kukidhi mahitaji yote basi ni madeni na shida za kutosha.

Na pia sio kwamba wanapenda ile hali there is no way out. Haiwezekani eti wale wote wamekosa akili but ukikaa nao wakakupa maswaibu yao unabaki tu kuwaombea Mungu awape wepesi coz wanapambana mno kuendesha familia zao ni tofauti kabisa wengine waliozaliwa na "Silver Spoon"

Na wahanga wakubwa kwenye hii kadhia ni walimu sababu ndio kada yenye watumimishi wengi. Mtu akiangalia foleni atasema tu wale ni walimu but humo humo kuna manesi, watendaji, watu sijui wa kilimo n.k

Way forward nafikiri njia pekee ni SERIKALI kuendelea kuongeza mishara kila mwaka km alivyokuwa anafanya mzee wa msoga, nafikiri itapunguza hii changamoto ya ukali wa maisha kwa baadhi ya watumimishi wake.
 
Uko sahihi sana ndg,huyu aliyeleta huu Uzi kwanza sio mtumishi wa serikali na kama mtumishi utakuta anafanyia kaz TRA ambako wao national housing ambako mtu wa certificate analipwa mshahara wa mwl wa degree hapo mtakuwa sawa? Aache umama huyo
 
Kwa card ukitumia app yao 100k unakatwa buku hivi.
Usitoe na likadi au 150.
Tumia app crdb makato ni sawa na bure
Ukishaipokea ukaenda kwa wakala kuitoa kwa simu unakatwa ngapi?
 
Hawa watu wametoka familia bora akina lizione huyo atapata tabu wapi? Kuna watu wanaropoka katika kutoa kauli zao juu ya watumishi,watumishi wrngi n tegemez huwez kujaji kitu kama hujafanya tafiti! Mwl wa degree aliyefanyq kaz zaid ya miaka 10 mshahara wake sawa na mtumishi wa certificate anaefanyia kaz TRA,TANESCO,NHC Sasa hapo mtakuwa sawa? Wache kuwasema vibaya Hawa watumishi jamani
 
Sasa kama Watu wenye nafasi ya hata kupata kuaminika na kukopesheka mnalalama, ni kwamba hamjui ya kuwa wapo mamilioni ya Wenzenu hawana hiyo nafasi, yaani wanaitwa "hawakopesheki?"...Sasa wao wamlalamikie nani?.
 
Yataisha.
I hope
Atafika Rais atakayekomesha umaskini na ufukara wa watumishi
Hilo sio swala la Rais kukomesha umaskini na ufukara. Yeye kashamaliza jukumu lake la kukulipa SALARY. Sasa kazi ipo kwako kujikwamua na umasikini na decession ya unakuwa tajiri au maskini inaanza pale tu message ya mwamala inaposoma. Elimu kuhusu pesa(Financial Literacy) ni ndogo sana kwa watu wetu, ndio maana unayaona yote hayo.
 
Kutoa wa wakala
KIASI GHARAMA
100,000 4,800

Kutoa kwa ATM
100,000 1,200

Kupanga ni kuchagua.
Kwa hili uliloandika kama ni sawa nadhani ni muhimu kuweka utoaji ukalingana ili kuvutia watu kutumia njia nyingine. Ila katika hili sote tunajuwa ATM haziko kila sehemu lakini mawakala kila mtaa uhitaji hata gari kufika kwa wakala sasa kama tofauti 1200 ili kuifuata ATM si utahitaji usafiri kwa maana kuna gharama hapo nakwenda kwa wakala jirani zero cost. Kama ulivyosema kupanga ni kuchagua lakini kwa mimi najuwa kuzifuata ATM ni gharama pia siku zote naenda kwa mawakala.
 
Muda kitu gani bana sisi wananzengo hatunaga Hayo mambo ya muda. Kama ufugaji kuku ni dili mbona huachi hicho kibarua cha ulinzi kulipwa 80k kwa mwezi uwekeze huo muda kwenye kuku? Sema tu ulichelewa foleni hapo.
 
Kwamba ukitoa kwa SIM BANKING makato yanalingana????

Kwamba unapaswa kusucrifuce laki 3 uanze kufuga kuku ili usiende Bank kupanga foleni???

Mbona wewe ndio unaonekana huna akili
 
Kwamba ukitoa kwa SIM BANKING makato yanalingana????

Kwamba unapaswa kusucrifuce laki 3 uanze kufuga kuku ili usiende Bank kupanga foleni???

Mbona wewe ndio unaonekana huna akili
Ukiwa na mradi wowote, hutaweza kupoteza muda kukaa foleni ili ukatoe laki kadhaa kwenye ATM.
Utaenda muda unaotaka wewe na si ikiingia tu umo.
Acha wendawazimu fanya biashara ili usiutie aibu utumishi wa umma
 
Ukiwa na mradi wowote, hutaweza kupoteza muda kukaa foleni ili ukatoe laki kadhaa kwenye ATM.
Utaenda muda unaotaka wewe na si ikiingia tu umo.
Acha wendawazimu fanya biashara ili usiutie aibu utumishi wa umma
Tafuta kazi ya kufanya ili uhangaisheena maisha ya watu wengine kwa kujipa umuhimu sana wa ratiba za watu.
 
Hapo tatizo sio ku-sucrifice shs 300000/= na kuingiza kwenye ufugaji, tatizo hapa ni riba na jinsi ya kutumia hela ya mkopo.

Riba zinazotozwa ni kubwa sana (wasiojua watasema ndogo), fedha ya aina hii inatakiwa iingizwe katika biashara iliyokomaa.

Kwakuwa mtu unakuwa na uhakika wa faida itakayoingizwa, basi makali ya marejesho yakuwa madogo na hivyo kutokuathiri hali yako kiuchumi.

Tatizo tunakopa halafu hela yote tunakwenda kujengea nyumba ya kuishi wenyewe, haiingizi hata mia, na makato (pamoja na riba), kodi, na michango, vinakula zaidi ya robo tatu ya mshahara, hapa unategemea nini?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi najiuliza kitu, ni kweli wengi huwa wanakopa na kuwekeza kadi za benki, sasa ikatokea nineunganisha simbanking na nikakopa nikaweka kadi mwisho wa siku mkopeshaji anabaki na kadi isiyo na msaada.

Wanafanyaje kuepuka kupigwa hawa wakopeshaji?
Wafanyakazi wengi hawana ujanja huo
 
Et Westlife πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…