MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
1. Kuwaanzisha Erasto Nyoni na Bernard Morrison ambao leo ndiyo Wachezaji wa Simba SC waliocheza vibaya na Kuharibu zaidi badala ya Kuwaanzisha Muzamiru Yasini na Rally Bwalya Kiufundi kumeigharimu Simba SC.
2. Kumuanzisha Clatous Chama ambaye bado Kichwa chake kimetawaliwa na Kumpoteza Mke huku ikijulikana Kiufundi kabisa Saikolojia ina nafasi yake katika Ufanisi wa Mchezaji Mpirani.
3. Kutangulia Kumuingiza Meddie Kagere ambaye kwa sasa hana tena Madhara yote na ameshuka mno Kiuchezaji na Kuchelewa Kumuingiza Mshambuliaji makini Chris Mugalu Kiufundi Kumeigharimu Simba SC.
4. Ama Kocha Mkuu na Msaidizi wake au Wachezaji wa Simba SC kwa sasa wamezidi Kujiamini na kuwa na Dharau wakisahau kuwa Mechi ya Derby'na Yanga SC ni zaidi ya Kucheza na akina AS Vita Club, Al Ahly na Kaizer Chiefs FC.
5. Simba SC kutokuheshimu Utamaduni wa Derby ambapo Kambi ya Simba SC kule Bunju ilikuwa ni ya wazi na kila Mtu hata Adui aliruhusiwa kwenda na Kuhudhuria tofauti na iliyokuwa Kambi ya Yanga SC ambayo ilitawaliwa na Umakini, Tahadhari na Ulinzi mkubwa sana.
6. Ndani ya Klabu ya Simba kuna Usaliti mkubwa sana na kuna Watu wanaodhaniwa ni Simba SC kweli kumbe ni Mapandikizi ya Yanga SC na ndiyo kwa miaka hii Minne wamechangia Yanga SC kuwa na Kiburi dhidi ya Simba SC japo Kiuwezo hata Wenyewe wanakiri Kuzidiwa na Simba SC.
7. Wachezaji wa Simba SC kutokuwa na Moyo wa Uchungu na wa Kujitolea Kuifia Timu / Klabu kama alionao Jose Miquissone ambaye huhitaji Akili Kubwa kujua kuwa ndiyo mwenye Uchungu hasa na Mafanikio ya Simba SC kuliko wengine ambao Uchungu walionao ni Kutongoza hovyo Wahudumu wa katika Ndege, Kutoroka Kambini kwenda Klabu na kufanya Uzinzi, Kujipodoa na Kutwa kuwa tu Mitandaoni kituringishia Gari zao, Nguo zao na Wake / Mademu zao.
Nitakuwa siyo Mwanamichezo, Mpuuzi na Mnafiki pia kama baada ya kusema yote haya nisiipongeze Klabu ya Yanga SC kwa Kushinda Mchezo wa leo kwa Goli la Kimchezo ambalo kamwe ukiwa Mtu wa Mpira huwezi Kumlaumu Kipa Aishi Manula na Beki Shomary Kapombe.
Kwa wale wanaomlaumu Mwamuzi Mwandembwa kuwa ameiumiza mno Simba SC je, tumeshajiuliza kuwa Timu inayoumizwa na Mwamuzi Wachezaji wake kwa Statistics wanaweza kuwa ndiyo wanaongoza kwa Kucheza Faulo / Rafu nyingi zile?
Ushauri wangu wa bure tu kwa Wana Simba SC ni kwamba badala ya Kumlaumu Mwamuzi tumeshukuru kwa Kuwavumilia sana Wachezaji wa Simba SC kwani nina uhakika angeamua Kuchezewa Kiukauzu na inavyotakiwa basi John Boko, Thadeo Lwanga, Joash Onyango, Bernard Morrison, Mohammed Hussein Tshabalala na Pascal Serge Wawa wangetolewa kwa Kadi Nyekundu.
Simba SC ikubali Matokeo ijipange mno.