Herbert Nkuluzi
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 2,592
- 2,629
Baada ya sub za Simba Yanga walikuwa bora zaidi ya Simba?Wewe hapa umechambua au umelalamika?
Kinachokufanya usikubali ubora wa mpinzani wako ni nini wakati kila mtu anayechambua hapa kaiona Yanga ilivyocheza kipandi cha kwanza na Simba kupotea kwa takribani DK 30 za kwanza? Ukiamua kuchambua chambua ukija kishabiki sema wewe ni shabiki.
Kitendo cha mechi kuisha bila Mzamiru huku kocha akichezesha 3 strikers ni kubet kusiko na mpangilio. Ukiangalia Sub alizofanya Nabil utakubaliana na mleta Uzi, ni kocha kichaa tu angekubali Kaseke acheze DK 70 uwanjani, Feitoto amecheza kwa nguvu muda mrefu na alikokuwa anaelekea ni kwenye kadi nyekundu ukikumbuka foul dhidi ya Engineer. Tuisila kuanzia DK ya 70 alikuwa likizo ya bila malipo kwa hiyo kupumzishwa ilikuwa haina mjadala.
Rudi kwenye Sub za Simba sasa.
Mbona game kadhaa tunacheza hivyo hasa tunapokuwa tunahitaji goli zaidi? Kimahesabu Yanga hawakuwa bora kwenda mbele ndiyo maana Kocha aliweka watu wengi wa kushambulia mbele cos nyuma kulikuwa na watu wengi upande wa Yanga ,he was right na ililipa japo goli halikupatikana kama Yanga wangepata goli la pili kwa mapungufu ya uwanjani basi ungesema sub imetuua ila haikutokea hivyo.Kama sub ya Simba ilikuwa mbovu mbona Yanga hawakuwawin Simba tena kupitia udhaifu huo? Tazama Chiefs walivyotumia udhaifu wa sisi kushambulia na kuwa walegevu kurudi kukaba tulikula 4 hiyo ndiyo huitwa matumizi ya udhaifu wa mpinzani.Mpinzani hawezi kuwa dhaifu afu clear chances hujapata.
Sema Yanga akikuwa bora kwenye nini hadi akapata matokeo yale na Simba sijaona udhaifu mkubwa cos kama ni loose balls timu yoyote ile inaweza kufungwa from far kwa situation ya jana ya goli wala hiyo haiwezi kuprove ubora wa timu.
Ubora wa timu unazingatia utengenezaji wa nafasi na kuzitumia , wewe sema Yanga walitengeneza nafasi ngapi na walitumia ngapi maana hata ya Zawadi ni loose ball sio created chance cos hakuwa assisted na mchezaji wa Yanga.Wachezaji wa Simba walijipanga kwa usahihi nyuma ila mpira ulimgonga mchezaji ukaenda upande ambao golikipa hakuwa na cha kufanya.
Tatizo la bongo kila timu inayoshinda ndiyo bora na hapo ndipo mwanzo wa matatizo.