Niliyoyaona kwa Mkapa (Lupaso) Stadium leo ambayo kama yasipofanyiwa Kazi basi yanaenda Kujirudia tena Lake Tanganyika 25 July, 2021 ni haya

Niliyoyaona kwa Mkapa (Lupaso) Stadium leo ambayo kama yasipofanyiwa Kazi basi yanaenda Kujirudia tena Lake Tanganyika 25 July, 2021 ni haya

Kila siku mnalalamika kuwa:
1. Mgalu si mchezaji wa maana;
2. Kagere hapa zei na kocha ingawa bado ni mchezaji jembe.
Leo hii imebadilika! Maajabu haya ya wanasimba
Ndy maana Rage aliwaita MAMBUMBUMBU hakukosea kiongozi wangu
 
Kwa kweli Tuisila alinikera sana jinsi alivyocheza Kipindi cha pili. Sikuelewa kwanini kocha alimuacha hadi dk ya 90. Alikuwa anatembea tu uwanjani,akipewa mpira anapoteza kirahisi. Na akipoteza hakabi!!

Kocha lazima awe mkali na amuonye.Shukrani kwa dogo Kibwana shomari alijitahidi mno kupambana na Morrison ambaye alikuwa akipewa mipira mingi iliyopotelea kwa Tuisila.
Hakumaliza kipindi cha pili
 
Watu wamesahau mpaka ubingwa!!! Mimi ni Simba japo sina ule ushabiki sana mpaka nikose usingizi na kwa bahati mbaya mechi sikuiona nilikuwa na majukumu mengine ila tatizo kubwa nadhani Simba waliaminishwa na viongozi wao kuwa wao ni bora na kama walizifunga Finalist wa kombe la CAF yanga ni nani hawana kitu na terehe ile walikimbia na hii walitafuta sababu ya kukimbia hii ikawakaa akilini wachezaji kuwa Yanga wanaogopa lakini mwisho wa siku wameshinda na kama harusi basi wametia mchanga chakula cha harusi kwa hili Simba wamekosa furaha ila wana nafasi ya kuweka sawa Kigoma wakikosea na huko basi huu ndio utakuwa ubingwa wa kwanza duniani lakini mshindi ana majonzi kuliko number 2. Focus mechi ya Kigoma na Manara afunge mdomo wake mchafu anawapa sifa sio zao mpaka kina Morison wanajiona kama wamekuwa kina De bruyne.
Ki Morrison Jana sijui kwanini refa hakukigonga yellow card maana muda wote anamfokea refa
 
Hata mechi ijayo tuna uwezo wa kuwafunga. Mechi ya mwisho ya sare, mlisawazasha dk ya 89 ya mchezo! Na kwa taarifa yako, Yanga siyo timu dhaifu hata kidogo.

Wachezaji wa Yanga wana ubora kuliko hata hao wa Simba! Kinacho ikumba Yanga ni ukosefu tu wa morali kwa baadhi ya wachezaji, na hasa wale wenye kudai malimbikizo ya mishahara, nk!

Siku zote mashabiki wa simba akili zenu zimeshikiliwa na yule mvuta bangi wenu Haji Manara, anayependa kucheza mpira nje ya uwanja! Huku Yanga ikiwekeza nguvu kubwa ndani ya uwanja! Na mkiendelea kumuendekeza, tutawafunga kila siku.
Hadija manara tangu aanze kukalia tako moja akili zimemhama kabisa
 
Kwa kweli Tuisila alinikera sana jinsi alivyocheza Kipindi cha pili. Sikuelewa kwanini kocha alimuacha hadi dk ya 90. Alikuwa anatembea tu uwanjani,akipewa mpira anapoteza kirahisi. Na akipoteza hakabi!!

Kocha lazima awe mkali na amuonye.Shukrani kwa dogo Kibwana shomari alijitahidi mno kupambana na Morrison ambaye alikuwa akipewa mipira mingi iliyopotelea kwa Tuisila.
Katika Mambo ninayomchukia Tuisila na Ntibazonkiza ni kwamba wao ni vinara wa kupoteza mipira na bad enough hawakabi kabisa, Tuisila hana msaada kabisa kwenye timu iwapo inashambuliwa mfululizo harafu sio Target man afikapo kwenye final third ya mpinzani the same to Saido yeye ndy kinara wa kupiga pass fyongo kwenye klabu ya Yanga sema mashabiki wengi wa mpira hawafuatilii mpira unavyochezwa wao furaha yao ni kuona goli za faulo anazofunga ndy maana wanamuimba Sana jamaa lkn kiukweli Ana mapungufu makubwa mnooo
 
Watu wamesahau mpaka ubingwa!!! Mimi ni Simba japo sina ule ushabiki sana mpaka nikose usingizi na kwa bahati mbaya mechi sikuiona nilikuwa na majukumu mengine ila tatizo kubwa nadhani Simba waliaminishwa na viongozi wao kuwa wao ni bora na kama walizifunga Finalist wa kombe la CAF yanga ni nani hawana kitu na terehe ile walikimbia na hii walitafuta sababu ya kukimbia hii ikawakaa akilini wachezaji kuwa Yanga wanaogopa lakini mwisho wa siku wameshinda na kama harusi basi wametia mchanga chakula cha harusi kwa hili Simba wamekosa furaha ila wana nafasi ya kuweka sawa Kigoma wakikosea na huko basi huu ndio utakuwa ubingwa wa kwanza duniani lakini mshindi ana majonzi kuliko number 2. Focus mechi ya Kigoma na Manara afunge mdomo wake mchafu anawapa sifa sio zao mpaka kina Morison wanajiona kama wamekuwa kina De bruyne.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hata mechi ijayo tuna uwezo wa kuwafunga. Mechi ya mwisho ya sare, mlisawazasha dk ya 89 ya mchezo! Na kwa taarifa yako, Yanga siyo timu dhaifu hata kidogo.

Wachezaji wa Yanga wana ubora kuliko hata hao wa Simba! Kinacho ikumba Yanga ni ukosefu tu wa morali kwa baadhi ya wachezaji, na hasa wale wenye kudai malimbikizo ya mishahara, nk!

Siku zote mashabiki wa simba akili zenu zimeshikiliwa na yule mvuta bangi wenu Haji Manara, anayependa kucheza mpira nje ya uwanja! Huku Yanga ikiwekeza nguvu kubwa ndani ya uwanja! Na mkiendelea kumuendekeza, tutawafunga kila siku.
Usitutishie hapa na wee, hakna lolote hilo goal lenyewe la ndondokela ndo unajitapa hivyo, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Tukutane kigoma.
 
Darby ya Simba na Yanga kama wewe ni mjuzi wa mpira hupaswi kushangazwaa na haya matokeo ya jana.

Kama mnakumbuka Darby ya Mwaka juzi yanga wakiwa hali dhoofu kaabisa, kipindi cha kwanza simba walitengeneza nafasi wakapata goal 2, kipindi cha pili Yanga wakabadilika wakatengeneza nafasi wakazitumia wakarudisha goal zote 2

Kilichotokea jana Yanga walipata nafasi nyingi kipindi cha kwanza wakaweka kambani simba wakapata nafasi nyingi kipindi cha pili wakashindwa kutumia nafasi.
 
Game nimeicheck vizuri kabisa ndiyo maana nimesema wazi shida ilikuwa kutumia nafasi tu upande wa Simba

Mfano Boko alikosa goli ambalo kwa mchezaji ambaye ni makini hakupaswa kukosa , Morisson alikosa goli hivyo hivyo , kwa kifupi game ilikuwa mikononi mwa Simba hasa second half ila nafasi hazikutumiwa vizuri na wachezaji wetu.Ukitazama vizuri utagundua kuwa tumeingia kwenye box ya Yanga mara nyingi zaidi , naamini huwezi kufanikiwa kuingia kwenye box ya mpinzani zaidi afu tuseme hamkucheza vizuri katikati ya uwanja au mpira kwa ujumla unless kucheza mpira vizuri kuwa kuna maana nyingine.

Goli la Yanga la deflection ni maamuzi ya mtu kupiga shuti kuelekea golini na likamgonga mtu likajaa wavuni at the end unakuwa umeshinda ila hata Kocha makini hawezi kujivunia hilo ,kocha makini atajiuliza kama ule mpira usingedeflect kwa beki wao Je,timu yangu ilikuwa na uwezo wa kutengeneza nafasi za wazi na kuzitumia? Kama hakuna nafasi zinazotengenezwa na timu kocha mzuri anajua hii sio class ni bahati tu.

Ninachokikubali kwa sehemu pia ni hili la kujitoa kufa kupona kwa Yanga (hii ni nature ya timu inayohisi ni dhaifu ila inajaribu kuonesha ina ubora mkubwa ) wachezaji katika game hizi wanacheza kwa umakini hata kama viwango vyao kesho hutoviona hivyo jambo linaloitofautisha na Simba na haya hujidhihirisha kwa namna ambavyo timu inaperform kwenye mashindano marefu hasa ya Ligi za mzunguko.

Jaribu kufikiri upya , ikiwa refa angetoa penalty ile Simba wakafunga then wakashinda tungekuja hapa kusema wachezaji wa Simba hawajitumi kama wa Yanga? Vipi kama nafasi za wazi za Morison na Boko zingekuwa magoli tungekuja na stori hiyohiyo? Kwangu ni hapana

So kama Yanga watashinda games tatu zijazo mwaka huu mbele ya Simba tutakuwa na cha kuhoji zaidi kwa nini ,ila kwa jana mi naona bahati tu maana mimi sijui ishu za uchawi naamini tu uchawi upo ila ulikuwa applied au la jana mie sijui.
"Mfano Boko alikosa goli ambalo kwa mchezaji ambaye ni makini hakupaswa kukosa"

[emoji115]Mchezaji gani makini hajawai kukosa goli?
 
1. Kuwaanzisha Erasto Nyoni na Bernard Morrison ambao leo ndiyo Wachezaji wa Simba SC waliocheza vibaya na Kuharibu zaidi badala ya Kuwaanzisha Muzamiru Yasini na Rally Bwalya Kiufundi kumeigharimu Simba SC.

2. Kumuanzisha Clatous Chama ambaye bado Kichwa chake kimetawaliwa na Kumpoteza Mke huku ikijulikana Kiufundi kabisa Saikolojia ina nafasi yake katika Ufanisi wa Mchezaji Mpirani.

3. Kutangulia Kumuingiza Meddie Kagere ambaye kwa sasa hana tena Madhara yote na ameshuka mno Kiuchezaji na Kuchelewa Kumuingiza Mshambuliaji makini Chris Mugalu Kiufundi Kumeigharimu Simba SC.

4. Ama Kocha Mkuu na Msaidizi wake au Wachezaji wa Simba SC kwa sasa wamezidi Kujiamini na kuwa na Dharau wakisahau kuwa Mechi ya Derby'na Yanga SC ni zaidi ya Kucheza na akina AS Vita Club, Al Ahly na Kaizer Chiefs FC.

5. Simba SC kutokuheshimu Utamaduni wa Derby ambapo Kambi ya Simba SC kule Bunju ilikuwa ni ya wazi na kila Mtu hata Adui aliruhusiwa kwenda na Kuhudhuria tofauti na iliyokuwa Kambi ya Yanga SC ambayo ilitawaliwa na Umakini, Tahadhari na Ulinzi mkubwa sana.

6. Ndani ya Klabu ya Simba kuna Usaliti mkubwa sana na kuna Watu wanaodhaniwa ni Simba SC kweli kumbe ni Mapandikizi ya Yanga SC na ndiyo kwa miaka hii Minne wamechangia Yanga SC kuwa na Kiburi dhidi ya Simba SC japo Kiuwezo hata Wenyewe wanakiri Kuzidiwa na Simba SC.

7. Wachezaji wa Simba SC kutokuwa na Moyo wa Uchungu na wa Kujitolea Kuifia Timu / Klabu kama alionao Jose Miquissone ambaye huhitaji Akili Kubwa kujua kuwa ndiyo mwenye Uchungu hasa na Mafanikio ya Simba SC kuliko wengine ambao Uchungu walionao ni Kutongoza hovyo Wahudumu wa katika Ndege, Kutoroka Kambini kwenda Klabu na kufanya Uzinzi, Kujipodoa na Kutwa kuwa tu Mitandaoni kituringishia Gari zao, Nguo zao na Wake / Mademu zao.

Nitakuwa siyo Mwanamichezo, Mpuuzi na Mnafiki pia kama baada ya kusema yote haya nisiipongeze Klabu ya Yanga SC kwa Kushinda Mchezo wa leo kwa Goli la Kimchezo ambalo kamwe ukiwa Mtu wa Mpira huwezi Kumlaumu Kipa Aishi Manula na Beki Shomary Kapombe.

Kwa wale wanaomlaumu Mwamuzi Mwandembwa kuwa ameiumiza mno Simba SC je, tumeshajiuliza kuwa Timu inayoumizwa na Mwamuzi Wachezaji wake kwa Statistics wanaweza kuwa ndiyo wanaongoza kwa Kucheza Faulo / Rafu nyingi zile?

Ushauri wangu wa bure tu kwa Wana Simba SC ni kwamba badala ya Kumlaumu Mwamuzi tumeshukuru kwa Kuwavumilia sana Wachezaji wa Simba SC kwani nina uhakika angeamua Kuchezewa Kiukauzu na inavyotakiwa basi John Boko, Thadeo Lwanga, Joash Onyango, Bernard Morrison, Mohammed Hussein Tshabalala na Pascal Serge Wawae wangetolewa kwa Kadi Nyekundu.

Simba SC ikubali Matokeo ijipange mno.

Safi uchambuzi makini
 
Katika Mambo ninayomchukia Tuisila na Ntibazonkiza ni kwamba wao ni vinara wa kupoteza mipira na bad enough hawakabi kabisa, Tuisila hana msaada kabisa kwenye timu iwapo inashambuliwa mfululizo harafu sio Target man afikapo kwenye final third ya mpinzani the same to Saido yeye ndy kinara wa kupiga pass fyongo kwenye klabu ya Yanga sema mashabiki wengi wa mpira hawafuatilii mpira unavyochezwa wao furaha yao ni kuona goli za faulo anazofunga ndy maana wanamuimba Sana jamaa lkn kiukweli Ana mapungufu makubwa mnooo
Tulisila jana hakuwa kwenye fomu kama game iliopita simba walikamia kumkaba sana the same na Yakuba, Saido nafikiri tulimsajili kishabiki zaidi lakini hayuko fiti ndiyo maana hana mwendelezo
 
Udhaifu wa Simba kwa sasa ni kukosa a best clinical finisher tu yaani ambaye ikitokea tu chance unahesabu ni goli na awe na uwezo wa mbio(speed) ,anaweza kupunguza watu na akaforce kuscore maana kwa sasa sioni kama tuna mshambuliaji halisi mwenye sifa tajwa hapo juu
Kagere hata control tu ni shida ,Boko vile vile ,Mugalu control anayo ila kufunga yupo chini ,naamini kwa sajili tatu ambazo Manara kasema basi hapo kwenye ushambuliaji watakuwa wamepaona pia.
"sajili tatu ambazo Manara kasema basi hapo kwenye ushambuliaji watakuwa wamepaona pia"

Hapo ni kubahatisha tu ktk usajili
Kumpata bora kuliko hao ni gharama kubwa sana

Ndio maana tunavizia ambao wanamaliza mikataba na mara nyingi uwezo wao unakuwa umeshuka
 
Watu wamesahau mpaka ubingwa!!! Mimi ni Simba japo sina ule ushabiki sana mpaka nikose usingizi na kwa bahati mbaya mechi sikuiona nilikuwa na majukumu mengine ila tatizo kubwa nadhani Simba waliaminishwa na viongozi wao kuwa wao ni bora na kama walizifunga Finalist wa kombe la CAF yanga ni nani hawana kitu na terehe ile walikimbia na hii walitafuta sababu ya kukimbia hii ikawakaa akilini wachezaji kuwa Yanga wanaogopa lakini mwisho wa siku wameshinda na kama harusi basi wametia mchanga chakula cha harusi kwa hili Simba wamekosa furaha ila wana nafasi ya kuweka sawa Kigoma wakikosea na huko basi huu ndio utakuwa ubingwa wa kwanza duniani lakini mshindi ana majonzi kuliko number 2. Focus mechi ya Kigoma na Manara afunge mdomo wake mchafu anawapa sifa sio zao mpaka kina Morison wanajiona kama wamekuwa kina De bruyne.
"Simba waliaminishwa na viongozi wao kuwa wao ni bora na kama walizifunga Finalist wa kombe la CAF yanga ni nani"
[emoji115]

Kwa mtu anayefatilia mpira hili hutokea
Hata uwe bora ila kuna siku inaitwa "siku mbaya kazini"

Hii kuaminishwa sidhani kama ni Hoja ya msingi.
Yaan nikae nimsikilize mtu aniaminishe[emoji23]
 
Ukiachana na Luis, Kinachoiangusha Simba ni wachezaji wengi wa kigeni hawajui thamani ya Derby. Wanacheza tu ilimradi wapo uwanjani mfano ni uchezaji wa Clatous Chama kwenye Derby zote ni wa kiwango cha chini sana.

Natamani hizi mechi za Deby wawe wanacheza wazawa wengi, kama ilivyo kwa Yanga na unaona jinsi wanavyojitoa kwa timu yao.
 
Back
Top Bottom