Niliyoyaona kwenye kampuni za ulinzi

Nakumbuka nililinda hotel Fulani kubwa city center wale wahindi sijui wamiliki sijui ni management ni wapumbavu sana eti kila mteja akiingia au kutoka getini ukimfungulia mlango ni lazima umpigie salute ukizingatia una elimu yako na usomi wako unampigia salute mtu kisa yupo kwenye vits katoka kula hotelini.
Maisha mapito maisha ni kitabu
 
Matron alikuficha kimkakati πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Watu wanaolala ni kitengo cha fire wao wakishapaki magari Yao wanasubiria tu call ya wapi Pana moto wakzime.
Lakini guard ukikutwa umelala unakatwa salary Kama ni mtu wa kulala lala utaambulia buku tu mwisho wa mwezi.
Pana kampuni Fulani waliwawekea king'amuzi magadi wao ili kuwazuia kulala inatakiwa kila baada ya dakika 15 unaponyeza batani uliyovaa inasoma control room kwamba upo macho.
Huna ujanja.
 
Usiku Pana madili mengi sana ya hatari Pana siku tumefacilitate mzigo wa madumu 40 ya mafuta ya kula wafanyakzi wa production walipiga kiwandani saa Tisa usiku wakapakia gari ya kampuni wakatuuza kwamba wanaleta mgao asubuhi kufika asubuhi wanatuletea kiswahili ooho mzigo wote wazee wa doria wametufukizia wameondoka nao.
Hatujui Kama tulipigwa au kweli
 
Hakuna sekta ambayo watu hawakulani hapa Bongo, iwe dini, siasa, elimu, ulinzi, afya na popote pengine.
As long as we are Black Africans we shall not separated with such kind of attributes + behaviors.
Sikupingi kwenye hili na mkulano makazini huambatana na uzembe.Wivu, majungu, uvivu na kuchomeana
 
Anhaaa pole sana .
Walinzi ukitaka ukosane nao waite walinzi wao upenda kuitwa askari , afande na mkuu sasa kupiga salute si kazi yao [emoji3][emoji3]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Nikimaliza kusoma naenda kuomba kazi ya ulinzi
 
"""Supervisor alinielewa nikawa naingia usiku tu asubuhi naulamba kutembeza kaki maofisini jioni naingia Lindon, home narudi weekend.""". Ulikua unalala mda gani mkuu
 
"""Wajinga wale mnalishwa wali maharage saa Saba baada ya kula mnaenda kuulipa uwanjani."""
πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“ Nimecheka sana
Unalipa vipi huo wali marage mkuu
 
""""Enzi hizo palikuwa na wizi wa mawasiliano ya simu.
Anakuja usiku mtaalamu anaingia kwenye control box ya TTCL anawaconnectia wahindi mjini wanapiga international call usiku kucha bill ikija inasoma kwenye kampuni au kiwanda husika""""

Mkuu hapa umeniacha kapa yaani ipo vipi
 
πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
Pole sana mkuu..
Kuna siku na wewe utapigiwa saloot
 
Kazi za ulinzi zinaokoa sana Kama hujapata ramani mjini umegraduate tafuta hizi kampuni kubwa ukipata laki 3 si haba.
Itakusaidia kulipa Kodi,nauli ya kutembeza bahasha mjini,kula nk.
Kozi unakaa kwa mda gani mkuu
 
Kampuni gani hizo nikajiunge kama tech mana nina ujuzi wa IT security
 
Kozi unakaa kwa mda gani mkuu
CV form 4,jkt, lugha.training Kama wiki 2 au mwezi hivi unakula mshahara.
Ingia hizi kubwa achana na hizi za kibongo zinazokopa walinzi mshahara yaani mshahara wa mwezi huu unapewa baada ya siku 40 au mwezi ujao na unapewa nusu ili usiache Kaz.
Hizi zinazolipa shilingi elf 4 kwa masaa 12 kwa siku 30
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…