Niliyoyaona kwenye kampuni za ulinzi

Niliyoyaona kwenye kampuni za ulinzi

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,221
Miaka kadhaa hapo nyuma Katika harakati za kupambana na maisha nimewahi kuajiriwa Katika kampuni kubwa ya ULINZI binafsi hapa nchini Kwa Wakati huo kulikuwa na kampuni kubwa za ulinzi hapa mjini kama nne hivi ambazo zilikuwa zinagombania soko la kulinda maeneo mbalimbali ya jiji ikiwemo mabanki,balozi,ofisi,viwanda na nyumba za matajiri.

Kwa kipindi kile Mimi niliajiriwa upande wa technical ambao mainly tulikuwa tuna-deal na security system ambazo ndani yake kuna masuala ya CCTV kamera,panick button system,intruder system, electrical fence, access control na vinginevyo.

Tuachane na upande wangu wa technical ambao nilikuwa. Leo nataka niongelee upande wa ulinzi (guards) ambao kutokana na experience yangu ndani ya kampuni niliyashuhudia na kuyasikia mengi ya ajabu hususani Mambo yanayohusisha rushwa ya pesa na ngono.

Kwa ujumla kwenye hizi kampuni mtu unapokuja kuomba kazi ya ULINZI Kwa kipindi kile unatuma maombi idara ya mafunzo (training) na kuambatanisha kopi ya vyeti vyako alafu idara itachagua watu na kuwapigia simu kuja kwenye interview na mafunzo.

Katika mchakato Huu kuna mengi hutokea Kwa wale amabo tayari washalengeshwa na kupewa namba za wahusika miamala ya rushwa Huwa inafanyakazi Kwa kipindi hiko,jambo lingine hata kama Unataka kuajiriwa Kwa nafasi ya juu ndani ya kampuni hakikisha hauweki vyeti vyako vya elimu kubwa kwenye maombi Kwa sababu trainer hawataki kudeal na mtu aliyewazidi elimu maranyingi wanaweza kukufanyia figisu kwenye training mpaka ukashindwa kuendelea na mafunzo au kukutafutia sababu ukawa disqualified.kiukweli sehemu hii mabinti wengi hulazimika kutoa rushwa ya ngono Kwa wakufunzi ili apite kwenye mafunzo salama na wakufunzi nao si haba huwaramba sawa sawa mabinti

Mkishamaliza mafunzo mnapatiwa mkataba wa ajira na uniform za kazi na kitambulisho na kuhamishwa kutoka idara ya training na kupelekwa idara ya operations huku ndio kuna kuna balaa la kila Aina maana kuna majungu,fitna,visasi,ujuaji,mapenzi,deals na rushwa.

Ukishakabidhiwa upande wa operations wao huanza Kwa kuwapangia malindo maeneo mbalimbali ya mji .hapa watu wengi hupambana kupata malindo ya sehemu nzuri ikiwemo ofisi za balozi,kiwanda, town kwenye majengo makubwa na maeneo ya Karibu na mtu anapokaa.

Ili kupata Lindo zuri aiza liwe linavi-tip,Karibu na nyumbani au mazingira mazuri na yasiyo na purukushani au mteja mkorofi basi inabidi uishi vizuri na site commander na sector sagent wa Hilo eneo hivyo sector sagent na site commander nae hutaka chochote kitu kama we ni me,basi akikuweka kwenye lindo hilo la maana na linalipa basi mwisho wa mwezi Inabidi umkatie chochote kitu au kama ni jinsia ke basi hapo ni kumpa penzi Tu ili akuweke kwenye lindo la sivyo utakaa stand by mpka basi na kuwa kama releaver kazi yako kuziba magap ya watu ambao nilikuwa wapo off au likizo kitu ambacho Huwa kinatesa sana maana unakuwa huna post maalum mara Leo hapa kesho kule.

Ukiwa mlinzi Inabidi uishi na mteja vizuri I mean mhusika wa eneo mnalolilinda maana wao wananguvu ya kuzuia wew kutolewa kwenye lindo husika pale inapotokea umefanyiwa figisu figisu na site commander au sector sagent. Mara nyingi kama ukishindwa kwenda sawa na site kamanda au sector sagent au wenzio wamekufanyia figisu au kuna mtu wake sector sagent anataka kumleta Katika Lindo hukufanyia vitimbi mbalimbali ikiwemo kukataa ruhusa zako na hata akikubali hatafuti mtu wa kuziba gap ili usionekane mtoro Kwa site commander.

Mara nyingi wale watu wa Karibu wa sector sagent aidha awe kimada wake,ndugu yake au mshikaji Huwa wasumbufu sana kwenye lindo na sio wafanyaji kazi wengi ni wambea na wanapenda majungu hawapendi shift za night wengi wao wanataka wapangwe shift za mchana na kama akipangwa na supervisor getini basi jioni atayafikisha Kwa sector sagent ili aje kumchimba mkwala supervisor.

Itaendelea ........
 
Nakumbuka 2014 nikiwa kijana mdogo tu maisha yakanipiga nikaenda kuomba kazi ya ulinzi, nikapata. Sasa kuna afande mzee mzee hivi (zonal manager) akawa ananiuliza wewe na mwili huo mdogo utaweza kazi kweli au tukakufiche, inabidi ukafanye kazi kwa mkurugenzi kulinda nyumba halafu mkurugenzi mwenyewe hakai hapo kwa hiyo ni kulinda nyumba tu.

Kukawa kuna site supervisor mmoja mdada akamwambia afande huyu nipe mimi awe kwenye crew ya patrol, mzee akagoma kabisa ila mdada akakaza. Mwisho nikapewa hicho kitengo cha patrol tukawa kila siku usiku tunazungukia malindo yote. Kumbe yule matron alishanipenda ikawa anaweka mazingira ya kuliwa. Mwisho nikamla kweli na tangu hapo niliishi maisha mazuri kazini kuliko hata mkurugenzi wa kampuni, nikitaka kwenda kazini naenda nisipotaka basi usiku nakeshea mbususu ya matron mpaka alfajiri then naanza kuchochea tena mpaka saa 1 asubuhi. Tukitoka hapo ni simu tu namuombea ruhusa Hassan leo anajisikia kuumwa haji kazini, nawekewa supu na chapati nakula nikimaliza nalala tu.

Umarioo mtamu asikwambie mtu.
 
Nakumbuka 2014 nikiwa kijana mdogo tu maisha yakanipiga nikaenda kuomba kazi ya ulinzi, nikapata. Sasa kuna afande mzee mzee hivi (zonal manager) akawa ananiuliza wewe na mwili huo mdogo utaweza kazi kweli au tukakufiche, inabidi ukafanye kazi kwa mkurugenzi kulinda nyumba halafu mkurugenzi mwenyewe hakai hapo kwa hiyo ni kulinda nyumba tu. Kukawa kuna site supervisor mmoja mdada akamwambia afande huyu nipe mimi awe kwenye crew ya patrol, mzee akagoma kabisa ila mdada akakaza. Mwisho nikapewa hicho kitengo cha patrol tukawa kila siku usiku tunazungukia malindo yote. Kumbe yule matron alishanipenda ikawa anaweka mazingira ya kuliwa. Mwisho nikamla kweli na tangu hapo niliishi maisha mazuri kazini kuliko hata mkurugenzi wa kampuni, nikitaka kwenda kazini naenda nisipotaka basi usiku nakeshea mbususu ya matron mpaka alfajiri then naanza kuchochea tena mpaka saa 1 asubuhi. Tukitoka hapo ni simu tu namuombea ruhusa Hassan leo anajisikia kuumwa haji kazini, nawekewa supu na chapati nakula nikimaliza nalala tu.

Umarioo mtamu asikwambie mtu.

Kumbe unapitia magumu hivi ndio mana makasiriko mengi.
 
Hizi ndizo akili halisi za kijana wa Kitanzania..... Ngono, Ngono, Ngono.
 
Ways back miaka ya elf 2 nakumbuka nilikula training moja kali Sana viwanja vya mwamposa kawe jkt wakasome yule Mkenya retired army alitupigisha training hatari utadhani unaajiriwa na Wagner Group kumbe KK security aisee.

Pana siku nilizidiwa nikatoka nduki Cha kufia nini nilipofika home nikikumbuka msoto wa mtaa kesho yake nikawahi kwenda kuomba msamaha nikatoa sababu,wakaniambia awaajiri vichaa toka hapa.

Nikabembeleza sana aisee life msoto wakanikubalia.Nikamaliza training ya wiki mbili.

Wajinga wale mnalishwa wali maharage saa Saba baada ya kula mnaenda kuulipa uwanjani.

Nikapiga kazi mwaka mmoja huku napiga mishe zingine.

Supervisor alinielewa nikawa naingia usiku tu asubuhi naulamba kutembeza kaki maofisini jioni naingia Lindon, home narudi weekend.

Hakika safari ya maisha ni simulizi tosha.

Pana siku likapigwa Dili la kuingiza wezi waibe mafuta Depot za matenk ya mafuta kurasini.

Kazi ikapigwa tukapewa pesa mbuzi wajinga wanazijua koki zote kulingana na aina ya mafuta dizeli, petrol,taa.
Kumbe security manager nyuma ya geti Kuna nyumba ya Mzee mmoja informer wao akamnyoshea mchezo wote mzima asubuhi tukaitwa tukawekwa mtu kati.

"Niambieni ukwel au muende jela ikabidi tufunguke ni kweli mchezo tunaijua ikaripotiwa ofisin kwetu,wakatufukuza kazi.

Nikashukuru maana jela miaka 7 walitusaidia sana.

Baada ya kazi kuisha nikazama BOT kuendesha crane za ukutani za kupandisha mafundi juu enzi zile za ujenzi wa majengo pacha ya BOT, Nikiwa kwenye mchakato wa kuchukua Hela yangu nssf nifanye nauli ya kuchomoka south Africa.Nikapata kazi panono bongo safari ya South ikafa.
Mlinzi mwenzangu niliyekuwa nae tukilinda akapata kazi panono tukaja kutana nae CBE tukapiga bachelor siku hizi anaporomosha vituo vya mafuta tu.

Maisha ni safari kutoka kulinda hadi Leo nalala nimelindwa.

Usikate tamaa,usichague kazi.
 
Miaka kadhaa hapo nyuma Katika harakati za kupambana na maisha nimewahi kuajiriwa Katika kampuni kubwa ya ULINZI binafsi hapa nchini Kwa Wakati huo kulikuwa na kampuni kubwa za ulinzi hapa mjini kama nne hivi ambazo zilikuwa zinagombania soko la kulinda maeneo mbalimbali ya jiji ikiwemo mabanki,balozi,ofisi,viwanda na nyumba za matajiri.

Kwa kipindi kile Mimi niliajiriwa upande wa technical ambao mainly tulikuwa tuna-deal na security system ambazo ndani yake kuna masuala ya CCTV kamera,panick button system,intruder system, electrical fence, access control na vinginevyo.

Tuachane na upande wangu wa technical ambao nilikuwa. Leo nataka niongelee upande wa ulinzi (guards) ambao kutokana na experience yangu ndani ya kampuni niliyashuhudia na kuyasikia mengi ya ajabu hususani Mambo yanayohusisha rushwa ya pesa na ngono.

Kwa ujumla kwenye hizi kampuni mtu unapokuja kuomba kazi ya ULINZI Kwa kipindi kile unatuma maombi idara ya mafunzo (training) na kuambatanisha kopi ya vyeti vyako alafu idara itachagua watu na kuwapigia simu kuja kwenye interview na mafunzo.

Katika mchakato Huu kuna mengi hutokea Kwa wale amabo tayari washalengeshwa na kupewa namba za wahusika miamala ya rushwa Huwa inafanyakazi Kwa kipindi hiko,jambo lingine hata kama Unataka kuajiriwa Kwa nafasi ya juu ndani ya kampuni hakikisha hauweki vyeti vyako vya elimu kubwa kwenye maombi Kwa sababu trainer hawataki kudeal na mtu aliyewazidi elimu maranyingi wanaweza kukufanyia figisu kwenye training mpaka ukashindwa kuendelea na mafunzo au kukutafutia sababu ukawa disqualified.kiukweli sehemu hii mabinti wengi hulazimika kutoa rushwa ya ngono Kwa wakufunzi ili apite kwenye mafunzo salama na wakufunzi nao si haba huwaramba sawa sawa mabinti

Mkishamaliza mafunzo mnapatiwa mkataba wa ajira na uniform za kazi na kitambulisho na kuhamishwa kutoka idara ya training na kupelekwa idara ya operations huku ndio kuna kuna balaa la kila Aina maana kuna majungu,fitna,visasi,ujuaji,mapenzi,deals na rushwa.

Ukishakabidhiwa upande wa operations wao huanza Kwa kuwapangia malindo maeneo mbalimbali ya mji .hapa watu wengi hupambana kupata malindo ya sehemu nzuri ikiwemo ofisi za balozi,kiwanda, town kwenye majengo makubwa na maeneo ya Karibu na mtu anapokaa.

Ili kupata Lindo zuri aiza liwe linavi-tip,Karibu na nyumbani au mazingira mazuri na yasiyo na purukushani au mteja mkorofi basi inabidi uishi vizuri na site commander na sector sagent wa Hilo eneo hivyo sector sagent na site commander nae hutaka chochote kitu kama we ni me,basi akikuweka kwenye lindo hilo la maana na linalipa basi mwisho wa mwezi Inabidi umkatie chochote kitu au kama ni jinsia ke basi hapo ni kumpa penzi Tu ili akuweke kwenye lindo la sivyo utakaa stand by mpka basi na kuwa kama releaver kazi yako kuziba magap ya watu ambao nilikuwa wapo off au likizo kitu ambacho Huwa kinatesa sana maana unakuwa huna post maalum mara Leo hapa kesho kule.

Ukiwa mlinzi Inabidi uishi na mteja vizuri I mean mhusika wa eneo mnalolilinda maana wao wananguvu ya kuzuia wew kutolewa kwenye lindo husika pale inapotokea umefanyiwa figisu figisu na site commander au sector sagent. Mara nyingi kama ukishindwa kwenda sawa na site kamanda au sector sagent au wenzio wamekufanyia figisu au kuna mtu wake sector sagent anataka kumleta Katika Lindo hukufanyia vitimbi mbalimbali ikiwemo kukataa ruhusa zako na hata akikubali hatafuti mtu wa kuziba gap ili usionekane mtoro Kwa site commander.

Mara nyingi wale watu wa Karibu wa sector sagent aidha awe kimada wake,ndugu yake au mshikaji Huwa wasumbufu sana kwenye lindo na sio wafanyaji kazi wengi ni wambea na wanapenda majungu hawapendi shift za night wengi wao wanataka wapangwe shift za mchana na kama akipangwa na supervisor getini basi jioni atayafikisha Kwa sector sagent ili aje kumchimba mkwala supervisor.

Itaendelea ........
Mbona hakuna chochote Cha kustaajibisha
 
Sijui siku hizi enzi hizo usiku wazee wa madili hawalali.
Wizi wa magodown ulifanyika usiku kwa msaada wa walinzi.
Plus wazee wa doria.
Enzi hizo palikuwa na wizi wa mawasiliano ya simu.
Anakuja usiku mtaalamu anaingia kwenye control box ya TTCL anawaconnectia wahindi mjini wanapiga international call usiku kucha bill ikija inasoma kwenye kampuni au kiwanda husika.
 
mkeo lazima azagamuliwe
Wa kwako alizagamuliwa kaka ?
Maana mimi nimezikumbuka njaa za walinzi na kujipendekeza kwa mabosi wao wanakolinda .

Hapo bado hawajashinda njaa kutwa nzima alafu eti ukiwaita walinzi wanasema mimi ni askari sio mlinzi [emoji848]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom