Miaka kadhaa hapo nyuma Katika harakati za kupambana na maisha nimewahi kuajiriwa Katika kampuni kubwa ya ULINZI binafsi hapa nchini Kwa Wakati huo kulikuwa na kampuni kubwa za ulinzi hapa mjini kama nne hivi ambazo zilikuwa zinagombania soko la kulinda maeneo mbalimbali ya jiji ikiwemo mabanki,balozi,ofisi,viwanda na nyumba za matajiri.
Kwa kipindi kile Mimi niliajiriwa upande wa technical ambao mainly tulikuwa tuna-deal na security system ambazo ndani yake kuna masuala ya CCTV kamera,panick button system,intruder system, electrical fence, access control na vinginevyo.
Tuachane na upande wangu wa technical ambao nilikuwa. Leo nataka niongelee upande wa ulinzi (guards) ambao kutokana na experience yangu ndani ya kampuni niliyashuhudia na kuyasikia mengi ya ajabu hususani Mambo yanayohusisha rushwa ya pesa na ngono.
Kwa ujumla kwenye hizi kampuni mtu unapokuja kuomba kazi ya ULINZI Kwa kipindi kile unatuma maombi idara ya mafunzo (training) na kuambatanisha kopi ya vyeti vyako alafu idara itachagua watu na kuwapigia simu kuja kwenye interview na mafunzo.
Katika mchakato Huu kuna mengi hutokea Kwa wale amabo tayari washalengeshwa na kupewa namba za wahusika miamala ya rushwa Huwa inafanyakazi Kwa kipindi hiko,jambo lingine hata kama Unataka kuajiriwa Kwa nafasi ya juu ndani ya kampuni hakikisha hauweki vyeti vyako vya elimu kubwa kwenye maombi Kwa sababu trainer hawataki kudeal na mtu aliyewazidi elimu maranyingi wanaweza kukufanyia figisu kwenye training mpaka ukashindwa kuendelea na mafunzo au kukutafutia sababu ukawa disqualified.kiukweli sehemu hii mabinti wengi hulazimika kutoa rushwa ya ngono Kwa wakufunzi ili apite kwenye mafunzo salama na wakufunzi nao si haba huwaramba sawa sawa mabinti
Mkishamaliza mafunzo mnapatiwa mkataba wa ajira na uniform za kazi na kitambulisho na kuhamishwa kutoka idara ya training na kupelekwa idara ya operations huku ndio kuna kuna balaa la kila Aina maana kuna majungu,fitna,visasi,ujuaji,mapenzi,deals na rushwa.
Ukishakabidhiwa upande wa operations wao huanza Kwa kuwapangia malindo maeneo mbalimbali ya mji .hapa watu wengi hupambana kupata malindo ya sehemu nzuri ikiwemo ofisi za balozi,kiwanda, town kwenye majengo makubwa na maeneo ya Karibu na mtu anapokaa.
Ili kupata Lindo zuri aiza liwe linavi-tip,Karibu na nyumbani au mazingira mazuri na yasiyo na purukushani au mteja mkorofi basi inabidi uishi vizuri na site commander na sector sagent wa Hilo eneo hivyo sector sagent na site commander nae hutaka chochote kitu kama we ni me,basi akikuweka kwenye lindo hilo la maana na linalipa basi mwisho wa mwezi Inabidi umkatie chochote kitu au kama ni jinsia ke basi hapo ni kumpa penzi Tu ili akuweke kwenye lindo la sivyo utakaa stand by mpka basi na kuwa kama releaver kazi yako kuziba magap ya watu ambao nilikuwa wapo off au likizo kitu ambacho Huwa kinatesa sana maana unakuwa huna post maalum mara Leo hapa kesho kule.
Ukiwa mlinzi Inabidi uishi na mteja vizuri I mean mhusika wa eneo mnalolilinda maana wao wananguvu ya kuzuia wew kutolewa kwenye lindo husika pale inapotokea umefanyiwa figisu figisu na site commander au sector sagent. Mara nyingi kama ukishindwa kwenda sawa na site kamanda au sector sagent au wenzio wamekufanyia figisu au kuna mtu wake sector sagent anataka kumleta Katika Lindo hukufanyia vitimbi mbalimbali ikiwemo kukataa ruhusa zako na hata akikubali hatafuti mtu wa kuziba gap ili usionekane mtoro Kwa site commander.
Mara nyingi wale watu wa Karibu wa sector sagent aidha awe kimada wake,ndugu yake au mshikaji Huwa wasumbufu sana kwenye lindo na sio wafanyaji kazi wengi ni wambea na wanapenda majungu hawapendi shift za night wengi wao wanataka wapangwe shift za mchana na kama akipangwa na supervisor getini basi jioni atayafikisha Kwa sector sagent ili aje kumchimba mkwala supervisor.
Itaendelea ........