Unaweza kuwa na hoja nzuri lakini uwasilishaji ukafanya hadhira ikupuuze, mfano hapo umesema boya halikusaidii chochote ziwani...
Mm nauliza kati ya ziwa na bahari kipi kina nguvu na rabsha rabsha nyingi? Still tunaona vyombo vyote majini ( baharini ) boya halikosekani alafu wewe unasema halina msaada.
Ukiweka hoja jitahidi kidogo kuingia deep, kama hapo uliposema " Maji ya madolo sio ya swimming pool ", basi weka tabia za hayo maji ya madolo tujionee namna boya si lolote na si chochote kama hujui kuogelea.
Naomba kujua maana ya haya maneno / majina uliyotumia...
komezi
Buhanga
Mlimbe
Mwigundu
Ngezi
Kubwa kuliko yote hakuna MSOKE!!
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu unapokuwa madolo namaanisha maji ya mbali kabisa maji ya wanaume yani matosi lii!!
Huko mkizama (kumbuka uzamaji wa huko unatokana na upepo mkali na wimbi)
Kutokana na hayo maupepo yanayopiga hapo pamoja na mawimbi,
Hakuna boya linaloweza kukusaidia hapo!
Hata kama unajua kuogelea kiasi gani utaogelea wee utaishia kuchoka na kulala yo!!
Ponapona yenu kuwe na mtubwi mwingine karibu yenu na wanaokuwa kwenye huo mtumbwi wapate ujasiri wa kuwaokoa!
Tofauti na hapo lazima parapanda lilie!
KOMEZI ni aina ya upepo!
Sifa zake:
1.hukata mvua
Hata kama kuna mvua kubwa kiasi gani upepo huu ukianza lazima mvua ijisalimishe!
2.huvuma siku kumi na nne mfululizo kila mwaka mwezi wa saba. Kama uko mazingira ya ziwani ndio upepo unaovuma kipindi hiki
Na ndio kipindi ambacho wavuvi wanakufa sana kwa ajali!
3. Unapovuma hasa nyakati za usiku hufukunyua mawe na kokoto kutoka chini ya ziwa kuleta juu!!
Na ndio wakati tunaona maji yanapungua ziwani!
MWIGUNDU:
Huu nao ni aina ya upepo unaoleta mvua!
Yaani mkiwa ziwani mkauona huu upepo pamoja na mawingu kama mko karibu na kisiwa chochote lazima mkimbilie huko!!
Kwasababu unatabia ya kuleta mvua kubwa pamoja na wimbi kubwa sana!
Hasa ukiwa maji ya visiwa vya bumbile na kerebe wilaya muleba!!
MSOKE:
HUU NI HATARI!!!
ZAIDI YA HATARI!!
USIOMBE KUKUTANA NAO!!
Ni upepo unaoanzia chini kwenye maji,
unafukuta maji yanapanda juu kuelekea kwenye mawingu huku yakizunguka kama kimbunga!
Na kule kwenye mawingu utaona kama mawingu yanashuka kufata hayo maji yanayopanda juu!!
Sasa usiombe vikutane!!
Ndio utajua hivyo viboya vyenu huwa ni vya maonyesho tu!
na kazi yake ni kusaidia maiti ionekane haraka kwa sababu ya riflekta!! ( utanisahihisha)
Yaani hata kama wewe ni bingwa wa kuogelea lazima ulale yo!!
KUHUSU HAYO MAJINA MIMI SIJUI NI LUGHA GANI!!
KWANI NA MIMI NILIKUTA WENYEJI WANAITA HIVYO HIVYO!!
NIMECHOKA!!
MLIMBE NA NGEZI KESHO!!!!
ILA CHA AJABU MTU MWENYE GOVI ANA UWEZO WA KUUKATA HUO UPEPO!!!