SEHEMU YA 10
VITENGO
Jeshi kuna vitendo vingi kama Ngoma coy, Kwata, karate na kitengo cha kazi mchanganyiko
Kipindi cha kupewa vitengo ukawadia sasa hapa nitaanza kuelezea kitengo kimoja hadi kingine sababu vyote nilipita, nilipita ila sio kwa kupenda ni vile tu maswahibu yaliniandama.
1. KWATA
Service man walituambia siku ya graduation kuna watu hawatovaa kombat na mabuti "Nyie fikirieni mtu yupo kitengo cha kazi mchanganyiko siku ya gradu avae kombati ya nini? Ila ukiwa kwata kombati lazima uvae, tena nyie ndo mnaanza kupewa" akasema
"Ooh! Kumbe kwata kuna kuvaa kombati na mabuti ya jeshiii! Hicho kitengo ndo nakitaka" hapo namwambia Anna
Anna akasema mimi nitaenda ngoma coy kwata siwezi. Mimi kwata ilinishinda tokea kombania usiku tulivyokua tunafundishwa lakini nikasema acha niende ili nivae kombati siku ya graduu....
Wa kwata tukaambiwa tupange mistari uelekeo uwanja wa nyuma ya jeshi! Nimeusahau jina lake. Tunaenda kwa kuchapa mkono bega la kushoto umelikaza
Hao tukaanza kutembea huku tunachapa! Chapa chapa... mpaka tukafika.
Tukaekwa kimakundi, nikaangukia kundi la Afande nampa jina afande mzee sababu age ilikua imeshamtupa mkono.
Akaanza kutupa intro pale halafu akasema kupima uwezo wenu, wote tulale tumbo juu tuangalie jua hakuna kukwepesha macho.
Ule uwanja una jua kalii kichizi! Tukitoka kambini hali ya hewa nzuri tukiingia ule uwanja jua kali kinoma.
Kuruta tumelala macho juu! Ole wako ujile kazi unayo
Macho hadi yanatoa machozi watu tunakodorea jua.
Baada ya hapo kazi ikaanza
"Kwa mwendo wa pole mbele tembeaaa...
Nyuma geuka....
Mbele geuka kushota geuka....
Aya chap mguu..."
Wazee tunapiga kwata!!
Mwanzoni wengi tulikua nanga, afande mzee akawa anatuelekeza kwa upole pale, kadri muda unaenda mananga yanapungua ila mimi nilikua nanga pro...
Kuchapa mkono sijui, mguu siwezi!
Afande mzee ananiambia "kaza tako hilo mwendo wa polepole chapa mkono kwa ukakamavu"
Ikafika muda hadi mabao nikawa nakula
Hapo nilijuta nikasema kwata siwezi! Bora nihame kitengo
Muda wa kwata umeisha afande mzee akaniambia "kesho nisikuone kwenye kundi langu, sitaki mananga mimi"
Nilijisikia unyonge ila nikasema nakaza hukuhuku kwata! ili nivae kombati siku ya graduu.....
Usiku muda wa kombania service man akawa ananielekeza kwata pale kidogo nikapata mwanga nikasema kesho nitaweza.
Kweli bhana kesho nikawa nimejitahidi afande mzee akaridhika niendelee kubaki kundi lake.
Mpaka siku ya tatu wiki haijaisha style nyingi za kwata tukawa tumefundishwa, hapo mzozo kwangu ukaanza.
Nilikua nachanganya madensa.
Ikitajwa style hii mimi nafanya style nyingine.
" kuruta wewe hama kitengo kabla muda haujaenda! Kama kombati utavaa hata lililochakaa, waziiii!?
Nikamwambia wazii Afande!
Safari yangu na kwata ikawa imeishia hapoo!
Wiki haijaisha kule kwenye kwata lakini mwili una mabadiliko mengi hii ilikua kwa wote sanasana wacheza kwata.
nikivua nguo mwili una alama mbili nyeusi na weupe
Sehemu iliyofunikwa na nguo kweupe rangi niliyotoka nayo nyumbani, sehemu ambayo inabaki wazi nikivaa imekua nyeusi kama mkaa! Uso wote mweusii shingo nusu nyeupe nusu nyeusi.
Itaendelea...
Muendelezo soma
Niliyoyashuhudia Jeshini