SEHEMU YA 11
2. NGOMA COY
Nilimwambia Anna mimi kwata nishafukuzwa, akanishauri nihamie ngoma coy.
Ngoma coy wanajihusisha na sanaa kuimba, kucheza, kuigiza hivyo.
Nikapiga picha mimi kuigiza, kucheza, kuimba siwezi nitafanyaje sasa? Nikajipa moyo kesho nikaongozana na Anna kitengo.
Nimefika pale bakabaka akaniambia bora umekuja ngoma coy huku utawala kama wote! hamna jua wala kutumia nguvu. Sasa kuna mchujo humu huingii bure, wote unaowaona hapa wamefanya vizuri kipindi cha mchujo.
"Aya imba tukusikie sasa ndo mchujo huu usifanye masihara"
Mimi kuimba sijui
"Sasa hujui kuimba, hapa umefata nini? Aya cheza tuone"
Kuna mziki kabisa kwenye lile hall! Navyokwambia ngoma coy utawala ujue utawala kweli!!
Mziki unapiga nicheze! Anna ananiangalia anacheka tu, nikajikaza kucheza😄
Naona kuruta wananicheka na mimi najua hapa naharibu tu.
"Weeee! Kuruta kucheza unajua lakini sasa hapa tumeshajaa tupo wengi, jaribu vitengo vingine" akaniambia bakabaka
Majibu hayo tu nikajua nimeboronga kucheza hivyo kanikataa kiaina kama walijua wamejaa kwanini hakuniambia tokea mwanzo?......
Sasa niende wapi! Ngoma coy sijafit ila ningekubaliwa hapa ingekua utawala kama wote.
Nikarudi hangani mapema, sababu muda ulikua umebaki mwingi kuruta wapo vitengoni.
Hairuhusiwi kwenda hangani muda wa kazi hivyo nililala chini ya deka ili bakabaka wakipita wasinione.
Usiku kama kawaida kombania! Ukifika unakaa chini vumbi kama lote. Kipindi hiki tushamaliza zile first weeks za mateso hivyo tukawa hatupewi mazoezi magumu hivyoo!
Tunanyanyua viroba (squats) tukichoka tunaimba chenja mambo yakizidi tunaekewa mziki tucheze bakabaka wetu alikua na speaker ndogo.
3. KITENGO CHA KAZI MCHANGANYIKO
Nilivyotoka ngoma coy nikaja huku sasa.
Kazi mchanganyiko wanadeal na kufyatua tofali na kubeba, kuchimba visiki, kuvuna machungwa na kupukuchua mahindi, kumwagilia bustani ya mbogamboga bondeni, kusafisha vyoo, kufyeka nyasi.
Mwanzo nilijitahidi nikaekwa kundi la kuvuna machungwa! Bakabaka walituambia kula machungwa hadi usaze kubeba hairuhusiwi hivyo nilikula utawala sana shambani.
Mpaka shamba likawa jeupe tumevuna kila kitu
Hivyo kazi ya machungwa baada ya kama wiki ikafa tukawa hatuendi tena.
Nikawa najila ili niende kundi la bustani nikafanikiwa, kule pia utawala sana tunamwagilizia michicha spinach ila tatizo likaja bustani kwenda ni asubuhi na jioni tu. Mchana tunaambiwa twende shambani kung'oa visiki.
Huko shambani mbali kama 2km nikaona hiki kipengele kila siku kubeba visiki nikawa nalalamika sana.
Anna akaniambia kwanini usiende kitengo cha karate?
Nikafunga ukurasa na kazi mchanganyiko nikahamia karate rasmi!
Itaendelea.
Muendelezo soma
Niliyoyashuhudia Jeshini