Niliyoyashuhudia Jeshini

Niliyoyashuhudia Jeshini

Yes nimejichanganya nlimaanisha wa mujibu, wa kujitolea walikuja nyinyi mkiwa mnakaribia Kumaliza lakini mlikuwa mnafoleni pamoja usiku ila mnatenganishwa ninyi na wao.
Siku ya sherehe yenu nilicheka sana mayanga alipokuwa amevaa yale majani(kikundi cha singe)

Ujenzi wa uwanja walikamilisha wa kujitolea op makao
Hv nikitaja force namba yangu utajua nlikuwa Mwaka gn🙄

Force no BA14XX

Jadda

Prince Mhando
 
Lakini tofauti na majeshi ya nchi zilizoendelea huku kwetu bado tunachapana kama punda, kule kwa wenzetu ni matusi tu kama kawa lakini drill instructors hawaruhusiwi hata kumkunja recruit, huku kwetu afande anamnyuka kuruti utasema anapiga mtoto wake
naafiki huku si ustaarabuless unatusumbua. japo na kwa wenzetu napo kuna fimbo ya maneno utaambiwa maneno mpaka unaweza kujiuluza mara mbilimbili mm kweli mwanaume..utaambiwa maneno ya shombo na dharau mpaka unaweza kupata hasira upigane bure ama kupata morali mara dufu.
 
Duuh asee hakuna kitengo ninachokipenda na ninachokiona rahisi jeshini kama kwata huwa sielewi kwanini watu wanakichukia na kukiona kigumu

Yani mimi kwangu kwata ndio ilikuwa sehemu ya kupoozea machungu ya jeshi, maana mimi sipendi mabio wala mazoezi nakumbuka mwishoni mwa six weeks za kwanza, nilikosa kuwepo kwenye pass of square tu roho iliniuma sana

Nikasema kwenye graduu lazima niingie kitengo cha kwata, na kweli graduu nilikuwa kwata coy sema kimbembe kuweka silaha begani, hadi mfupa wa bega ukaanza kuuma nikawa naweka handkerchief

Yani mimi kiujumla jeshini vitu nilivyovipenda ni chenja, kwata, range (japo niliishia kulenga mijusi), syndicate na route march (kutembea tu), ila ukishaniambia nikimbie daah nilikuwa najionea tabu tu

Na yale maovyoovyo mengine nilikuwa siyapendi kabisa
Kwata nzuri ukiwa na mobility(ushirikiano wa viungo na akili)
Nguvu
Uhakika wa vitendo
 
Back
Top Bottom