Duuh asee hakuna kitengo ninachokipenda na ninachokiona rahisi jeshini kama kwata huwa sielewi kwanini watu wanakichukia na kukiona kigumu
Yani mimi kwangu kwata ndio ilikuwa sehemu ya kupoozea machungu ya jeshi, maana mimi sipendi mabio wala mazoezi nakumbuka mwishoni mwa six weeks za kwanza, nilikosa kuwepo kwenye pass of square tu roho iliniuma sana
Nikasema kwenye graduu lazima niingie kitengo cha kwata, na kweli graduu nilikuwa kwata coy sema kimbembe kuweka silaha begani, hadi mfupa wa bega ukaanza kuuma nikawa naweka handkerchief
Yani mimi kiujumla jeshini vitu nilivyovipenda ni chenja, kwata, range (japo niliishia kulenga mijusi), syndicate na route march (kutembea tu), ila ukishaniambia nikimbie daah nilikuwa najionea tabu tu
Na yale maovyoovyo mengine nilikuwa siyapendi kabisa