Niliyoyashuhudia Jeshini

SEHEMU YA 13
MAOKOTO

mwanzoni kuruta wote tulipewa kopo la uani na sanitizer sisi tukajua ni upendo tunapendwa sanaaa na bakabaka.
Mwisho wa mwezi ukafika kuruta njoeni kuna maokoto yenu jeshi tunawapa iwasogeze siku.

Tumekaa kombania bakabaka kashika burungutu mimi jina langu ni herufi ya mwanzo kwahiyo hela nilikua napewa wa kwanza

Nikaitwa jina nikaenda nikapewa hela halafu nisign, nikapiga jicho kwenye amount iliyoandikwa ni tofauti na niliyopewa, nikimaanisha nimepewa nusu ya hela.

Wote tukapewa tukaanza kuulizana vipi mbona tumepewa hela nusu?
Bakabaka akatuambia "Mlivyokuja mlichukua makopo yetu na sanitizer mlidhani tumewapa bure?"

Ikawa kila mwezi tunapewa maokoto nusu kisingizio ety tulivyokuja walitupa makopo na sanitizer zao!

NADHARIA YA WANAJESHI KUTEMBEA NA KURUTI

NIilivyotoka nyumbani usia ulikua kua makini huko wajeda sio watu wazuri!
Nikiri kwa nilichokiona WANAJESHI MNAWASINGIZIA!

Labda kama hiyo tabia ipo kambi zingine lakini kambi niliyokuepo mimi wanajeshi walikua wanajiheshimu sana.

Hawakua hata hivyo kusema wanatusumbua kuruta hapana.
Ila wanaoharibu sifa ni wale service man, wale ni vichomi kazi nyingi tunakua nao hivyo wanachukua nafasi hiyo kupenyeza nia yao ovu.

Ole wako service man umkatae utapata adhabu kama zote.
Mzazi usiogope mtoto kwenda kwa mujibu, faida ni nyingi kuliko hasara

"If it's bitter at the start, then it's sweeter in the end"
 
Hizi tips ningezipata mapema kuna mjomba wangu ningempatia alipoenda jeshini mwaka jana mwezi wa sita
 
Lazima alirudi kaharibika
 
Basi tunatofautiana maana ya madeko.
Kwangu hayo yote uliyoainish hapo ni madeko.
 
Hakuna MSU mimi naongea kitu ambacho nna uhakika nacho ungekuwa hapo usingekosea kuandika kifupi

Kile kituo ulichoshukia kinaitwa Resort wakati unareport ,shamba kule njiani ni majumba 6 yule mwalimu wa karate ni Ah*d ,
 
Asante kwa credits! Ethics muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…