SEHEMU YA 9
Tukaitwa kombania "Hongereni kwa kuweza kuvumilia wiki nzima bila kulala, hakika mmeiva kuruti. Ilitakiwa mkae wiki 6 bila kulala lakini tumewaonea huruma mtatufia wiki moja kwenu inatosha"
"Tii amri fungua moyo pandisha morali, jeshi ni zuri sana mlikuja mnalia ila sasa hivi mnafurahi na wiki hii ni ya kula utawala leo kwa mara ya kwanza tutawapa nafasi mkaoge, mfue nguo, mnyoe tutakutana na nyie baada ya chakula cha mchana"
Tulifurahi tukaenda angani kufanya kama tulivyoagizwa.
Nikiri jeshi kuna raha yake
Ratiba ilibadilika mateso yalipungua, kuna kazi haziepukiki kwenda shamba kung'oa visiki, kupukuchua mahindi, kubeba matofali, kubeba michanga, kumwagilizia bustani, kusafisha mazingira.
Ukiangalia ni kazi za kawaida na nzuri pia kama utafanya kwa moyo mmoja.
KUJIFUNZA KULENGA SHABAHA
Ratiba mpya ikaja baada ya chai tunaenda kombania kujifunza kulenga shabaha.
Wakati ule niliona kero na nilikua sisikilizi kwa makini nasinzia ila nilifanya jambo baya.
Somo lilikua zuri kwa waliokua makini aina za silaha, sehemu za silaha hapa nachokumbuka ni magazine kama sehemu ya kuhifadhia risasi, kitako cha bunduki na risasi zenyewe basi.
Sikumbuki kingine, Sinilijifanya Nanga acha nivune mabua.
Somo liliendelea mpaka wiki ikaisha ikabaki kwenda range kulenga shabaha.
Kumbuka mimi sikua nasikiliza darasani, hiyo siku tumeamka alfajiri kwenda huko range. Safari ilikua ndefu tunaenda kwa kukimbia ila sio kesi tukafika.
Tunasimama kimafungu kulenga shabaha wengi walikua nanga kama mimi hawakulenga lkn kufyatua risasi waliweza.
Zamu yangu ikafika nikalala chini service man akaniambia "vuta focus koki bunduki"
Nimeshika bunduki kukoki najua basi!? Nabung'aa macho
"Kuruta koki bunduki haraka"
"Afande nakoki haitaki" nikamjibu
"Wewe hujaiva! Si hivi nimeweza kukoki wewe unashindwa nini? Aya nishakoki fyatua risasi"
Nifyatue risasi! Nikavuta picha nikaona hichi kidude kinachocheza kwenye movie huwa wanakibinya... kumbuka kitako cha bunduki nimekiweka kwenye kwapa.
Basi nikakibinya! Weeee nilitoka ndukiii nalia...
Mimi nilijua ukipiga inakua kawaida tu kumbe nilivyofyatua bunduki ikanitetemesha mwili nikahisi kuzimia.
Nilichezea mabanzi! nikaambiwa naleta masihara ningejipiga risasi je?
Kuna kuruta alipewa zawadi alilenga shabaha 3 halafu anapiga risasi kwa ufasaha.
Ratiba tuliizoea kuamka alfajiri kurudi angani saa 6 usiku
Muda mwingine tukirudi tunajikuta tunapiga stori hadi kunakucha, wenyewe tunaamùa kukesha na kesho tunapiga mzigo fresh.
Nilipata wasaa wa kuongea na mama!
"Unaendeleaje"
Vizuri mama..
"Vipi bado unataka kurudi nyumbani"
Hapana! Nitakaa hadi nimalize course...
Akacheka sana.
Jeshi lilikua raha hadi wenzangu wakinikumbusha nilivyokua nalia najicheka.
Yule bakabaka mchumba ake namesake akiniona ananitania "Ephen naona umeiva!!"
Itaendelea.....
Muendelezo soma
Niliyoyashuhudia Jeshini