Tarehe 1 Jan 2026 (yaani Leo) nimesafiri kuja DSM, ninapoishi, kwa gari la KLM.
Kabla ya hii safari nilichukua lodge uchwara karibu na ofisi za Kilimanjaro hotel (bei elf 20). Wakati naenda kuchukua lodge ilikua majira ya saa kumi na mbili jioni. Nikapumzika mpaka saa tano, ilivyofika saa tano nikasema niende The picnic kusubiria mwaka kwani pako jirani na nilipolala.
Hamadi! Niliyoyashuhudia ni huzuni. Ufuska wa kutisha maeneo yote kuzunguka the picnic. Africana lounge, na grocery zingine kedekede.
Kwa kuwa sikutumia kilevi nilikua rada sana. Kuna makundi matatu ya Wala bata. Kuna watu unaona kabisa Wana fedha zao na magari, Kuna kundi la kati, halafu Kuna machaliii.
Machalii wamelewa pombe na bangi ni hawafai ni kuporomosha matusi ya nguoni, kutokujali magari, yaani wamejiachia full.
Malaya wenyewe ukiwaona ni huruma! Wamechoka kwa pombe na kukosa usingizi! Ili ulale na watu sampuli ile lazima uwe umekunywa pombe ya kutosha na wewe maana hawavutiii hata kidogo. Wapo wachache standard.
Mademu wamelewa wengine hata kutembea hawawezi wanakokotwa na wanaume wawili kupelekwa lodge.
Malaya wamekaa njenje wakiwa nusu uchi wakiwinda Kila wakikuona wanakuita! Sikutaka kabisa kujisogeza. Niliendelea kurandaranda hapo mpaka saa saba nikarudi kulala.
Nikiwa njiani nilikuwa naogopa sana maana wale vijana hawako kawaida kiakili. Sijawahi ona vijana wapo rafu na walevi kama Jana.
Kwa upande wa picnic wahudumu hawajachoka sura ni warembo na Wana mizigo (kwa wale wa kike) na wamevalia nadhifu, japo vibukta ni vifupi hadi huruma.
Wanaume huku na kule wanaongea na Malaya huku wakinywa pombe za bei. Vijana wanakatiza barabara bila kuangalia kama Kuna gari au la!
Aise nimeishi dar sijawahi ona uchafu wa namna ile. Wale mademu anayewagonga ni amekata tamaa!
Ukiacha watu wa faraja la juu walioenda kula pesa zao, Kuna kundi pale Yale ni maisha duni, ikiwa wanafanya starehe za hivyo Kila siku.
Mademu wamenona hovyo hovyo hovyo huelewi tako na tumbo ni lipi.
Upande wa bia ni zinanyeka kama vile hakuna kesho.
Ooo inatosha nitarudi siku na Mimi nikiwa nakunywa, nione kama nitaona kinyaa kama Jana na kuamkia Leo!
Chugaaaa!!!!!
1/1/2026.