JINN CATCHING
Nianze kwa kusema maelezo nitakayoyatoa kuhusu njia hii ya kumkamata jinni ni kwa mujibu wa
sheikh Abdorauf Benhalima nitajitaidi kufupisha kama mtu atakuwa na swali atauliza.
Nianze hivi, Nadhani wengi wetu tushaona mtu ana pandisha majini wengine husema kupandisha pepo sasa mtu anapokuwa katika hali ile maana yake jini ndio kamvaa mtu kinyume chake ni kuwa mtu anaweza kumvaa jini yaani mtu anamkamata jini hii ni kwa lazima jini ata kama hataki atakuja na atakuwa kakamatwa hio ndio jinn catching.
ili njia hii ifanye kazi ni lazima kuwe na catcher, Catcher ndio mtu atayemkamata huyo jini na sio kila mtu anaweza kuwa catcher ila ni mtu ambaye ashawahi kukumbwa na majini na majini yakaongea kupitia yeye ndio maana mwanzoni nikasema wale wanao pandishaga majini, hawa wanaweza kuwa catcher.
Sasa kwanini njia hii itumike?, Kwa mujibu wa sheikh anasema uchawi upo wa aina nyingi mtu anaweza fanyiwa uchawi na uchawi ule ukafukiwa, ukatupwa baharini, ukatupwa kwenye kisima ukazikwa makaburini n.k sasa ikiwa utamsomea mtu atapata nafuu lakini uchawi ule bado upo huko ulipowekwa hivyo mgonjwa atapata nafuu ila ataendelea kuumwa baada ya muda tena na ni ngumu wewe kujua uchawi unaomsumbua ulipo na ikatokea ukajua mfano umefukiwa makaburini ni ngumu wewe mwanadamu kufukua huko ndio maana njia hii inamwezesha tabibu kumuita jini aliyehusika katika huo uchawi maana uchawi ukifanyika majini waovu huulinda uchawi huo sasa jini yule akija anakuwa kakamatwa yeye na sio yeye kamvaa mtu na atalazimishwa autoe uchawi ule uko ulipo pamoja na mambo mengine kulingana na ugonjwa wa mtu.
Maelezo ni marefu ila kwa ufupi ni kuwa njia hiyo inafanyika kwa kusoma aya ya 196 ya surat al a`raf mara moja kisha utasoma aya ya 148 surat baqarah kuanzia aynama takoon mpka mwisho wa aya utairudia mara nyingi mpaka jini adhihiri.
إِنَّ وَلِيِّيَ اللَّـهُ الَّذِي نَزَّلَ الْكِتَابَ وَهُوَ يَتَوَلَّى الصَّالِحِينَ -- Araf --196 ayat
Inna waliyyi Allahu allathee nazzala alkitaba wahuwa yatawalla as-saliheen."
وَلِكُلّٖ وِجۡهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَاۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ أَيۡنَ مَا تَكُونُواْ يَأۡتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ--- baqara 148 ayat
Wa likullinw wijhatun huwa muwalleehaa fastabiqul khairaat; ayna maa takoonoo yaati bikumullaahu jamee’aa; innal laaha ‘alaa kulli shai’in qadeer.
Hii surat baqarah utaanzia hapo kwenye ayna maa takoonoo mpka mwisho kwa kurudia mara nyingi mpaka jini adhihiri.
N.B: Wapo baadhi ya masheikh wanampinga sheikh ben halima wakidai kuwa njia hii anayotumia sio sahihi na wametoa hoja zao na sheikh ben halima akatoa hoja zake pia kutetea njia hii hivyo kama wewe unapenda kujifunza zaidi unaweza ingia mtandaoni ukawasikiliza you tube video zao zipo nyingi tu.
sheikh amezunguka nchi nyingi sana kupamabana na wachawi na mashayatwiin na moja katika mada zake alizozifanyia jini catching ni pamoja na vita kati ya israel na palestina, barmurda triange, freemason,Pyramid za misri, Emarald book, vitabu vya imam ghazal, The coming of masih dajjal, vita vya somalia, vita vya nigeria,political issues kama za watoto kuuwawa sana zinapokaribia chaguzi katika nchi mbalimbali n.k zote hizo anakuwa anawakamata majini wanohusiana na kitu anachotaka kujua kisha ana jadiliana nao.
ukitaka kujifunza zaidi kuhusu njia hii ingia katika website yake linki hio
Site officiel BEN HALIMA ABDERRAOUF - Biographie, ses oeuvres, la roqya, le captage, spiritualités, démonstration de captage, vidéos, téléchargements
www.benhalimaabderraouf.fr
Arsis niliomba ulifafanue ili zaidi maana bado nalifanyia research pia