Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Da yaani ushirikina unaanzaga mdogomdogo baadaye unakuwa mchawi
 
Da yaani ushirikina unaanzaga mdogomdogo baadaye unakuwa mchawi
 
5...
Tunapoendelea na aya ya 27 inatoa ufumbuzi zaidi kuwa kilichokusudiwa siyo mfano wa mbu wala siyo mbu. Ingawa neno mbu limetumika lakini kilichokusudiwa ni yale makundi yanayofanya upotofu. Mtafsiri wa aya ya 27, Sheikh Ali Muhsin Barwani ametarjama hivi;

Q 2:27. Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara. 27

Ni wazi hata kwa kutumia hio tafsiri ya Barwani, kuwa "mfano wa mbu sio kusudio walla gaongelewi mbu, ispokuwa "mbu" kwenye aya ya 26 inamaanisha moja katika makundi ya uharibifu, kama inavyofafanua aa ya 27.

Katika aya ya 27 napo tunakumbana na tatizo lingine la watafsiri ambao hawajatumia mbinu ya kuifahamu Qur'an ya "tafsil" na ulimi (lisan) wa Ibrahim au "Abrahamic locution".

ٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مِيثَـٰقِهِۦ وَيَقْطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ ٢٧


27. Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara. 27

Nimeweka rangi ya njano kwenye maneno ya Kiarabu na ya tarjama ya Kiswahili; Mtarajama katumia maneno "uharibu katika nchi" kutafsiri maneno "ufisadi katika ardhi" kama yalivyo kwenye Qur'an.

Nasema kama yalivyo kwenye Qur'an kwa sababu maneno ufisadi na ardhi yanatokana na Kiarabu na neno lililotumika kwa Kiarabu "Yafsidun fil Ardh". utajionea kuwa hayana tofauti kubwa isipokuwa matamshi tu na Kiswahili.

Cha kujiuiza je, neno ufisadi linaweza pia kuwa "uharibifu", bila shaka ni ndiyo. Na neno "ardh" halina maaan nyingine zaidi ya ardhi hii tunayotembea juu yake? Jibu ni kuwa lina maana nyingine na ndiyo nina uhakika ilimaanisha hivyo, maana nyingine ya neno "ardh" katika Kiarabu ni "maandiko" (scripture). Hili kwa wale wanaofahamu Kiarabu ni wepesi sana kulijua. Ukiwa nchi za Kiarabu mtu akikwambia leta kwa maandishi (quotation) mapoatano yetu, atakwambia leta "ardh" yako. Sifahamu kwanini mtafsiri akaamua kuweka neno nchi kwenye tarjama yake.

Kwa maaa hiyo, mimi nawahakikishia kua maana kusudiwa hapo ni wale wanaofanya "ufisadi katika maandiko". Sababu ziko wazi, Bani Israel walikuta maandiko ya Musa (tawrat) wakayafisadi mpaka yakayapotea /potezwa kabisa na hata iliopo leo kwenye biblia sio "torati" kama wengi wanavyofikiria kwani hata ukiisoma biblia yenyewe inakwambia ni "kumbukumbu la torati".

Kwa maana hio basi Waislam tua mwongozo na igezo ambacho hakijawahi kupotezwa wala kubasilishwa na mtu toka kimeletwa (Qur'an) kwa sababu moja kuu na muhimu sana, Qur'an toka imekuja inahifadhiwa katika vifua vya watu, haijawahi kubadilika, ukienda China, ukija Tanzania, ukienda Marekani, Qur'an inabaki kua ni moja tu. Siongelei tafsiri naongelea Qur'an kwa lugha na ndimi zake iliyukuja nazo. Ndio ibaki kua rejea ya mwisho na uongofu kwa watu wote, ndio, watu wote sio Waislam peke yao, kwani yenyewe inasema;


Q 45:20. Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu, na rehema kwa watu wanao yakinisha. 20


...6
 
...7

Kama mnakumbuka tulisema juu kidogo hapo, kua njia mojawapo iliotumika kwenye Qur'an ni ya kiota. Kwa maana kua Qur'an yote na aya zake zote zimeshikana, huu ni muujiza mmojawapo wa Qur'an.

Mtarajama au mfasiri wa Qur'an akisema kua "neno hili limezidi au neno hili limewekwa kwa ajili ya matamshi tu" kwa kua tu halielewi maana yake, kwanini lipo, anatakiwa achimbe kwa kutafuta neno kama hilo au mzizi wake (root word) imetumika wapi kwengine ili upate maana kamili. neno mzizi huitwa "masdar" na wasomi wa lugha ya Kiaradu.

Wale wanaaofahamu maneno ya Kiarabu yanaundwa vipi wanafahamu maana ya neno "root word" (masdar), tunamaanisha nini kwenye Kiarabu. Maneno mengi ya Kiarabu yanaundwa kutokana na mzizi wa maneno matatu ya neno fulani.

Kuifatilia mzizi (masdar) kuichambua Qur'an (tafsil) neno kwa neno na kwa kutumia maana ya maneno kusudiwa kwa ndimi (lexicona au locution) za lilipoongelewa ndipo tunapopata ufumbuzi wa kuitafsiri maana halisi iliokusudiwa kwenye aya za Qur'an bila kutumia vielelezo vya nje ya Qur'an.

Waislam wengi, hususan wa kuwalaumu ni watasiri wa zamani, ambao wengi hufata kwa kua tu wamejijengea majina makubwa na wengine ni wazeew na wazai wetu ambao tumekuta wakifata mkumbo bila kuhoji wala kuuliza na wengi tunatishana, mpaka lehii, kua "kuuliza hayo utakufuru au 8unakufuru".

Hilo siliafiki, elimu bila kua na ushahidi. kwa mfano unapoulizwa "umetoa wapi kua adam ni mtu wa kwanza kuumbwa" au Hawa umemtoa wapi? unashindqa kujibu au unaana kubabaika. Kinachotakiwa ujibu ukweli wako tu na kama ukiona hakuna ulipolitoa na au ulipolitoa hata wewe mwenyewe unaona haya kusema kweli, elewa kua hilo sio sahihi au hulijui vizuri, unatakiwa uulize (inquisitive) nimesoma hapa JF, kuna Muislam aliwahi kuandika kua "Uislam sio dini ya Misukule" ya kukubali kila unchoambiuwa bilka kuuliza".

Nakubaliana nae mia kwa mia. Ni wajibu wa kila Muislam na asie Muislam kuuliza kila fundisho la Kiislam aneliongelea amelitoa wapi? kwa sababu kuna Waislam waliopotoishwa na wao wanaendelea kupotosha wengine na kuna vikundi vya watu wnaofanya ufisadi wa maandiko kwa makusudi kabis. Kwa hio mnaonisoma wote, mkiwa Waislam na msio Waislam, mpo huru kuuliza chochote, wakati wowote kuhusu yote ninayoyaandika nimeyatoa wapi. Na nikikupa nikupe na ushahidi, kama sina ushahidi hayo yanabaki kua ni angu bonafsi na sio ya Muumba wetu, mwongozo waa Muumba wtu ni Qur'an na Qur'an ipo, kwanini ukosekane ushahidi?

Tunasema elimu ni ujuzi wenye ushahidi (education is evidence-based knowledge). kama uliyatoa uyajuayo kwa wazee wako tu, sema ukweli, kama uliyatoa kwenye vitabu vingine, sema ukweli.

Kosa kubwa linafanyika hivi sasa na watarjama wamengia mkenge, ni kuitafsiri Qur'an kwa kutumia vilivyomo kwenye biblia. Narudia hilo ni kosa kubwa sana, kwa kua Qur'an ni maneno ya Muumba wetu, hayo ni bora kuliko maneno ya binadam au shetani yoyote yule.

...7
 
katika hiki kisa cha Adam wanaokisoma wote wakiisoma post, wagonge like au mshangao, au masikitoko, au makasirisho. Nielewe tu kua imesomwa na fulani na fulani, hususan ningependelea Lidafo Etugrul Bey Nourhan FaizaFoxy na wengine wote wakipitie na kukifatilia kisa hiki cha Adam, kina mafunzo mengi sana ndani yake.

Nipo tayari kujibu chochote katika haya niandikayo, hii ni elimu.
Simba.
 
وَيَنْبَغِي أَنْ تَدْفَعَ رِسَالَةً رَسْمِيَّةَ تُرَافِقُ عَرْضَ الْأَسْعَارِ لِلْبَيْعِ.
neno ardh ni kweli limetumika hapa kama quatation. na sio ardhi kwa maana ya earth.
swal langu.wakat wa kisa miraj niliwah kusikia jibril huwa anapewa aya kuzishusha ila anapewa si kwa lugha ya kiarabu ispokuwa anakuja kuifikisha kwa lugha ya kiarabu dunian.je ninkweli?
 
Mimi nitalike kila post yako kwa maana ya kwamba tupo pamoja nafuatilia mada kama ulivyoshauri
 
Ww bwana usizunguke mara tafsiri mara hili kama adam sio binadam wa kwanza utuambie wa kwanza alikua nani?
Evidence tutaenda kutafuta
 
Mimi nipo nakusoma sana, toka ulipoanza tena kisa cha Adam post #3833 mpaka hapa ulipofika.
. Nitakuwa na maswali mengi sana lakini nasubiri nwendelezo wako.
 
Ambacho hajuwi si jibu wewe? Kwani alificha? Hata habari ya majini mbona kaandika humu kuwa anaileta kwa imani yake ya Kiislam.

Ninachomkubali mimi, hajakataza mtu yeyote kuleta chochote jwa imani yake isipokuwa katusisitiza Waislam tutumie Qur'an kwenye hoja zetu.
 
Je Arsis anaweza kutabiri mambo yajayo..kama ilivyo kuwa kwa shehe yahya ..kama ndio emu atabiri jambo moja kati ya mwaka huu hapo..ndipo ntaa Amin angalau
 
Huyu jamaa ni muongo tu, hakuna cha arsis wala nini mada sake zime jikita kwenye uislam tu maswli mengine anaya kwepa, Mara atajibu simba Mara sijuwi Arsis
Lugha kali sana unatumia, kwani kuna ugomvi ndugu yangu?

Kama jibu silijuwi na anaelijua ni mwingine, nikisema atalijibu yeye ni kosa?
Unaonesha hujaupitia uzi vizuri, hilo Arsis aliliona ukapita uamuzi, tulisema sasa tujibu tu, bila kusema nani anajibu.

Jibu utalolipata ujue limetoka kwetu sote. Simba na Arsis.
 
Acha kupotezea watu muda
 
Ww bwana usizunguke mara tafsiri mara hili kama adam sio binadam wa kwanza utuambie wa kwanza alikua nani?
Evidence tutaenda kutafuta
Hilo la adam mbona tumelijibu sana, kwa kua unaonesha hujaupitia uzi vizuri, jibu ni hili...

Qur'an haijaandika mtu wa kwanza ni nani.

Siwezi kutia yangu ya kubuni au kuyatoa nje ya Qur'an.
 

Katika Uislamu kuna kitu kinaitwa Bidaa yaani uzushi katika Dini ... Nakupa mfano wa kina Dr sule ..sheikh yahaya na watu mfano wao .. tiba zao zinazohusisha majini wanaziingiza au kunasabisha na Uislamu bidaa au uzushi wa aina hii ukifumbiwa macho , unakuwa ushirikina then unapanda daraja na kuwa uchawi ... Mtume wetu Mohammad S.A.W kama kiigizo chetu katika uislamu na maswahaba zake hawakuwahi kutibu kutumia majini au kushirikisha majini ..
 
Acha kupotezea watu muda
Mbona unakasirika bila ya sababu?

Hapa ni jukwaa huru. Karibu sana na wewe utupe elimu na ujuzi wako ulionao. Sisi wetu ndio kama unavyotusoma. Hakuna kigezo wala mipaka kwenye elimu.

Kama kitu hujakielewa usikasirike, uliza maswali.

Hkienda page namba 1 ya uzi huu, utapunguza kupoteza muda, tumeweka links za mada zilizomo.
 
Nimefurahi sana kwa mchango wako mzuri, michango namna hio ndio inatoa elimu kwa wengi wetu kwa tudioyajua.
Nimekuelewa sana unachosema. Nina maswali maafupi sana.

Hayo mafunzo ya "bidaa" umeyaona wapi kwenye huu uzi?

Wewe hio elimu ya kujua hii na hii si "bidaa" umeitolea wapi?

Unafahamu maana ya Qareen?

Mtume wetu alikua nae Qareen au alikua hana?

Qur'an si imeletwa kupitia kwa mtume Muhammad?

Haijaleta kisa cha mtume Suleiman?
Simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…