5...
Tunapoendelea na aya ya 27 inatoa ufumbuzi zaidi kuwa kilichokusudiwa siyo mfano wa mbu wala siyo mbu. Ingawa neno mbu limetumika lakini kilichokusudiwa ni yale makundi yanayofanya upotofu. Mtafsiri wa aya ya 27, Sheikh Ali Muhsin Barwani ametarjama hivi;
Q 2:27. Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara.
27
Ni wazi hata kwa kutumia hio tafsiri ya Barwani, kuwa "mfano wa mbu sio kusudio walla gaongelewi mbu, ispokuwa "mbu" kwenye aya ya 26 inamaanisha moja katika makundi ya uharibifu, kama inavyofafanua aa ya 27.
Katika aya ya 27 napo tunakumbana na tatizo lingine la watafsiri ambao hawajatumia mbinu ya kuifahamu Qur'an ya "tafsil" na ulimi (lisan) wa Ibrahim au "Abrahamic locution".
ٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مِيثَـٰقِهِۦ وَيَقْطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ
وَيُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ ٢٧
27. Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na
wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara.
27
Nimeweka rangi ya njano kwenye maneno ya Kiarabu na ya tarjama ya Kiswahili; Mtarajama katumia maneno "uharibu katika nchi" kutafsiri maneno "ufisadi katika ardhi" kama yalivyo kwenye Qur'an.
Nasema kama yalivyo kwenye Qur'an kwa sababu maneno ufisadi na ardhi yanatokana na Kiarabu na neno lililotumika kwa Kiarabu "Yafsidun fil Ardh". utajionea kuwa hayana tofauti kubwa isipokuwa matamshi tu na Kiswahili.
Cha kujiuiza je, neno ufisadi linaweza pia kuwa "uharibifu", bila shaka ni ndiyo. Na neno "ardh" halina maaan nyingine zaidi ya ardhi hii tunayotembea juu yake? Jibu ni kuwa lina maana nyingine na ndiyo nina uhakika ilimaanisha hivyo, maana nyingine ya neno "ardh" katika Kiarabu ni "maandiko" (scripture). Hili kwa wale wanaofahamu Kiarabu ni wepesi sana kulijua. Ukiwa nchi za Kiarabu mtu akikwambia leta kwa maandishi (quotation) mapoatano yetu, atakwambia leta "ardh" yako. Sifahamu kwanini mtafsiri akaamua kuweka neno nchi kwenye tarjama yake.
Kwa maaa hiyo, mimi nawahakikishia kua maana kusudiwa hapo ni wale wanaofanya "ufisadi katika maandiko". Sababu ziko wazi, Bani Israel walikuta maandiko ya Musa (tawrat) wakayafisadi mpaka yakayapotea /potezwa kabisa na hata iliopo leo kwenye biblia sio "torati" kama wengi wanavyofikiria kwani hata ukiisoma biblia yenyewe inakwambia ni "kumbukumbu la torati".
Kwa maana hio basi Waislam tua mwongozo na igezo ambacho hakijawahi kupotezwa wala kubasilishwa na mtu toka kimeletwa (Qur'an) kwa sababu moja kuu na muhimu sana, Qur'an toka imekuja inahifadhiwa katika vifua vya watu, haijawahi kubadilika, ukienda China, ukija Tanzania, ukienda Marekani, Qur'an inabaki kua ni moja tu. Siongelei tafsiri naongelea Qur'an kwa lugha na ndimi zake iliyukuja nazo. Ndio ibaki kua rejea ya mwisho na uongofu kwa watu wote, ndio, watu wote sio Waislam peke yao, kwani yenyewe inasema;
Q 45:20. Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu, na rehema kwa watu wanao yakinisha.
20
...6