Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Kumbe ninapoteza muda na mtu aliyeishia kidato cha nne.

Ndio maana basi..
Naam, nimekuuliza sana jina "mtanashati" maana yake nini na limenzia wapi. Nikakuuliza elimu ya Antropolijia unaifahamu? Naona yote yamekushinda kujibu msomi wetu.

Sasa ngoja form IV nikupe kidogo nikijuacho kwa ufupi kuhusu hayo mawili.

1) Antropolojia; Ni somo, sana linakua kl utafiti wa kujua chanzo cha maneno au tabia fulani au mchezo fulani. Nilikuuliza wewe kwa ajili ya hili neno "mtanashati".

Uzuri katika elimu ya Uislam ndio mabingwa wa antropolojia kwa sababu Uislam sio elimu butu, ni lazima kila neno kila tabia au mwenendo wa Kiislam ufahamike chanzo chake.

2) Mtanashati; Hili neno lilianzia huko Mvita (natumai unapafahamu) Kwa Kwa Kiswahili cha mvita hawawezi kusema mchana, wao husema "mtana" sasa unganisha "mchanashati" ujielezee kwaninni mpaka uwe 'mtanashati"?

Huu sisi tunauita uchokozi wa kielimu, kama mvita tungesema "utokozi wa kiilm".
Simba.
 
Umeandika ujinga.
 
Nakusihi jikite kwenye kisa cha Adam, wacha uchokozi.
Binafsi nafatilia kwa umakini sana kisa cha Adam. Bahati nzuri hiyo mada naifahamu, na sasa naipata kutokea upande mwingine.
 
Umegusia aya zisizo zidi 10 Mtume alielezea je naweza zifahamu na hayo maelezo ni yap??
 
8...
Katika tafsil ya aya 26 na 27 nimewapa vifungu muhimu tu, kama utangulizi wa Kisa cha Adam. Lakini aya hizo tunaweza kuzifanyia tafsil ya kina ya neno kwa neno, watu wakapata kuelewa jinsi tunavyofanya tafsil na kutumia mbinu zingine tunazofundoishwa na Qur'an yenyewe kuielewa Qur'an.

Nimeona kila itapobidi tutafanya hivyo lakini post hii tujikumbushe mbinu zinazotumika na zilizopo ndani ya Qur'an ili twende huku tunayo post ya rejea.

Tutaelezea baadhi ya mbinu na maneno tuliyoyapata maana yake nyingine baada ya kutumia mbinu za Qur'an.

1) Tafsil; kwa ufupi ni uchambuzi kwa kufafanua, na kuna sura ya Q 41 Fussilat inatufundisha hilo.

2) Ndimi (lisan) ya Ibrahim (Abrahamic locution), hii nayo tunaipatakila tunapoitaja "Milat Ibrahim".

3) Kiota (nested); Hii ni mbunu na muujiza wa Qur'an kua maneno na mpoaka herufi zake zimeungana na hakuna isiokua na maana yake au iliozidi bila kua na kazi yake.

4) Ardh; Sehemu nyingi kwenye Quran haimaanishi ardhi (earth) bali humaanisha ni maandiko (scripture).

Tutakua tunaijazilia post hii maa kwa mara na tutazielezea kwa kina kila tunavyoendelea. Hapa naonesha tu istilahi (terminologies) za mbinu tunazotumia kupata maana sahihi iliokusudiwa zaaidi ya tarjama za neno kwa neno au tafsiri zilizotumia vitabu vingine kuitafsiri Qur'an.

Tunatumia Qur'an yenyewe kama msingi wa ushahidi (primary source), kikitajwa kitabu cha nje ya Qur'an kama ni hadith au cha lugha, au tafsiri, itakua ni msisitizo wa kukazia tu hoja lakini sio kama ushahidi wa msingi wa hii tafsil tuifanyayo. Usichanganye neno "tafsil" na "tasir" ni maneno mawili tofauti..

Kama hujaelewa kitu uliza au kama una maoni au tunachohitilafiana kilete na ushahidi wako sio mano yako tu, tukijadili.
Simba.
 
Umegusia aya zisizo zidi 10 Mtume alielezea je naweza zifahamu na hayo maelezo ni yap??
Hio ilikua ni kusisitiza tu kua hakuna alipotajwa au kuelezwa Adam kua ni mtu wa kwanza na kusisitiza kua Bwana Mtume Muhammad (SAW) hajafanya tafsiri ya Qur'an.

Tafsiri zimekuja kufanywa miaka zaidi ya 200 toka kuondoka kwa Mtume. Nakushauri soma historia ya tafsiri, utanielewa.
Simba.
 

Q 17:81. Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke! 81
 

Ahsante kwa maswali mazuri .. mimi bado Taalib ilmu ni mwanafunzi ..lakini katika uanafunzi wangu .. Bidaa kuijua hainitatizi.. mwanzoni mwa uzi wako ulimention kwamba babu yako anaagua na kwenda kuswali .. wewe mwenyewe ulilala pangoni kupewa mikoba ya uganga hapohapo unaotakidi ni swala tano ... Kwa ufupi mnafanya ushirikina na ibada .. ni kitu ambacho si sahihi kwa mafundisho ya wema waliotangulia....

Kuhusu Qareen hebu nijuze nini maana ya qareen as I told you earlier bado ni talib ilmu nipo tayari kujifunza elimu iliyo sahihi kwa misingi ya Mtume pamoja na maswahaba wake ...

Kuhusu Suleiman, ni kweli yeye alipewa mamlaka kutoka kwa Allah ambayo hakuna yoyote atakaye na aliyepewa baada ya yeye , kuna hadithi sahihi .. mtume aliwahi kupambana na jini na akawaambia maswahaba zake kwamba kama isingelikuwa kiapo ambacho Suleiman aliomba Allah kwamba asitokee mwingine baada yake mwenye uwezo kama wake basi yule Jini angemfunga kwenye kigogo ili watu waje wamshuhudie... Kiigizo chetu sisi ni Mtume na hakutaka kuwatumia wala kuwafuga majini kwanini wewe ufanye hivo?! Unless otherwise wewe ni mshirikina au mchawi au kafiri ..
 
Naam, nafuatilia unaenda vizuri, bado nasubiri muendelezo wa hizo aya mpaka tufike kwenye baqarah aya ya 30
 
Hili nakubaliana na wewe, tena naongezea kidogo, tukisoma historia ya tafseer ya zamani zaidi iliyotufikia kimaandiko ni ya ibn Jarir Al Tabari, inayisemekana iliandikwa miaka 200 mpaka 300 baada ya Mtume Muhamnad Sala Allahu alayhi wasalam.
 
Naam, nafuatilia unaenda vizuri, bado nasubiri muendelezo wa hizo aya mpaka tufike kwenye baqarah aya ya 30
In shaa Allah tutafika na zaidi, hii elimu ni ya kina sana, ndio maana naenda nayo taratibu, nikiijaza mistari na nikianza kuchambua kwa kina, basi hata hizo aya 2 nilizoanzia kuzigusia kijuujuu tu ya 27 na 28 ingetubisi tupige zaidi ya kurasa 50 mpaka 60 kuzichambua. Tafsil ni kuchambua neno kwa neno na herufi kwa herufi ya Qur'an.
Simba.
 
Hili nakubaliana na wewe, tena naongezea kidogo, tukisoma historia ya tafseer ya zamani zaidi iliyotufikia kimaandiko ni ya ibn Jarir Al Tabari, inayisemekana iliandikwa miaka 200 mpaka 300 baada ya Mtume Muhamnad Sala Allahu alayhi wasalam.
Kweli, waandishi wengi wamemnukuu Tabari, kama ni ya ukweli ni yeye au ni yao ajuae ni Muumba wetu tu, kwani hakutuahidi kua atazilinda hadeeth na tafaseer nje ya Qur'an yenyewe.

katika hayo kwa kuwa Maulamaa wamejitahidi kivyao, Tuchukue kwao katika yale yanaoendana na Qur'an tu. Yaliozusha (bidaa) ambayo hayamo kwenye Qur'an, mfano wa hili kua adam ni 'mtu wa kwanza kuumbwa' kama wameliongelea na halimo kwenye Quraan, tuyaache.
Simba.
 
Naomba jibu maswali niliokuuliza ili twende kielimi, ili kitu unachokijua tukijue kwa elimu yako sio kwa maneno yako. Elimu ni ufahamu wenye ushahidi.

Nimefurahi sana kukusikia ukisema wewe ni "Talib ilm" kwa wingi wetu na lisan za sasa? Tunakua Taliban, au sio?

Maswali niliokuuliza myepesi sana. Au hujayajua niyarudie kiwepesi zaidi?
Simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…