Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Kumbe ninapoteza muda na mtu aliyeishia kidato cha nne.

Ndio maana basi..
Naam, nimekuuliza sana jina "mtanashati" maana yake nini na limenzia wapi. Nikakuuliza elimu ya Antropolijia unaifahamu? Naona yote yamekushinda kujibu msomi wetu.

Sasa ngoja form IV nikupe kidogo nikijuacho kwa ufupi kuhusu hayo mawili.

1) Antropolojia; Ni somo, sana linakua kl utafiti wa kujua chanzo cha maneno au tabia fulani au mchezo fulani. Nilikuuliza wewe kwa ajili ya hili neno "mtanashati".

Uzuri katika elimu ya Uislam ndio mabingwa wa antropolojia kwa sababu Uislam sio elimu butu, ni lazima kila neno kila tabia au mwenendo wa Kiislam ufahamike chanzo chake.

2) Mtanashati; Hili neno lilianzia huko Mvita (natumai unapafahamu) Kwa Kwa Kiswahili cha mvita hawawezi kusema mchana, wao husema "mtana" sasa unganisha "mchanashati" ujielezee kwaninni mpaka uwe 'mtanashati"?

Huu sisi tunauita uchokozi wa kielimu, kama mvita tungesema "utokozi wa kiilm".
Simba.
 
Naam, nimekuuliza sana jina "mtanashati" maana yak nini na limenzia wapi. Nikakuuliza elimi ya Atropolijia unaigfahamu, naoina yote yamekushinda msomi wetu.

Sasa ngoja fprm IV ni kupe kidogo nikijuacho kwa ufupi kuhusu ayo mawili.

1) Antropolijia; Ni somo, sana linakua kl autafiti wa kujua chanzo cha maneno au tabia fulani au mchezo fulani. Nilikuuliza wewe kwa ajili ya hili neno mtanashati.

Uzuri katika elimu ya Uislam ndio mabingwa wa antropolojia kwa sababu Uislam sio elimu butu, ni lazima kila neno kila tabia au mwenendo wa Kiislam ufahamike chnzo chake.

2) Mtanashatiu; Hili neno lilianzia huko Mvita (natumai unapafahamu) Kiswahili cha mvita, hawawezi kusema mchana, wao husema "mtana" sasa unganisha "mchanashati" ujieleze kwaninni mpa auwe 'mtanashati"?

Huu sisi tunauita uchokozi wa kielimu, kama mbvita tungesema "utokozi wa kiilim".
Simba.
Umeandika ujinga.
 
Naam, nimekuuliza sana jina "mtanashati" maana yake nini na limenzia wapi. Nikakuuliza elimu ya Atropolijia unaifahamu? Naona yote yamekushinda kujibu msomi wetu.

Sasa ngoja form IV nikupe kidogo nikijuacho kwa ufupi kuhusu hayo mawili.

1) Antropolojia; Ni somo, sana linakua kl utafiti wa kujua chanzo cha maneno au tabia fulani au mchezo fulani. Nilikuuliza wewe kwa ajili ya hili neno "mtanashati".

Uzuri katika elimu ya Uislam ndio mabingwa wa antropolojia kwa sababu Uislam sio elimu butu, ni lazima kila neno kila tabia au mwenendo wa Kiislam ufahamike chanzo chake.

2) Mtanashati; Hili neno lilianzia huko Mvita (natumai unapafahamu) Kwa Kwa Kiswahili cha mvita hawawezi kusema mchana, wao husema "mtana" sasa unganisha "mchanashati" ujielezee kwaninni mpaka uwe 'mtanashati"?

Huu sisi tunauita uchokozi wa kielimu, kama mvita tungesema "utokozi wa kiilm".
Simba.
Nakusihi jikite kwenye kisa cha Adam, wacha uchokozi.
Binafsi nafatilia kwa umakini sana kisa cha Adam. Bahati nzuri hiyo mada naifahamu, na sasa naipata kutokea upande mwingine.
 
Arsis; Swali zuri sana.

Wanatumia bila kujijua, wamekua "brain washed" na hawaelewi tofauti, kwa sababu wanafata tafsiri. Hivi visa na mafundisho ya biblia yaliingizwa miaka mingi sana kwenye tafsiri za Wur'an sio Qur'an yenyewe. Ilianza baada ya kufa Mtume Muhammad.

Mtume, hakuitafsiri Qur'an, wanamzushia eti katafsiri. Mtume hakuna aya zaidi ya 10 au ishirini ndizo alielezea maana yake. Tafsiri zingine zote ni za kutunga au kugtokea biblia au fantasy za waandishi wa tafsiri, kama alfu lela u lela tu.

Mkiependa kujua zaidi kuhusu historia ya hadithi na kuna majina makubwa ya watu wa hadithi kwenye vitabu vyao wanakiri kuna visa wamevielezea kutokana na biblia, hii ni kwa kutokujua ubora na umuhimu wa Qur'an au kwa kudhani watu wataelewa zaidi wakifanya hivyo. Na wengine ni kwa makusudi kabisa ili wapotoshe ubora wa Qur'an.

Pia mkipenda kujua zaidi elimu ya Qur'an bila kutumia hadithi za kujitungia, ulizeni maswali kama hili, yenye nguvu. Kuna njia nyepesi za kila mmoja wetu kuweza kutambua hii hadithi ya kwe;i au sio hya kweli.

Kama mnakumbuka kuna mtu kaleya mstari juu huko, kaupamba kwa Kiarabu nikamuuliza aya ipi hii? Akajibu hadithi, nikamwabia hadithi ipi hio? Hajajibu tena, sasa ananisoma kwa kunusa nusa tu. Namwambia usofanye hivyo, sio elimu hio. Kama yalikua ni maneno ya mshairi sema tu ni mshairi, kama hujui yametoka wapi na uliyasikia tu, sema hayo nilisikia tu lakini sina elimu nayo yametoka wapi.

Tuytumie hili jukwa kujua mengi sana. Ya dini, ya sayansi, ya ulimwengu. Ya dhahiri na siri za kidunia. Tusowe na jazba kama hatujui kitu au tunas shaka nacho, sisi hatuwezi kujua kila kitu, isipokua tunasema umri huongeza maarifa na busra, nadio elimu yenyewe hio.

Hakuna zaidi ya Allah na mafundisho yake.
Arsis.
Umegusia aya zisizo zidi 10 Mtume alielezea je naweza zifahamu na hayo maelezo ni yap??
 
...7

Kama mnakumbuka tulisema juu kidogo hapo, kua njia mojawapo iliotumika kwenye Qur'an ni ya kiota. Kwa maana kua Qur'an yote na aya zake zote zimeshikana, huu ni muujiza mmojawapo wa Qur'an.

Mtarajama au mfasiri wa Qur'an akisema kua "neno hili limezidi au neno hili limewekwa kwa ajili ya matamshi tu" kwa kua tu halielewi maana yake, kwanini lipo, anatakiwa achimbe kwa kutafuta neno kama hilo au mzizi wake (root word) imetumika wapi kwengine ili upate maana kamili. neno mzizi huitwa "masdar" na wasomi wa lugha ya Kiaradu.

Wale wanaaofahamu maneno ya Kiarabu yanaundwa vipi wanafahamu maana ya neno "root word" (masdar), tunamaanisha nini kwenye Kiarabu. Maneno mengi ya Kiarabu yanaundwa kutokana na mzizi wa maneno matatu ya neno fulani.

Kuifatilia mzizi (masdar) kuichambua Qur'an (tafsil) neno kwa neno na kwa kutumia maana ya maneno kusudiwa kwa ndimi (lexicona au locution) za lilipoongelewa ndipo tunapopata ufumbuzi wa kuitafsiri maana halisi iliokusudiwa kwenye aya za Qur'an bila kutumia vielelezo vya nje ya Qur'an.

Waislam wengi, hususan wa kuwalaumu ni watasiri wa zamani, ambao wengi hufata kwa kua tu wamejijengea majina makubwa na wengine ni wazeew na wazai wetu ambao tumekuta wakifata mkumbo bila kuhoji wala kuuliza na wengi tunatishana, mpaka lehii, kua "kuuliza hayo utakufuru au 8unakufuru".

Hilo siliafiki, elimu bila kua na ushahidi. kwa mfano unapoulizwa "umetoa wapi kua adam ni mtu wa kwanza kuumbwa" au Hawa umemtoa wapi? unashindqa kujibu au unaana kubabaika. Kinachotakiwa ujibu ukweli wako tu na kama ukiona hakuna ulipolitoa na au ulipolitoa hata wewe mwenyewe unaona haya kusema kweli, elewa kua hilo sio sahihi au hulijui vizuri, unatakiwa uulize (inquisitive) nimesoma hapa JF, kuna Muislam aliwahi kuandika kua "Uislam sio dini ya Misukule" ya kukubali kila unchoambiuwa bilka kuuliza".

Nakubaliana nae mia kwa mia. Ni wajibu wa kila Muislam na asie Muislam kuuliza kila fundisho la Kiislam aneliongelea amelitoa wapi? kwa sababu kuna Waislam waliopotoishwa na wao wanaendelea kupotosha wengine na kuna vikundi vya watu wnaofanya ufisadi wa maandiko kwa makusudi kabis. Kwa hio mnaonisoma wote, mkiwa Waislam na msio Waislam, mpo huru kuuliza chochote, wakati wowote kuhusu yote ninayoyaandika nimeyatoa wapi. Na nikikupa nikupe na ushahidi, kama sina ushahidi hayo yanabaki kua ni angu bonafsi na sio ya Muumba wetu, mwongozo waa Muumba wtu ni Qur'an na Qur'an ipo, kwanini ukosekane ushahidi?

Tunasema elimu ni ujuzi wenye ushahidi (education is evidence-based knowledge). kama uliyatoa uyajuayo kwa wazee wako tu, sema ukweli, kama uliyatoa kwenye vitabu vingine, sema ukweli.

Kosa kubwa linafanyika hivi sasa na watarjama wamengia mkenge, ni kuitafsiri Qur'an kwa kutumia vilivyomo kwenye biblia. Narudia hilo ni kosa kubwa sana, kwa kua Qur'an ni maneno ya Muumba wetu, hayo ni bora kuliko maneno ya binadam au shetani yoyote yule.

...7
8...
Katika tafsil ya aya 26 na 27 nimewapa vifungu muhimu tu, kama utangulizi wa Kisa cha Adam. Lakini aya hizo tunaweza kuzifanyia tafsil ya kina ya neno kwa neno, watu wakapata kuelewa jinsi tunavyofanya tafsil na kutumia mbinu zingine tunazofundoishwa na Qur'an yenyewe kuielewa Qur'an.

Nimeona kila itapobidi tutafanya hivyo lakini post hii tujikumbushe mbinu zinazotumika na zilizopo ndani ya Qur'an ili twende huku tunayo post ya rejea.

Tutaelezea baadhi ya mbinu na maneno tuliyoyapata maana yake nyingine baada ya kutumia mbinu za Qur'an.

1) Tafsil; kwa ufupi ni uchambuzi kwa kufafanua, na kuna sura ya Q 41 Fussilat inatufundisha hilo.

2) Ndimi (lisan) ya Ibrahim (Abrahamic locution), hii nayo tunaipatakila tunapoitaja "Milat Ibrahim".

3) Kiota (nested); Hii ni mbunu na muujiza wa Qur'an kua maneno na mpoaka herufi zake zimeungana na hakuna isiokua na maana yake au iliozidi bila kua na kazi yake.

4) Ardh; Sehemu nyingi kwenye Quran haimaanishi ardhi (earth) bali humaanisha ni maandiko (scripture).

Tutakua tunaijazilia post hii maa kwa mara na tutazielezea kwa kina kila tunavyoendelea. Hapa naonesha tu istilahi (terminologies) za mbinu tunazotumia kupata maana sahihi iliokusudiwa zaaidi ya tarjama za neno kwa neno au tafsiri zilizotumia vitabu vingine kuitafsiri Qur'an.

Tunatumia Qur'an yenyewe kama msingi wa ushahidi (primary source), kikitajwa kitabu cha nje ya Qur'an kama ni hadith au cha lugha, au tafsiri, itakua ni msisitizo wa kukazia tu hoja lakini sio kama ushahidi wa msingi wa hii tafsil tuifanyayo. Usichanganye neno "tafsil" na "tasir" ni maneno mawili tofauti..

Kama hujaelewa kitu uliza au kama una maoni au tunachohitilafiana kilete na ushahidi wako sio mano yako tu, tukijadili.
Simba.
 
Umegusia aya zisizo zidi 10 Mtume alielezea je naweza zifahamu na hayo maelezo ni yap??
Hio ilikua ni kusisitiza tu kua hakuna alipotajwa au kuelezwa Adam kua ni mtu wa kwanza na kusisitiza kua Bwana Mtume Muhammad (SAW) hajafanya tafsiri ya Qur'an.

Tafsiri zimekuja kufanywa miaka zaidi ya 200 toka kuondoka kwa Mtume. Nakushauri soma historia ya tafsiri, utanielewa.
Simba.
 
Kwa kweli mimi ni aina ya wale watu ambao ni wahafidhina, lau hii thread ingeandikwa pale juu kuwa labda "Mnajua kuwa Adam sio wa kwanza kuumbwa duniani?" basi mimi nisingefungua kuusoma huo uzi. Na ndo mana hata dada yetu FaizaFoxy anasema ni thread ilishawahi kuletwa humu na watu wakaipita.

Ila kwa bahti mbaya ama nzuri niseme nikajikuta nimeingia mteo wa Arsis nikasoma habari za Adam (A.S) kupitia uzi wake. Kiukweli kwa sasa hata mie nina 50% kwa sasa, yani nimekaa katikati nasubiria ushahidi zaidi niamua niwe upande upi. Mana kuna aya nyingine hata ukizisoma unaanza kuwaza, pengine hii inamaanisha ni watu before sisi, mfano hii:
{ وَرَبُّكَ ٱلۡغَنِیُّ ذُو ٱلرَّحۡمَةِۚ إِن یَشَأۡ یُذۡهِبۡكُمۡ وَیَسۡتَخۡلِفۡ مِنۢ بَعۡدِكُم مَّا یَشَاۤءُ كَمَاۤ أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّیَّةِ قَوۡمٍ ءَاخَرِینَ } Al-An'aam, aya ya 133
"Na mola wako mlezi ndiye Mkwasi, akitaka atakuondoeni na awaweke wengine awapendao badala yenu, kama alivyokutoeni nyie kutokana na uzazi wa watu wengine"

Kumbe wapo wanachuoni kama Ibn kathir wameelezea maisha before Adam, uwepo wa viumbe kama hinn, rimm, timm, rimm, jann, na wengine wakasema hata Adam ni cheo kinachokuja kila baada ya miaka kadhaa, kiasi cha kutaja Adam wamekuja mara 30 duniani katika span ya miaka 1000.

Kweli elimu ni bahari na kila mtu anazama kwenye kina chake
17_81.gif

Q 17:81. Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke! 81
 
Nimefurahi sana kwa mchango wako mzuri, michango namna hio ndio inatoa elimu kwa wengi wetu kwa tudioyajua.
Nimekuelewa sana unachosema. Nina maswali maafupi sana.

Hayo mafunzo ya "bidaa" umeyaona wapi kwenye huu uzi?

Wewe hio elimu ya kujua hii na hii si "bidaa" umeitolea wapi?

Unafahamu maana ya Qareen?

Mtume wetu alikua nae Qareen au alikua hana?

Qur'an si imeletwa kupitia kwa mtume Muhammad?

Haijaleta kisa cha mtume Suleiman?
Simba.

Ahsante kwa maswali mazuri .. mimi bado Taalib ilmu ni mwanafunzi ..lakini katika uanafunzi wangu .. Bidaa kuijua hainitatizi.. mwanzoni mwa uzi wako ulimention kwamba babu yako anaagua na kwenda kuswali .. wewe mwenyewe ulilala pangoni kupewa mikoba ya uganga hapohapo unaotakidi ni swala tano ... Kwa ufupi mnafanya ushirikina na ibada .. ni kitu ambacho si sahihi kwa mafundisho ya wema waliotangulia....

Kuhusu Qareen hebu nijuze nini maana ya qareen as I told you earlier bado ni talib ilmu nipo tayari kujifunza elimu iliyo sahihi kwa misingi ya Mtume pamoja na maswahaba wake ...

Kuhusu Suleiman, ni kweli yeye alipewa mamlaka kutoka kwa Allah ambayo hakuna yoyote atakaye na aliyepewa baada ya yeye , kuna hadithi sahihi .. mtume aliwahi kupambana na jini na akawaambia maswahaba zake kwamba kama isingelikuwa kiapo ambacho Suleiman aliomba Allah kwamba asitokee mwingine baada yake mwenye uwezo kama wake basi yule Jini angemfunga kwenye kigogo ili watu waje wamshuhudie... Kiigizo chetu sisi ni Mtume na hakutaka kuwatumia wala kuwafuga majini kwanini wewe ufanye hivo?! Unless otherwise wewe ni mshirikina au mchawi au kafiri ..
 
katika hiki kisa cha Adam wanaokisoma wote wakiisoma post, wagonge like au mshangao, au masikitoko, au makasirisho. Nielewe tu kua imesomwa na fulani na fulani, hususan ningependelea Lidafo Etugrul Bey Nourhan FaizaFoxy na wengine wote wakipitie na kukifatilia kisa hiki cha Adam, kina mafunzo mengi sana ndani yake.

Nipo tayari kujibu chochote katika haya niandikayo, hii ni elimu.
Simba.
Naam, nafuatilia unaenda vizuri, bado nasubiri muendelezo wa hizo aya mpaka tufike kwenye baqarah aya ya 30
 
Hio ilikua ni kusisiytiza tu kua hakuna alipotajwa au kuelezwa Adam kua ni mtu wa kwanza na kusisitiza kua Bwana Mtume Muhammad (SAW) hajafanya tafsiri ya Qur'an.

Tafsiri zimekuja kufaywa miaka zaidi ya 200 toka kuondoka kwa Mtume. Nakushauri soma historia ya tafsiri, utanielewa.
Simba.
Hili nakubaliana na wewe, tena naongezea kidogo, tukisoma historia ya tafseer ya zamani zaidi iliyotufikia kimaandiko ni ya ibn Jarir Al Tabari, inayisemekana iliandikwa miaka 200 mpaka 300 baada ya Mtume Muhamnad Sala Allahu alayhi wasalam.
 
Naam, nafuatilia unaenda vizuri, bado nasubiri muendelezo wa hizo aya mpaka tufike kwenye baqarah aya ya 30
In shaa Allah tutafika na zaidi, hii elimu ni ya kina sana, ndio maana naenda nayo taratibu, nikiijaza mistari na nikianza kuchambua kwa kina, basi hata hizo aya 2 nilizoanzia kuzigusia kijuujuu tu ya 27 na 28 ingetubisi tupige zaidi ya kurasa 50 mpaka 60 kuzichambua. Tafsil ni kuchambua neno kwa neno na herufi kwa herufi ya Qur'an.
Simba.
 
Hili nakubaliana na wewe, tena naongezea kidogo, tukisoma historia ya tafseer ya zamani zaidi iliyotufikia kimaandiko ni ya ibn Jarir Al Tabari, inayisemekana iliandikwa miaka 200 mpaka 300 baada ya Mtume Muhamnad Sala Allahu alayhi wasalam.
Kweli, waandishi wengi wamemnukuu Tabari, kama ni ya ukweli ni yeye au ni yao ajuae ni Muumba wetu tu, kwani hakutuahidi kua atazilinda hadeeth na tafaseer nje ya Qur'an yenyewe.

katika hayo kwa kuwa Maulamaa wamejitahidi kivyao, Tuchukue kwao katika yale yanaoendana na Qur'an tu. Yaliozusha (bidaa) ambayo hayamo kwenye Qur'an, mfano wa hili kua adam ni 'mtu wa kwanza kuumbwa' kama wameliongelea na halimo kwenye Quraan, tuyaache.
Simba.
 
Ahsante kwa maswali mazuri .. mimi bado Taalib ilmu ni mwanafunzi ..lakini katika uanafunzi wangu .. Bidaa kuijua hainitatizi.. mwanzoni mwa uzi wako ulimention kwamba babu yako anaagua na kwenda kuswali .. wewe mwenyewe ulilala pangoni kupewa mikoba ya uganga hapohapo unaotakidi ni swala tano ... Kwa ufupi mnafanya ushirikina na ibada .. ni kitu ambacho si sahihi kwa mafundisho ya wema waliotangulia....

Kuhusu Qareen hebu nijuze nini maana ya qareen as I told you earlier bado ni talib ilmu nipo tayari kujifunza elimu iliyo sahihi kwa misingi ya Mtume pamoja na maswahaba wake ...

Kuhusu Suleiman, ni kweli yeye alipewa mamlaka kutoka kwa Allah ambayo hakuna yoyote atakaye na aliyepewa baada ya yeye , kuna hadithi sahihi .. mtume aliwahi kupambana na jini na akawaambia maswahaba zake kwamba kama isingelikuwa kiapo ambacho Suleiman aliomba Allah kwamba asitokee mwingine baada yake mwenye uwezo kama wake basi yule Jini angemfunga kwenye kigogo ili watu waje wamshuhudie... Kiigizo chetu sisi ni Mtume na hakutaka kuwatumia wala kuwafuga majini kwanini wewe ufanye hivo?! Unless otherwise wewe ni mshirikina au mchawi au kafiri ..
Naomba jibu maswali niliokuuliza ili twende kielimi, ili kitu unachokijua tukijue kwa elimu yako sio kwa maneno yako. Elimu ni ufahamu wenye ushahidi.

Nimefurahi sana kukusikia ukisema wewe ni "Talib ilm" kwa wingi wetu na lisan za sasa? Tunakua Taliban, au sio?

Maswali niliokuuliza myepesi sana. Au hujayajua niyarudie kiwepesi zaidi?
Simba.
 
Back
Top Bottom