Kisa cha Adam 2.5
Nimepitia maoni, nimeona
Lidafo kataka kisa cha Adam nikilete kwa wingi na
FaizaFoxy anasema niende kwa kina zaidi.
Nitajitahidi kufanya yote hayo. Mnistahamilie tu.
Natumai mpaka sasa sasa tunaelewa kiasi jinsi Qur’an inavyotupa (bayyina) yaani mbinu kadhaa za kujibainisha yenyewe (Mubyin). Nasisitiza sana tuifahamu mbinu ya “tafsil”. Tukiielewa na tukiitumia mbinu hii ya kuchambuwa Qur’an, tutaona raha sana tukiisoma Qur’an kwa nia ya kuielewa. Aidha aya moja moja, neno moja moja moja au hata herufi moja moja, kuijuwa tafsili itatusaidia sana kuifahamu Qur’an kila tutapoisoma na itatufungulia muono mpana sana kupita maelezo.
Faida nyingine kubwa ya kufanya tafsil, ni kwa sisi amabao tumesoma sekula kwa maandishi ya kilatini, iwe Kiswahili au Kingereza. Haya maansishi yetu ya shule yana koma, vituo, mabano, nukuu na kashalika. Ndani ya Qur’an yote hayo yapo na zaidi lakini kwa kutumia mbinu ya tafsil tutayapata kiurahisi kabisa.
Mbinu za kuijua Qur’an ni lazima tuzifanyie kazi, haziji tu hivi hivi, lakini amini nimwaambie, kila unapoisoma Qur’an kwa nia Fulani unayapata majibu kiajabu kabisa mpaka tutajishangaa.
Humu kila tunavyoendelea tutaitumia sana njia ya tafsil na tutajitahidi kuielezea kila tunavyoendelea, Pamoja na mbinu zingine. In shaa Allah tutaziweka zote kwenye ukurasa wetu wa fahairisi ili iwe rahisi kuzirejea. Na kama mmoja wetu ataona kitu ambacho kinafaa tukiweke kwenye fahirisi basi anijulishe nami nitakiweka.
Niligusia kidogo hapo juu kuwa wanaoongelewa hapo ni bani israil. Na nikagusia kionjo kimoja cha Qur’an, kua Qur’an katika ayah io hio moja moja au katika aya kadhaa zinazofatana inaweza kuongelea kikundi cha watu (third party) halafu hapo hapo ikaanza kuongelea moja kwa moja kama inaongea na mmoja wao ana kwa ana. Kama ilibyo aya za 26 na 27 mpaka kufikia kuongea moja kwa moja kwenye aya ya 28.
Kitu kama hicho pia kipo katika sura ya Abbasa. In shaa Allah Tutakileta siku za usoni tutajionea, au tunaweza kukipitia pitia tukajionea kwa tafsiri zilizopo. Kama tutaligundua hilo tujulishane. Hio ni homework kwa sote.
Tuendelee na aya 29 kwa ufafanuzi wetu.
Q 2:29
| Yeye ndiye aliye kuumbieni kwa ajili yenu, (Baudha) yote yaliyomo katika Maandiko (ardh), | هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ لَكُم مَّا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًۭا ٢٩ |
| “thumma” (Baada ya muda kupita) akawizani (balance) katika utambuzi (Alsamaa). | ثُمَّ ٱسْتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ |
| akafanya tabaka saba za uelewa (sabaa samaawat) na yeye ndie mfundishaji wa kila kitu. | فَسَوَّىٰهُنَّ سَبْعَ سَمَـٰوَٰتٍۢ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌۭ ٢٩ |
Ufafanuzi wa Aya ya 29 ya Sūrah (2) Al-Baqara
Mwanzo wa aya hiyo kama nilivyoichambua hapo juu, inaanza kwa kuwajulisha “baiudha”, kuwa yeye ndiye aliyewaumbia yote yaliyomo katika maandiko (ardh), mnakumbuka mwanzoni huko tulielezea kua “ardh” pia inamaanisha maandiko na sio lazima iwe ni hii ardhi yetu tuliyozowea kuifikiria kila tunaposikia neno “ardh”. Hapo mtaona kua katika kipande hicho cha awali halikutajwa kabisa neo “samaawat) likaja kutajwa Baadae. Lakini baada ya neno “ardh” tu likaja neno “thumma”, hili linaonesha wazi kua muda ulipita.
Ikaja “stawaa (ku-balance) katika utambuzi “ala samaa”.
Tunajifunza nini katikja aya hiyo? Muujiza wa Qur’an.
Hapo inaonesha wazi kua makundi waliyopata kitabu kabla ya Qur’an, yalikuwamo humo mafundoisho na uelewa uliohitajika. Lakini Baadae, ilipokuja Qur’an ndio tukapewa maandiko ambayo ni Qur’an yenyewe na tukapewa tabaka (samaawat) za uelewa, tumepewa tabaka saba, ili tukifata anri ya Muumba wetu ya “soma” )ikraa) kila trunaposoma basi yeye mwenyewe ndie mwenye kutuongezea elimu kwa kutupandisha tabaka za uelewa (samaawaat). Huu ni muujiza amabo tunauishi kila siku. Tunayasikia kila sikuwatu wanasema “Qur’an ukiiacha na yenyewe inakuacha”, jali kadhalika kila unapoisoma Qur’an kwa kutaka kuielewa basoi mwenyewe mwenye Qur’an yake anakufungulia milango ya uelewa kiajabu kabisa. Kuielezea hii ni ngumu sana. Na utakapoisom kwa kuisoma tu, basi uelewa wako utabaki kwenye tabaka hio ya kuisoma tu.
Namaanisha kila unapoi[pigia mbizi Qur’an kutafuta chaza wenye oulu, basi mwenye lulu zakje hakunyimi hata kidogo. Na hilo linathibitika hapo kwenye maneno ya mwisho, kua yeye ndiye “Alim” wa kila kitu. Naamini spote tunafahamu kua kazi ya Alim ni kufundisha.
In shaa Allah rukirudi tutakuja kipande kinachosubiriwa kwa hamu kubwa. Mniwoie radhi, imebidi tuanzie huko ili tupate uelewa, In shaa Allah tumeupata japo kwa uchache wake. Nasema kwa uchache wake kwa sababu uchambuzi (tafasil) wa hizi aya ni mrefu sana na ningesema niulete wote basi naamini mpaka leo tungekua bado hatujaimaliza aya ya 26 tu na tungejaza zaidi ya kurasa 100.
Kwa hayo, nakaribisha maswali, ushauri, kukosolewa na chochote kinachuhusiana na elimu hii.
Itaendelea.
Kisa cha adam 2.6
Je,
Je, Malaika walimuuliza Allah?
Dibaji (prelude) ya kisa cha adam. Aya ya 30 ya Sūrah (2) Al-Baqara
Kwanza kabisa naomba niweke angalizo;
Natumai umegundua kuwa nimeweka “adam” kwa "a" ndogo. Tutaelewa mbele huko kwanini tumefanya hivyo.
Ufafanuzi wetu wa ayah hii, kwa wengine wetu, utatushangaza. Utatufikisha katika ukomo wetu wa jinsi tunavyoijua na kutupeleka mbele zaikdi au kwa jinsi tunavyoelewa kutokana na watafsiri wengine mbali mbali tuliokwisha wahi kuwasoma au tunavyosomesha au kuwasoma Masheikh na Maulamaa wetu walipoielezea. Licha ya hayo, hagtuna budi tujikite na kuusoma ufafanuzi wa ayah ii wa wazu tuliouweka chini hapa.
Naamini tutaelewa na tutajionea wenyewe jinsi “software” yetu ya ajabu, Qur’an, inavyotuongezea uelewa wetu (samaawat).
Tujikumbushe na tujionee wenyewe kuwa yote haya sio ya kutoka vichwani mwetu, bali ni ni zao la kutumia mbinu za Qur’an yenyewe inavyotufundisha kila tunavyoendelea.
Nimeona tuiweke hio aya kamili kama ilivyo kwa Kiarabu, kisha kwa kutumia mbinu za Qur’an yenyewe, In shaa Allah tujaaliwe kuifafanua kila kipande kwa ufasaha na tujaaliwe kulielewa ayah ii kila tunapoisoma. Ina mambo mengi sana ya faida kwenye uelewa wetu.
Aya Q 2:30
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّى جَاعِلٌۭ فِى ٱلْأَرْضِ خَلِيفَةًۭ ۖ قَالُوٓا۟ أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّىٓ أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ٣٠
Tunaanza kui “fasil” na kuielezea kwa vipoande vipande (tafsil);
| Na Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika (katika vitabu vya kabla), Mimi daima Najaalia ( جَاعِلٌۭ) “Khalifa” (خَلِيفَةًۭ ۖ)(mrithi /msimamizi) katika maandiko / vitabu (ٱلْأَرْضِ). | وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّى جَاعِلٌۭ فِى ٱلْأَرْضِ خَلِيفَةًۭ ۖ |
Na Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika (katika vitabu vya kabla), mimi daima Najaalia “Khalifa” warithi /wasimamizi katika maandiko / vitabu.
Licha ya “Khalifa” Kwenye kipande hiki cha kwanza kuna dhana (concepts) nyingi ambazo tunahitaji kuzifanyia uchambuzi (tafsil) kuupata uhakika zaidi.
Tuanze na kipande cha mwanzo kabisa cha aya ya 30 chenye neno “Jaailoun”, tumelikooza (highlight) kwa rangi ya njano,
“
جَاعِلٌۭ“ hili ni ni jina (nomino) sio kitenzi (verb) bali ni (Ism fail (Kiarabu) jina shirikishi amilifu (active participle noun). Natumai tunakumbuka kwenye vipande vilivyopita tulipitia “sarf” na “Masdar” kijuujuu. Kama kuna tuliosahau, tukirudi nyuma kidogo tutajikumbusha, sio mtihani huu ni kuelimishana tu.
Kwa wale waliopitia masomo ya lugha ya Kiarabu wanaelewa kutofautisha baina ya utenzi (verb), nomino (noun) au nomino shirikishi wakiyasoma tu.
In shaa Allah leo hata ambao hatujapitia Kiarabu kwa kina tutaelewa maana yake nini. Kwani Kiswahili chetu kina maneno mengi sana ya Kiarabu.
Natumai hakuna asiyeelewa neno Majaaliwa, ambalo kwa “sudfa” (coincidence) ni jina pia la Waziri Mkuu wetu, Kassim Majaliwa.
Maneno, majaaliwa, kujaalia, kujaaliwa, tujaalie na kadhalika, yalipotokea hayo yote ni kwenye “Jaala”. Naamini sote tunalielewa neno hilo na mpaka hapo tumeshaanza kuelewa ni kwanini tunaposema “Jaailoun” ni jina tunalipata kutokea wapi. Kwa ufupi ni nii sarf (ism fail) ya Jaala.
Kiarabu chepesi sana kwa sisi watumiaji wa Kiswahili, ugumu wake unakuja kwa kutishana tu. Tunachohitaji ni mazoezi tu ya matamshi ili tuwe mabingwa wa Kiarabu.
“Jaailoun” ni Allah mwenyewe. Yeye ndiye mwenye kujaalia yote. Allah daima amejaalia warithi na wasimamizi (Khalifa) wa vitabu na maandiko yake, kama alivyosema mwenyewe “Inni Jaalilon fil ardh (vitabu) Khalifa” (warithi / wasimamizi).
Hizo ndio maana za “Jaailoun” na “Khalifa”.
Kwa hayo, hiki, cha u-Khalifa sio kitu ambacho kimeishia kwenye mapokeo ya kwanza ya Maandiko. Pia sio kitu ambacho kinaishia na maandiko ya mwisho, Qur’an”.
Qur'an Tukufu imeteremshwa na Allah. Na Allah (SWT) daima hujaalia wale watu ambao wanaendelea kuchukua nafasi ya kuwa warithi na wasimamizi wa maandiko“Al Ardh”. Hii ni muhimu sana, kwa sababu mimi nazungumza na wewe kwa sasa. Na nina matumaini kuwa Wewe na mimi ni sehemu ya warithi/wasimamizi (MaKhalifa) wa sasa wa Kitabu “Qur’an”. In shaa Allah tuwe miongoni mwa wale Waliojaaliwa (Jaailoun) na Allah kuwa MaKhalifa.
Tujaaliwe kurithi, kukisimamia na daima kudumisha ufahamu wa kweli wa uelewa wa Qur'an. Insha Allah, sote tunaoyapitia haya hapa, kwa nia njema kabisa, tutakuwa pamoja katika jukumu hili, tutachukua na kulibeba jukumu hili kwa hiari zetu.
Hizo “jaailoun na Khalifa” ni kauli za mwanzo za kwenye hii aya. Hayo ni baadhi tu ya mambo mengi sana ambayo tutayagundua katika ayah hii, na itabidi tuyafanyie uchambuzi ((tafsil) ili tupate uelewa sahihi na wenye maana zaidi (meaningful).
.Mpaka hapo hatujajionea kuwa hakuna uhusiano wowote wa uumbaji wa mtu yeyote wa kwanza kwenye kipande hicho. Tumeona kuwa Allah (s.w.t.) anawaambia Malaika juu ya maandiko au Kitabu (Al-Ardh). Kwa hiyo, hili la maandiko (Ardh) ni jambo ambalo Mwenyezi Mungu amelitangaza kwa mara ya kwanza alipofunua maandiko (revelation) ya mwanzo kabisa.
Jambo muhimu ambalo tunapaswa kulielewa ni kuwa, neno “Khalifah” linatumika sehemu nyingi mbalimbali ndani ya Qur'an.
“Ikhtilaaf” yaani watu ambao wao kwa wao hawakubaliani (khitilafiana),
Khalifah au Khilfa au Khalafun na kadhalika, maneno yote haya yanamaanisha mabadiliko (alteration), ambayo kikundi baada ya kikundi baada ya kikundi hubadilika. Hili linafahamika sana na mabingwa wote wa lugha ya Kiarabu, haimaanishi kuwa ni makamu (viceroy) wala mfalme au mtawala wa vitu vya asili kama wanyama au mimea.
Allah (s.w.t.) anatueleza kama tulivyofafanua kua hayo ni maandiko (ardh). Na mpaka sasa hata maandiko haya ya Qur’an Allah ametueleza tangu mwanzo, kwamba ujumbe huu utakua na watu wenye kujali, wenye kustahili na wenye uwezo wa kutosha kuyabeba na kuyatunza maandiko haya, licha ya kupigwa vita kutokea kila upande, mwenyewe hujaalia Khalifa (makhalifa) apendavyo.
Na hata katika maandiko na vitabu vilivyotangulia na kupotea kulikua na makhalifa ambao sasa Allah anawaelezea kwenye Qur’an. Kama tunavyoona haya yapo mwanzo mwanzo mwa Suratul Baqara ya kwenye Qur’an. Allah anatufikishia mwongozo kuwa hata wewe au mimi tunaweza kuwa katika hao Makhalifa. Tuendelee.
Allah (s.w.t.) anawaelezea Malaika, wala hazungumzi nao, Allah kuongea na Malaika ni kuwapa amri tu na wao wanatii. Tunayaona hayo hata kwa viongozi wa nchi tu, tunaambiwa “Rais leo anaongea na wanajeshi wake” Lakini tukitazama na kusikiliza tunaona anayeongea ni Rais tu, wanajeshi wake wanasikiliza na kutii tu. hakuna maongezi, wanajeshi ni kupewa amri na kupokea kwenda kutimiza tu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hutoa malekezo na Amri. Mwenyezi Mungu hazungumzi wala hazungumzii kuwa anzungumza na Malaika.
Allah (s.w.t.) Yeye ni Muumba wa kila kitu, hana haja ya kushauriana na Malaika au mtu yeyote au kutoa mapema taarifa, kutuma telegram kuwa anataka kufanya hivi au vile.
Allah (s.w.t.) anatujulisha kwenye aya hiyo kuwa katika maandiko / Kitabu cha kwanza aliwaambia Malaika ambao hubeba ujumbe, maandiko hayo kuyawasilisha kwa watu. Allah (s.w.t.) daima huamrisha Malaika kwenda kuufiksha ujumbe kwa wasimamizi (Khalifa) wa maandiko / kitabu (ardh). Hayo ndiyo sehemu ya aya hiyo inatujulisha.
Pia sehemu ya aya hio inatujulisha...
... Itaendelea.