Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Usemayo ni sahihi kabisa lkn pamoja na kwamba neno ardhi latumika kama maandiko lkn kwa namna fulani inategemea na ujumbe ulio kusudiwa katika aya fulani,lkn kwa muktadha wa hiyo aya ambayo inaelezewa hapana shaka kusudio la maana hapo ni ardhi kama ardhi

Vile vile ukija mwanzo wa hiyo haya ambapo Allah anaeleza au kumtaja mbu, Allah anasema yeye haoni haya kutoa mfano mdogo hata wa mbu,na akasema kwa mfano huo huwaongoza wengi na kuwapoteza wengi,ukiangalia huo mfano wa mbu ni dhahiri azungumziwaye ni mbu halisi,na si kikundi cha ban israel

Ngoja tuendelee kusoma
 
'ujumbe aliyokusudiwa'...

Hili ni tata kulibaini ukweli wake, kwa kuwa watu wenye upeo na daraja tofauti tofauti la usentienti, konsayansi na nuru ya ufahamu hujinasibu na 'Ujumbe Tofuati' kwa kile kile kinachoweza kuwasilishwa wazi--na kuwa wazi kwa wote; japo hakuna utofauti khasa ya 'ujumbe' bali mtanuko wa dhana na vina vya tafsiri--vyenye nasibu ya koherensia ya ufikirifu.

Katika hali ya kawaida: Kimfaacho mtu, ni chake...

Kuna namna fulani, waalimwengu wa dunia hawajajijenga ili kufahamu/maizi ukweli wa kwamba lugha ni alama za nasibu; nasibu inaweza kuwa na zaidi ya ngozi moja ya 'vina vya tafsiri'.

Mambo ya kuwa na zaidi ya ngozi moja ya vina vya tafsiri ndicho ambacho tunaweza kutaja kama 'topografu ya Uono'; vivyo hivyo, mikondo sambamba ya nasibu ya michepuko ya vina vya tafsiri ndiyo tunaweza kusema ni 'Topolojia ya ufikirifu'.

Kinachokadirisha Uono ndiyo jambo tunaloweza kulitaja kama isitilahi 'Muktadha Akilifu'--kwa wanaozungumza kiingereza hili wangalitaja kama 'Intelligible Context'...

Haya ndiyo msingi wa 'Uono na Ufikirifu Mifumo'... Na tena huu ni muhimu sana kwa walimwengu wote kujizoesha nao; pasipo huu waalimwengu wataishia kuwa na ufikirifu wa juu juu wa mambo na tena kwa mazoea hafifu na duni; ujuzi wa vitu kama vile mashairi, ngonjera na tamathali za semi huwa na nasibu ya 'vionjo vyenye utamu zaidi' wa kifahamu kwa kuwa haya ndiyo huwapa waalimwengu ladha ya 'Mawezekano Zaidi ya Kiutambuzi' kuliko 'utambuzi wa juu juu wa mambo'...

SASA, mambo ya 'ardhi na Mbingu', kwa mfano, yanaweza kusadifiwa katika maudhui fulani na kumbe yakabeba mikondo sambamba ya maudhui ya kitopolojia; hili linahitaji ujuzi na ufundi sahihi wa kuwabangulia wafikiwa wa hayo maudhui kweli zilizositirika za kimaudhui.

Mara nyingine jambo/mambo kama haya ndiyo huwa ni msingi wa shughuli ya kuwatenganisha watu ambao wako tayari 'kuya-JUA ya kina'; na kuwa na subira na wengine ambao bado hawako tayari kuwa na 'Uono na Ufikirifu Mifumo' kwa mfano.

Utamu wa Mawaidha yoyote ni sanaa na utundu wa kucheza na topografu na topolojia ya ufikirifu--kwa mashauri yenye 'mbegu za u-JUA-ji'.

Kwa hivyo, ardhi na mbingu inaweza kuwa ni mapana ya usentienti, konsayansi na nuru ya ufahamu; kwa hivyo hata mtu asiye na 'mwili' pia yuko kwenye mapana ya topografu na topolojia za 'ardhi na mbingu'--kwa mapokeo ya Ukristo, kwa mfano, maandiko ni kisawe cha 'Neno'; na neno ni dhahiri ya miili ambavyo pia kuna 'Neno' kwa dhahiri ya 'Uzima wa Miele'; haya mawili ndiyo yanaweza kutengeza mashina na matawi ya maarifa ya 'Mbingu na Nchi'...

Maandiko ni mambo ya kumbukumbu ya miili na uzima wake, ikiwa mtu anajinasibu na Uono na Ufikirifu Mifumo. Kwa hivyo hata mambo ya 'Kila mtu kaandikiwa Riziki yake' ni muendelezo wa shauri lile la nasibu ya kheri ya 'Uzima wa Miili'...

Sasa haya mambo yana 'Rizayati yake'; kiasi kwamba haijalishi mtu atasema kapata maarifa kutoka kwenye kitabu kipi--kama anajua khasa ukweli wa mambo kuna 'lugha ya alama na ishara' huleta hesabu ya 'Uono na Ufikirifu Mifumo'... Ulimwengu wote mzima ni Neno Linaloishi !

Ardhi na Mbingu ni mambo ya ushahibiano wa 'Maarifa na Maarifu' ya ukweli khasa wa mambo... Kwa hivyo kwa mfano, kwa Kiswahili neno 'Samawati' ni rangi ya 'Anga'... Kwa hivyo usijekushangaa shauri la 'Samawati' laja kuwa pia ni 'Mbingu'... Mambo UONO na tena 'Muktadha Akilifu' yana 'mizania' ya vina vya tafsiri na visawe vyake kwa lugha za alama na ishara.

Unaweza kufanya mazoezi ya kusoma katikati ya mistari katika haya kwa mfano:​
Hmmmm​
 
Ardh kwa Kiarabu ni maandiko au vitabu (scriptures) pia. Tulifafanua hili hapo nyuma kidogo. Hiyo ardhi" uisemayo kwako muongeaji wa Kiswahili inakua ni mara moja uelewa wako ( "arsh" yako) kukupekeka kwenye hii ardhi tuliyozowea kuisikia kwa Kiswahili. Hapo ni kama nilivyotafsiri, ushahidi wa ziada;

Ukitazama aya ya 27 katika tafsiri ya Barwani utakuta neno hilo hilo kalitafsiri kama "nchi" aya mbili baadae, hapo unapopapaongelea, kabadili tafsiri na kuliita neno hilo kua ardhi. Nchi inajulikana, ina maneno kadhaa trofauti kwa Kiarabu, haiwezekani "ardh" kua ni nchi kwa muktadha wa aya hizo.

Sisi sio wa kwanza kutumia neno ,maandiko au vitabu, LUkitazama tafsiri nyingine ya Kiswahili ya Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr na Sheikh Nasir Khamis utakuta wametumia neno "vitabu".

Ukisoma vizuri kuanzia aya ya 26 kwa jinsi tulivyofafanua utaona kua neno sahihi na linaloleta maana zaidi ni "maandiko au vitabu". Kwani hapo hauongelewi uumbaji, inaongelewa ahadi (iliovunjwa).

Natumai umeelewa na In shaa Allah unaweza kuzipata tafsiri zote hizo hapa:The Noble Quran - Quran.com ukajisomea zaidi mwenyewe. Ingawa zote mbili binafsi napitia kujisomea na kulinganisha kisomi lakini ufafanuzi wetu hauzitegemeai hizo kua ndio chanzo cheu cha msingi (npt our primary source). Utajionea kwanini, mbele kidogo. Tunapoifanyia 'tafsil" aya ya 30.

Sio tabaka za elimu, tabaka za uelewa "samaawat" zinapelekea kuikuza (arsh yetu).

Hatujakosea.
 
hii kweli arsis kaitabaruku elimu hii kwa muda wa miaka elfu 5000. form 4 leaver haiwezekan uwe hivi. mzee kweli alsis alikaa kukufundisha au mlikua na darsa ya tafsil.?
AlhamduliLlah naendelea kujifunza kutoke kwake. Mambo ninayojifundisha ni mengi sana tena sana, na sasa nimeona hii elimu kwanini nife nayo, nami niigawe kama ninavyopewa mimi.

Ni form IV kweli, lakini ukinisoma vizuri utaona kua elimu haitegemei darasani pekee, inategemea na Muumba wetu kukufungulia uelewa wako ukionesha juhudi zako.

Kwa nia njema kabisa, tukimuomba Muumba wetu atuzidishie elimu, basi itatujia hio elimu kwa njia ambazo hatukuzitegemea wala kuzifikiria.
Simba.
 
Kama ni ndoto ya kweli itajirudia rudia. Kumbuka ndoto ni somo la Nafs, tutaligusia kidogo huko mbeleni.

Muombee dua ndugu yako, toa na sadaka kwa nia ya kumtolea yeye sadaka yake.
Simba
 
Nataka kujua kwanza,anayechambua hapa ni wewe simba au arsis?
Hilo tulishalitolea maamuzi na ufafanuzi nyuma nyuma huko. Haijalishi ni nani, wewe unachotakiwa kujibu au kuleta hoja tu.
Mwaga elimu.
Simba.
 
Kwasababu aya inasema "yeye ndiye aliyewaumbia yote katika ardhi" iweje yawe hayo ni maandiko?
Lugha ya Kiarabu na ndimi (lisan) hiyo ndiyo kaichaguwa mwenyewe Muumba wetu kufikishia mwongozo wake. Ni aya ya Qur'an yenye hayo, siyo yetu sisi.

Wengi sana, hususan, wanaoongea Kiswahili wanachukulia neno ardh kuwa ni ardhi hii tunayoitenbelea juu yake tu. ++Sasa umeielewa maana nyingine ya neno "ardh", kila unapokutana nalo pasome kua ni maandiko (scripture) ujionee tofuti ya uelewa.

Nadhani nilishalijibu hili swali na majibu yangu aya hayabadilishi maana bali yanakazia tu jibu langu la awali.
Simba.
 
Nataka k

Naona kuna kitu hakipo sawa hapa

Uzuri wa elimu za Kiislam ni kuwa upo wazi na haujawahi kufichwa na sio elimu kipofu au bubu. Maandiko (ardh) ya Qur'an ipo wazi na yanapatikana popote, wakati wowote.

Samaawat ni tabaka za uelewa wetu, mebele huko tutajiponea kua zipo tabaka saba na Mtume Muhammad (sAW) kajaaliwa zote saba kwa kazi zake alizopewa za Nabii na Rasul.

Haoo tunaoata somo lingine, je, tunafahamu tofauti ya Nabii na Rasul? Je, kuna Nabii ambae sio Rasul?

Waislam tunatakiwa tujiulize na kuuliza maswali kila tunapokiona kitu hatukielewi. Sio kukiwacha tu na kusema "naona kuna kitu hakipo sawa hapa".

Kama unaona hakipo sawa, inamaanisha unacho unachokiona "kipo sawa". Badala kubishana, tukhitilafiane na utupe elimu ya kile unachokoiona wewe kipo sawa. In shaa Allah uelewa (samaawat) zetu kiyapokee yote na kukiweka kwenye "arsh "zetu kile kilicho sahihi tu.

YTusiache vitu vinaning'inia (hanging) kwenye elimu hii ya Qur'an ilio bora kuliko elimu zote.
Simba.
 
mkuu Arsis mimi naona kisa cha adam ni bora ungeuanzishia uzi wake tu ujitegemee sababu kisa cha adamu kina mambo mengi complex yanachanganya na jinsi ulivyoanza mbali sijui mambo ya tafsili mara lisan na tafsiri za mashkhe haya yanafaa ukiwa umesoma japo vitabu vya dini ndio utaunga doti..ushauri wangu yafungulie uzi mpya uite"UKweli Kuhusu Adam-je, ni binadamu wa kwanza kuumbwa?" maana tulianza vizuri sana kuhusu ww kufunguliwa macho tukaja visa na vionjo vya Arsis ilikuwa moto sana ila hili darasa la lisan na tafsiri na maandiko ya mashekhe inachosha tena inaboa maana inahitaji uwe na akili pana na kisomi ya kuchanganua vitu hiyo wanayo wachache humu hadi lengo la uzi mama wa visa na vionjo vya arisis linapotea fanya kusitisha hili darasa la adam lipe uzi wake linaonekana refu sana kisha turudi tuendelee kwenye Visa na vionjo vya Arsis..
Kumbuka lengo ni kutoa elimu basi ni bora uwe na nyuzi nyingi tofauti zinazojitegemea zenye elimu tofauti kwa ajili ya marejeo kuliko hii ya kutumia nyuzi moja kurundika mambo kibao yenye maudhui tofauti yasiyohusiana na yaliyotangulia haileti maana zaidi ya kuchoshana.
 
Nimekuelewa, wazo lako zuri. akini kisa cha adam sifungulii kwa sasa uzi mpya. Tukimaliza sehemu inayohusiana na majini na shetani kwenye kisa cha adam labda ndio tutakifungulia uzi mpya.

Lengo ni wale ambao hawajapitia huo usomi uusemao na wao waupitie hapa, wale waliopitia usomi mwengine na wao waongezee tabaka zao za uelewa.

AlhamduliLlahi, macho hayakufunguliwa kuyajua majini ni nini tu, macho yamefunguliwa mpaka wenye Qur'an na mengine mengi sana tena sana.
Simba.
 
Kama ni ndoto ya kweli itajirudia rudia. Kumbuka ndoto ni somo la Nafs, tutaligusia kidogo huko mbeleni.

Muombee dua ndugu yako, toa na sadaka kwa nia ya kumtolea yeye sadaka yake.
Simba
Mkuu,simba Nina swali la ndoto inanirudia rudia toka mwalka 2017,huwa nimepata ota ndoto kwamba nipo jukwaa moja na Hayati Rais mwinyi (kabla hajafariki)...Nikaja ota nipo na Hayati Ben mkapa jukwaan (kabla ajafa) Nilipata Ota nipo natembea na Rais wa Rwanda Kagame,,,Paul makonda (alkiwa mkuu wa mkoa wa Dar) nilipata Ota nipo na magufuli ( kabla hajafariki) tunatembea kwenye julkwaa,,,mwalka Jana niliota Mara mbili nipo na raisi Mama Samia,,,mwaka huu nimepata ota nipo ofcn na Rais wa marekani Joe Biden ,Kisha nikaota nipo na Trump(aliyewah kuwa Rais wa Us) pia juz tar 26/9 nimepata Ota nipo na Rais wa Russian (Putin) Mm si mwanasiasa,sijawahi kuwa hata mjumbe au monitor wa darasa,si baloz bali ni raia wa lkawaida,,Sasa naomba nisaidie nijue hiz ndoto Zina mema au ni Ubongo tuu unajidanganya wenyewe? Pia niliwah Kluota nipo na kikkwete tunasalimiana.Naomba ufafanuz kwa hili.
 
Kisa cha adam 2.6

Je, Je, Malaika walimuuliza Allah?

Dibaji (prelude) ya kisa cha adam. Aya ya 30 ya Sūrah (2) Al-Baqara



Kwanza kabisa naomba niweke angalizo;

Natumai umegundua kuwa nimeweka “adam” kwa "a" ndogo. Tutaelewa mbele huko kwanini tumefanya hivyo.

Ufafanuzi wetu wa ayah hii, kwa wengine wetu, utatushangaza. Utatufikisha katika ukomo wetu wa jinsi tunavyoijua na kutupeleka mbele zaikdi au kwa jinsi tunavyoelewa kutokana na watafsiri wengine mbali mbali tuliokwisha wahi kuwasoma au tunavyosomesha au kuwasoma Masheikh na Maulamaa wetu walipoielezea. Licha ya hayo, hagtuna budi tujikite na kuusoma ufafanuzi wa ayah ii wa wazu tuliouweka chini hapa.

Naamini tutaelewa na tutajionea wenyewe jinsi “software” yetu ya ajabu, Qur’an, inavyotuongezea uelewa wetu (samaawat).

Tujikumbushe na tujionee wenyewe kuwa yote haya sio ya kutoka vichwani mwetu, bali ni ni zao la kutumia mbinu za Qur’an yenyewe inavyotufundisha kila tunavyoendelea.

Nimeona tuiweke hio aya kamili kama ilivyo kwa Kiarabu, kisha kwa kutumia mbinu za Qur’an yenyewe, In shaa Allah tujaaliwe kuifafanua kila kipande kwa ufasaha na tujaaliwe kulielewa ayah ii kila tunapoisoma. Ina mambo mengi sana ya faida kwenye uelewa wetu.

Aya Q 2:30
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّى جَاعِلٌۭ فِى ٱلْأَرْضِ خَلِيفَةًۭ ۖ قَالُوٓا۟ أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّىٓ أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ٣٠


Tunaanza kui “fasil” na kuielezea kwa vipoande vipande (tafsil);

Na Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika (katika vitabu vya kabla), Mimi daima Najaalia ( جَاعِلٌۭ) “Khalifa” (خَلِيفَةًۭ ۖ)(mrithi /msimamizi) katika maandiko / vitabu (ٱلْأَرْضِ). وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّى جَاعِلٌۭ فِى ٱلْأَرْضِ خَلِيفَةًۭ ۖ

Na Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika (katika vitabu vya kabla), mimi daima Najaalia “Khalifa” warithi /wasimamizi katika maandiko / vitabu.

Licha ya “Khalifa” Kwenye kipande hiki cha kwanza kuna dhana (concepts) nyingi ambazo tunahitaji kuzifanyia uchambuzi (tafsil) kuupata uhakika zaidi.

Tuanze na kipande cha mwanzo kabisa cha aya ya 30 chenye neno “Jaailoun”, tumelikooza (highlight) kwa rangi ya njano,

جَاعِلٌۭ“ hili ni ni jina (nomino) sio kitenzi (verb) bali ni (Ism fail (Kiarabu) jina shirikishi amilifu (active participle noun). Natumai tunakumbuka kwenye vipande vilivyopita tulipitia “sarf” na “Masdar” kijuujuu. Kama kuna tuliosahau, tukirudi nyuma kidogo tutajikumbusha, sio mtihani huu ni kuelimishana tu.

Kwa wale waliopitia masomo ya lugha ya Kiarabu wanaelewa kutofautisha baina ya utenzi (verb), nomino (noun) au nomino shirikishi wakiyasoma tu.

In shaa Allah leo hata ambao hatujapitia Kiarabu kwa kina tutaelewa maana yake nini. Kwani Kiswahili chetu kina maneno mengi sana ya Kiarabu.

Natumai hakuna asiyeelewa neno Majaaliwa, ambalo kwa “sudfa” (coincidence) ni jina pia la Waziri Mkuu wetu, Kassim Majaliwa.

Maneno, majaaliwa, kujaalia, kujaaliwa, tujaalie na kadhalika, yalipotokea hayo yote ni kwenye “Jaala”. Naamini sote tunalielewa neno hilo na mpaka hapo tumeshaanza kuelewa ni kwanini tunaposema “Jaailoun” ni jina tunalipata kutokea wapi. Kwa ufupi ni nii sarf (ism fail) ya Jaala.

Kiarabu chepesi sana kwa sisi watumiaji wa Kiswahili, ugumu wake unakuja kwa kutishana tu. Tunachohitaji ni mazoezi tu ya matamshi ili tuwe mabingwa wa Kiarabu.

“Jaailoun” ni Allah mwenyewe. Yeye ndiye mwenye kujaalia yote. Allah daima amejaalia warithi na wasimamizi (Khalifa) wa vitabu na maandiko yake, kama alivyosema mwenyewe “Inni Jaalilon fil ardh (vitabu) Khalifa” (warithi / wasimamizi).

Hizo ndio maana za “Jaailoun” na “Khalifa”.

Kwa hayo, hiki, cha u-Khalifa sio kitu ambacho kimeishia kwenye mapokeo ya kwanza ya Maandiko. Pia sio kitu ambacho kinaishia na maandiko ya mwisho, Qur’an”.

Qur'an Tukufu imeteremshwa na Allah. Na Allah (SWT) daima hujaalia wale watu ambao wanaendelea kuchukua nafasi ya kuwa warithi na wasimamizi wa maandiko“Al Ardh”. Hii ni muhimu sana, kwa sababu mimi nazungumza na wewe kwa sasa. Na nina matumaini kuwa Wewe na mimi ni sehemu ya warithi/wasimamizi (MaKhalifa) wa sasa wa Kitabu “Qur’an”. In shaa Allah tuwe miongoni mwa wale Waliojaaliwa (Jaailoun) na Allah kuwa MaKhalifa.

Tujaaliwe kurithi, kukisimamia na daima kudumisha ufahamu wa kweli wa uelewa wa Qur'an. Insha Allah, sote tunaoyapitia haya hapa, kwa nia njema kabisa, tutakuwa pamoja katika jukumu hili, tutachukua na kulibeba jukumu hili kwa hiari zetu.

Hizo “jaailoun na Khalifa” ni kauli za mwanzo za kwenye hii aya. Hayo ni baadhi tu ya mambo mengi sana ambayo tutayagundua katika ayah hii, na itabidi tuyafanyie uchambuzi ((tafsil) ili tupate uelewa sahihi na wenye maana zaidi (meaningful).

.Mpaka hapo hatujajionea kuwa hakuna uhusiano wowote wa uumbaji wa mtu yeyote wa kwanza kwenye kipande hicho. Tumeona kuwa Allah (s.w.t.) anawaambia Malaika juu ya maandiko au Kitabu (Al-Ardh). Kwa hiyo, hili la maandiko (Ardh) ni jambo ambalo Mwenyezi Mungu amelitangaza kwa mara ya kwanza alipofunua maandiko (revelation) ya mwanzo kabisa.

Jambo muhimu ambalo tunapaswa kulielewa ni kuwa, neno “Khalifah” linatumika sehemu nyingi mbalimbali ndani ya Qur'an.

“Ikhtilaaf” yaani watu ambao wao kwa wao hawakubaliani (khitilafiana),

Khalifah au Khilfa au Khalafun na kadhalika, maneno yote haya yanamaanisha mabadiliko (alteration), ambayo kikundi baada ya kikundi baada ya kikundi hubadilika. Hili linafahamika sana na mabingwa wote wa lugha ya Kiarabu, haimaanishi kuwa ni makamu (viceroy) wala mfalme au mtawala wa vitu vya asili kama wanyama au mimea.

Allah (s.w.t.) anatueleza kama tulivyofafanua kua hayo ni maandiko (ardh). Na mpaka sasa hata maandiko haya ya Qur’an Allah ametueleza tangu mwanzo, kwamba ujumbe huu utakua na watu wenye kujali, wenye kustahili na wenye uwezo wa kutosha kuyabeba na kuyatunza maandiko haya, licha ya kupigwa vita kutokea kila upande, mwenyewe hujaalia Khalifa (makhalifa) apendavyo.

Na hata katika maandiko na vitabu vilivyotangulia na kupotea kulikua na makhalifa ambao sasa Allah anawaelezea kwenye Qur’an. Kama tunavyoona haya yapo mwanzo mwanzo mwa Suratul Baqara ya kwenye Qur’an. Allah anatufikishia mwongozo kuwa hata wewe au mimi tunaweza kuwa katika hao Makhalifa. Tuendelee.

Allah (s.w.t.) anawaelezea Malaika, wala hazungumzi nao, Allah kuongea na Malaika ni kuwapa amri tu na wao wanatii. Tunayaona hayo hata kwa viongozi wa nchi tu, tunaambiwa “Rais leo anaongea na wanajeshi wake” Lakini tukitazama na kusikiliza tunaona anayeongea ni Rais tu, wanajeshi wake wanasikiliza na kutii tu. hakuna maongezi, wanajeshi ni kupewa amri na kupokea kwenda kutimiza tu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hutoa malekezo na Amri. Mwenyezi Mungu hazungumzi wala hazungumzii kuwa anzungumza na Malaika.

Allah (s.w.t.) Yeye ni Muumba wa kila kitu, hana haja ya kushauriana na Malaika au mtu yeyote au kutoa mapema taarifa, kutuma telegram kuwa anataka kufanya hivi au vile.

Allah (s.w.t.) anatujulisha kwenye aya hiyo kuwa katika maandiko / Kitabu cha kwanza aliwaambia Malaika ambao hubeba ujumbe, maandiko hayo kuyawasilisha kwa watu. Allah (s.w.t.) daima huamrisha Malaika kwenda kuufiksha ujumbe kwa wasimamizi (Khalifa) wa maandiko / kitabu (ardh). Hayo ndiyo sehemu ya aya hiyo inatujulisha.

Pia sehemu ya aya hio inatujulisha...

... Itaendelea.
 
Kwa ufupi, mara nyingi ninapoulizwa kuhusu ndoto huwa najibu kwa ufupi kua hiyo ni elimu ya Nafs (saikolojia).

Mimi napendelea sana kufundisha kuhusu ndoto ili mwenye kuota awe anatafsiri mwenyewe. Sababu kuu ni kua; Binaadam kila siku tunaota na ndoto tunazoziota hutokana au husababishwa na mambo mengi sana. Ni vigumu sana kuyaelezea bila kutoa somo kamili kuhusu ndoto.

Tafadhali sana, nistahamilie nimalize kisa cha Adam, tutakuja kutoa somo la elimu ya ndoto kwa kadiri ya tujuavyo. Lakini kwa sasa elewa kua;

Ndoto ni moja ya uthibitisho kuwa kuna ulimwengu mwingine sambamba na huu tunaouona, kuusikia na kuuhisi kwa hisia zatu za uhai. Tukilala tunakua kwenye mfumo usio wa uhai, ambao huitwa "umauti". Usiogope, simaanishi kifo, ingawa kuna msemo usemao "kulala ni nusu ya kufa".

Kuna ulimwengu (realm) nyingine iliyo sambamba na sisi na hio ndio hubeba maono ya roho (spirits) zetu na za nyinginezo, nyingi tu.

Ndoto inaweza kua ni ujumbe wa kutoka kwa malaika, majini, qareen, vivuli, mashetani au hata nafsi zetu wenyewe.

Ndoto zako kwa ufupi zitazame kwa matamanio, maisha unayoishi, au unayoyafikiria daima, kwanini hivi kwanini sio vile.

Utanisamahe sana. Siwezi au siruhusiwi kutafsiri ndoto isipokua naruhusiwa kufundisha ili watu waweze kujitafsiria wenyewe ndoto zao. Ndoto zako zina viashiria vya matumaini.
Simba.
 
Habari zenu ndugu zangu?

Kwanza kabisa nitoe pongezi za dhati kwa mleta mada na wachangiaji wote kwa ujumla.

Kuna elimu kubwa iliyojificha wengi hatuifahamu vzr lakini kwa mapitio yanayowasilishwa tumejikuta mengi kati yao yanatuhusu kwa kiasi fulani,kama halijakugusa wewe basi kuna mtu unamfahamu anapitia haya hata kwa uchache.

Natanguliza samahani km nitakuwa nmetoka nje ya mada.
Mimi nina mke na tumefunga ndoa miezi 4 iliyopita, umri wetu ni 20's. Tangu tumeoana kumekuwa na changamoto ambazo nyingi kati ya hizo ni kwa mke wangu kupata maradhi ya mara kwa mara na ndoto za ajabu nyingine za vitisho nyingine za maelekezo(kama maono juu ya kitu fulani) kwa maelezo yake mke wangu anasema yeye ana walimu tangu alivyokuwa mdogo na alipofikisha umri fulani baba yake aliwafunga hao walimu kwa maana walikuwa wakimuonesha vitu ambavyo vipo juu ya umri wake(mfano kuona uchawi au kitu kibaya)

Natamani kumsaidia mke wng lakini ukweli mimi sifahamu chochote kuhusu hao walimu na sijui nianzie wapi maana nikimshauri mke wng twende kwa baba yake anakataa hataki hata kusikia.
Nahitaji msaada kwa yoyote atakaekuwa na uelewa wowote juu ya hili, mke wng ana asili ya tanga amechanganya kabila la msambaa na mgunya.

Samahani kama kutakuwa na uwasilishaji mbaya kwny uandishi mimi sio mzoefu wa kuchangia hoja hapa jamii forum.

Shukrani kwenu M/mungu awabaribiki nyinyi na vizazi vyenu.
 
Hapa huyu qareen anasimama kama kiumbe gani?
 
Arsis
 
Ushauri tu, kwanini wewe peke yako huongei na baba mkwe wako, pekeenu kiume (man to man) ?

Ni matumaini yangu utapata ufumbuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…