Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Ungemuuliza hao waislamu wanaleta majini wanayatoa wapi?
Ni kwamba sie tu
Ungemuuliza hao waislamu wanaleta majini wanayatoa wapi?
Story ni ndefu Ila kiufupi huwa kuna mambo huwa yanatokea ambayo nilishayasema au katika mazungumzo nasema kwa mtazamo wangu mbona hiki kitu or business naona haitakuwa au itakuwa tuendelee nayo or tusipoteze muda na inakuwa hivyo mara nyingi..
siko vizuri sana Kwenye mambo ya spiritual ndo akawa anasema itakuwa una majini..nikamwambia kama yapo basi ya kheri labda maana vitu vingi ni positive .
sasa ndo hapo alipoanza nyie waislam na majini mnausiana nayo hakuna wa kheri wala wa shari wote wabaya..
Anyway siyajui sana haya mambo so nilivyopata ile comment yako ndo nikamwonyesha..Akabaki anashangaa tu ..
 
Umefanya vizuri kumpa elimu.
 
Simba katuacha kwa muda tumpe udhuru. Ila nilikuwa napitia darsa ya sheikh Sayyid Kamal Al-Haidari, anatoa hoja kwa kuanza na hoja ya kisayansi, kuwa baina ya baba yetu Adam (A.S) na Mtume Muhammad (S.A.W) ni vizazi baina ya 30 mpaka 40 tu haizidi hapo, na kizazi baina ya Mtume na sisi si zaidi ya 40 pia, kiujumla ni vizazi 80 toka Adam mpaka hivi sasa, na inakadiriwa haifiki miaka 100 000 baina ya hapo, wengine wakikadiria ni miaka 6000 na wengine wakisema 60 000 tokea Adam aliyetajwa kwenye Qur an mpk hivi sasa. Sasa msingi wa hoja yake ni ushahidi wa uwepo wa mifupa ya binadamu inayokadiriwa kuwepo kwa miaka zaidi ya milioni 2 iliyopita, tena katika nchi yetu hii ya Tanzania hapo Olduvai Gorge. Hawa binadamu waliokuwepo mwanzo ni akina nani kama Adam (A.S) aliyetajwa alikuwepo kwa miaka isiyozidi 100k tu iliyopita?
 
nimejifunza mengi na naendelea kujifunza mengi kwako na kwa wachangiaji wengine .
naomba kuuliza Simba ..ukisema jini akipanda ni mbaya .lkn katika kisa hichi umesema..
Jin2 ..kama alikuwa anakwambia maneno ya kusema kumuuliza mzee Ally..ok so hapo si amepanda pia au kama ni utofauti naomba unifafanulie pia .
shukran
 
TTaf
Tafuta elim zaid uchache wa elim utafanya upotoshe watu.... Ila pia hongera maana sio haba unejitahid kutoa maelezo mazuri

Japo Kuna angle flan inabidi uongezeke zaidi
 
Nakusoma sana Dr Matola sababu umeegama ktk misingi(Foundatiom) labda wewe unaweza kuwa na uvumilivu ila wengine naona kabisa wameshapanic nachelea kuona wakitoka nje ya mada punde tu.


Nashauri tuendee na vionjo na darasa maridhawa la Adamu ni nan?
 
mIMI ATAKA KUJUA
MIMI NIGEPENDA KUJUA JINA LA KIJIJI HASA, NA KAMA BABU YAK YU HAI,NAKAMA ATARIDHIA KUMFUNDISHA MTU ELIMU HII. HII NI ELMU KAMA NYINGINE WAACHE WAJINGA HAPA, MUDA WA KUWA HUMDHURU MTU
 
Dni
Unajitoa fahamu?

Kuran ni kitabu cha uganga. Kwamba hujui.
Duniani kuna watu wajinga sana! Yaani alivyolishwa Kanisani hata hatumii kichwa chake! Hatuna hiyo katika Uislamu. Waislamu ni 'one of the freest thinking people in the world' Huwezi kuja na mafuta ya upako ukambambia Mwislamu ...
 
mIMI ATAKA KUJUA

MIMI NIGEPENDA KUJUA JINA LA KIJIJI HASA, NA KAMA BABU YAK YU HAI,NAKAMA ATARIDHIA KUMFUNDISHA MTU ELIMU HII. HII NI ELMU KAMA NYINGINE WAACHE WAJINGA HAPA, MUDA WA KUWA HUMDHURU MTU
Kwanza umekuwa mvivu kusoma, halafu unaita watu wajinga.
Kila kitu ulichouliza hapo, alishajibu humu.

Babu alishatangulia mbele za haki, kijiji kipo Tanga, nadhani alitaja kitu kama Maforoni, na picha ya bango ikawekwa
 
Hii Mada ingekuwa na kichwa cha habari kinacho sema.

"Mambo nilivyo yashuhudia baada ya kurithishwa uchawi na babu yangu"
 
mIMI ATAKA KUJUA

MIMI NIGEPENDA KUJUA JINA LA KIJIJI HASA, NA KAMA BABU YAK YU HAI,NAKAMA ATARIDHIA KUMFUNDISHA MTU ELIMU HII. HII NI ELMU KAMA NYINGINE WAACHE WAJINGA HAPA, MUDA WA KUWA HUMDHURU MTU
Mahandakini.

Babu yangu alitangulia mbele ya haki miaka mingi iliopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…