Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Ungemuuliza hao waislamu wanaleta majini wanayatoa wapi?
Ni kwamba sie tu
Ungemuuliza hao waislamu wanaleta majini wanayatoa wapi?
Story ni ndefu Ila kiufupi huwa kuna mambo huwa yanatokea ambayo nilishayasema au katika mazungumzo nasema kwa mtazamo wangu mbona hiki kitu or business naona haitakuwa au itakuwa tuendelee nayo or tusipoteze muda na inakuwa hivyo mara nyingi..
siko vizuri sana Kwenye mambo ya spiritual ndo akawa anasema itakuwa una majini..nikamwambia kama yapo basi ya kheri labda maana vitu vingi ni positive .
sasa ndo hapo alipoanza nyie waislam na majini mnausiana nayo hakuna wa kheri wala wa shari wote wabaya..
Anyway siyajui sana haya mambo so nilivyopata ile comment yako ndo nikamwonyesha..Akabaki anashangaa tu ..
 
Ni kwamba sie tu

Story ni ndefu Ila kiufupi huwa kuna mambo huwa yanatokea ambayo nilishayasema au katika mazungumzo nasema kwa mtazamo wangu mbona hiki kitu or business naona haitakuwa au itakuwa tuendelee nayo or tusipoteze muda na inakuwa hivyo mara nyingi..
siko vizuri sana Kwenye mambo ya spiritual ndo akawa anasema itakuwa una majini..nikamwambia kama yapo basi ya kheri labda maana vitu vingi ni positive .
sasa ndo hapo alipoanza nyie waislam na majini mnausiana nayo hakuna wa kheri wala wa shari wote wabaya..
Anyway siyajui sana haya mambo so nilivyopata ile comment yako ndo nikamwonyesha..Akabaki anashangaa tu ..
Umefanya vizuri kumpa elimu.
 
Simba katuacha kwa muda tumpe udhuru. Ila nilikuwa napitia darsa ya sheikh Sayyid Kamal Al-Haidari, anatoa hoja kwa kuanza na hoja ya kisayansi, kuwa baina ya baba yetu Adam (A.S) na Mtume Muhammad (S.A.W) ni vizazi baina ya 30 mpaka 40 tu haizidi hapo, na kizazi baina ya Mtume na sisi si zaidi ya 40 pia, kiujumla ni vizazi 80 toka Adam mpaka hivi sasa, na inakadiriwa haifiki miaka 100 000 baina ya hapo, wengine wakikadiria ni miaka 6000 na wengine wakisema 60 000 tokea Adam aliyetajwa kwenye Qur an mpk hivi sasa. Sasa msingi wa hoja yake ni ushahidi wa uwepo wa mifupa ya binadamu inayokadiriwa kuwepo kwa miaka zaidi ya milioni 2 iliyopita, tena katika nchi yetu hii ya Tanzania hapo Olduvai Gorge. Hawa binadamu waliokuwepo mwanzo ni akina nani kama Adam (A.S) aliyetajwa alikuwepo kwa miaka isiyozidi 100k tu iliyopita?
 
Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 1.

nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.


Baada ya kuongea na mshikjai nikampigia Babu. Baada ya kusalimiana.
Mimi; Babu umesikia kilichokuepo?
Babu; Kuhusu nini Simba nifahamishe.
Nikamuelez kama alivonambia Dokta.

Babu; Hilo nakifahamu, Sheikh...wa Unguja kanipigia jana, akanambia nikujulishe, nikaona saa hizi upo kazini, nilikua nangojabaada ya dhuhuri niku[igoie, Najua hua mnapumzika kidogo.
Mimi; kwa mwanao hapa kuna kupumzika, kama hujajiongeza mwenyewe, hata siku moja hasemi ka[pimzikeni.
Baba; Simba huyo, simba hawapumziki wawe wameshiba.
Mimi; Mwanao huyu saa zote ana njaa?
Babu: Muulize, mtajuana nae wenyewe, mbona mimi unanuliza?
Mimi; Mwanao huyu si unajua haongei ongei sana?
Babu; Simba, huyo achana nae wewe nenda ukapaone Pemba na Kojani ukaone huo mwaka koga wao wa Kojani, nasikia wanatoka dunia nzima siku hio, ha[patoshi. Kajonee huko, umekosa kuoa Unguja labda huko utapata, usinisahau lakini.
Mimi; Babu tunangea vitu serious wewe unaleta mambo ya kuoa?
Babu; hakuna itu seripous duniani kama kuoa, asikudanganye mtu, huyo wako mke ndagu, sasa tafuta asie ndugu. Pemba kuna mitotoya Kimanga huko, Wewe nenda tu babu...


Babu: Sikiliza Simba, wewe ukiweza leo hii nenda kwa Mzee Ali ukamsikilize, maana kishaambiwa bila wewe Dokta haendi, nenda ukamuone, kisha leo usiku nambie. Tena usimpigoie simu kama unakwenda, wewe mstukize tu. Si ulinambia pete uliitumia kujificha kwa mara ya kwanza Unguja?

Mimi; Ndio babu.
Babu; Sasa leo nenda kwake kama ulivyoingia kwa Bi S. Unguja akustukize upo ndani. Haya kwaheri Simba, usiache kwenda.

Akakata simu, nikawa nafanya kazi zangu lakini sina raha kabisa, baada ya kusa alasiri tu nikwamuaga Mzee.

Mzee; Babu yako kakwambia nini, umeongea nae?

Nikamweleza Mzee yote.

Mzee; Sawa, wewe nedna mradi babu yako kakwambia hivyo usitie shaka, na mimi nikitika hapa 11 nakuja huko moja kwa moja, Wewe fanaya mambo yako lakini usiningoje mimi.

Mimi; Nikatoka nikaomba dua ya safari nikaanza.

Njiani nikawa nafikiria ntaiweka wapi gari pale na parking mpaka lifunguliwe geti, likanijia wazo, kuna Kituo cha mafuta pale Buguruni naweza kuweka gari, kuna jamaa fundi pale, gari zake zote hizi za za kisasa tunamtengenezea kwetu.

Kufika, kweli nikamkuta, nikamwambia mimi naingia Buguruni pale nikamwelekeza hakuna parking mtaa ule, akanambia mitaa nuksi kweli ile chukua boda mwanagu, wacha gari yako hapa au nikupe pikipiki utaendesha mwenyewe? Nikamwambia hapana boda tu anatosha.

Nikaenda na boda mpaka karibu ya kufika nikamwambia hapahapa, nimefika. Ngapi mshikaji? Akanambia fundi pale kanambia nisichukue pesa kwako, nikampa buku mbili, nikamwabia basi hii kunywa soda mwanangu. Akanambia hapa Buku tu. Nikamwabia ubani wako huo mwana, usiwe na shaka. Akaondoka zake.

Kufika nyumba moja kabla ya Mzee Ali sikutazama hata kama kuna watu au hakuna, nikaigeuza pete nikaiminya, nikaingilia mlango wa uani kama tulivyoingizwa siku ile noikauta kina mama na kina dada wamekaa hawana habari kabisa, nikaenda moja kwa moja chumba chake cha kutibu watu, kuna watu wa pale pale kwake walikua wamekaa nje mlangoni kama kawaida.

Nikakaa kama dakika tatu nikaona hakuna anaekuja, nikatoka nikatazama tazama uani, wapo watu na shughuli zao kama mwanzo, hakuna hata anaeniona. Nikaingia mlango wa uani wa kuingilia nyumba kubwa, nikasikia Mzee Ali anaongea na mtu zaidi ya mmoja lakini kwenye chumba sio kule ukumbini kwake.

Nikatime mlango nikaona umefungwa, nikiufungua itakua noma.

Nikaenda ukumbini kwake nikakaa peke yangu mara nikasikia mlango umefunguliwa nikasoge wakawa wanatoka ndani, kumbe walikua watu watatu na yeye Mzee Ali, wawili wanaume mmoja mwanamke.

Mzee Ali; Sasa wewe mama na mumeo subirini kule ukumbini tulipokaa kwanza mke wangu lazima akupe nguo za mapambano mupe kama nusu saa mjje. Mimi na huyu bwana tunakwenda, kazi yake huyu ndogo tu. Nikawapita nikaenda chumba chake cha uganga nikawapita wale qa mlangoni, hakuna alieniona wala kustuka kabisa, nikaingia ndani nikakaa nikaiachia pete. Nikamsikia mzee Ali uwani anampa maelekezo mkewe kuhusu yule mwanamke na huku chumbani kwake aletewe ndoo za maji.

Nilikua nimekaa kiti anachokaa yeye, sijui kwanini niliamua hivyo. Cha ajabu nilikua sina uoga wala kuwaza matokeo ya kitendo changu. Mara namsikia mzee Ali mlangoni anamkaribisha mgeni wake karibu bwana karibu.

Akatangulia Mzee Ali kuingia hakuniona au hakutengenmea sielewi, ghafla aageukia mlangoni, karibu, karibu bwana yule mgeni alioingi tu macho yake na yangu, akapiga Salamu alekum, nikaitika Alekum Salam, na mzee Ali ndio anageuka ananiona, nikamuona kama kanitole macho, mdomo kawacha wazi, akapiga kelele kama yowe hivi halafu akaruka juu mara ya kwanza, karuka mara ya pili akapiga samasolti kwa mbele, mpaka nikashangaa, mtu mzima na ana mwili kidogo lakini kapiga samasalti, alipofikia akakaa chini, akatoa macho, akaanza kutazama chumba kizima akawa kama kapigwa ganzi, yule jamaa aliekuja naenkasimama karibu ya ukuta macho na kijasho chembembamba kina mtoka, hajui kinachoendelea.

Mzee Ali; Salaam, salaam salaam. Nimekuja kwa amani, nilikua nategemea utakuja lakini sio kimya kimya. Akamgeukia mgeni wake, kaa chini, huyu mhgeni wangu pia.

Mgeni; Au niwapishe?
Mimi; Kaa chini, hakuna siri inayotoka nje ya chumba hiki.
Mzee Ali; kaa bwana kaa.

Nakajua alikuwa sio yeye kwanza anaepiga samasamasolti, sasa ni yeye anaongea.
Mzee Ali; Bwan Simba, hali yako bwana?
Mimi; Sisi salama, wewe tu?
Mzee Ali; Nyie watotohapoo nje, hebu njooni haraka.

Hosi hodi. Mzee Ali piteni, ile kuingia tu.
Mzee Ali; kwanini anakuja mgeni hamnambii mnamkaribisha humu ndani peke yake?
Mabinti: Hakuna megni aliyekuja Baba.
Mimi; Mzee Ali, hawakuniona hao, hii habari yetu haiwahusu hao, waache wakafanye yao.
Mzee Ali; haya nendeni. Bwana Simba mbina umenistuwa, leo mpaka kaja mwenyewe hapa. Habari kubwa hii. Haya nambie bwana Simba.
Mimi: Mzee Ali unasema ulikua uanjua kua nitakuja, haya nambie wewe.

Mzee Ali; Bwana mgeni tafadhali katungoje pale ukumbini tuna mazungumzo ya faragha kidogo na bwana Simba hapa. Samahani sana.

Nikaona yule mgeni kama kashukuru kutoka nje. Akatoka nje.
Mzzee Ali alikua kasimama.
Mzee Ali; Nikae chini mkuu?
Mimi; kaa tu, usiwe na hofu, wala usiwalumu wanao au yeyote yule hakuna alieniona nikiingia, mimi nilikua na nyinyi toka kule mlipokaa na wale wengine, si umewaambia atakwenda mkeo kumpa yule dada nguo za mampano? Nakueleza hayo ili ujue kua nilikua na nyinyi. Sasa sema ukweli wako, uwe ukweli mtupu.

Mzee Ali; kama kashikwa kigugumizi cha mbali, Sikiliza Simba, mimi niliambiwa utakuja lakini sikujua kama utakuja ghafla hivi, nilijua utakuja Dokta akiwepo hapa ili tuongee na wewe habari ya safari.

Mimi: Ongea yote, Mzee Aliaua nikuulize ujibu maswali?
Mzee SAli; Itakua vozuri maana sijui yepi ya kuongea yepi sio ya kuongea.
Mimi: Hii safari ilikua ya Dokta tu, kwanini sasa iwe na yangu?
Mzee Ali; Nilipata maelekezo kwa huyu Mkuu aliekuja hapa sasa hivi, hakukaa lakini kaondoka haraka, kanambia niyamalize haraka na niseme ukweli mtupu, kama ulivyonambia wewe.
Mimi; Nataka kujua kama nilivyokuuliza, tafadhali kila unavyochelewa unazidi kuwachelewesha wageni zako.

Mzee Ali; Mimi ndio mkubwa wa shughuli inayofanyika nyumbani, ilikua niende na dokta poeke yake, lakini nimeletewa habari kua kuna watu wetu aliokua nao Dokta tunamtazama hali yake, wameshikwa wote na hakuna njia ya kuwawachiwa walioshikwa mpaka tukamuombe msamaha mbele ya wakubwa kojani na wewe tukuombe usaidie ili watu wetu wapoatikane.
Mimi; Wangaoi watu wenu?
Walioshikwa ni site lakini na wanaopokezana nao kumi na mbili nao hawajashikwa wapo nyumbani lakini wamezuliwa kufanya kazi yoyote si kwa Dokta si kwengine. Wakubwa wakajua kwanza ni Vibuki, vibuki sisi tunaviweza, lakini imeonekana hii nguvu kubwa inatokea kwako na haiwezekani kuwakatali, tutasambaratishwa Kojani nzima. Huo ndio ujumbe nilioletewa, kwa hio ilikua ukija nikuombe twende wote Kpojani.
Mimi; Bado hujasema ukweli, wakubw azako wamekwambia uniombe mimi twende kojani?

Mzee Ali; Hapoana Bwana Simba, hilo nasema mimi, wao wamenambia utakuwepo Kojani nikukaribishe kwa salama na amani na wamenambia ukija hapa nikukaribishw kwa salama na amani.
Mimi; Sasa kwanini wewe umetaka nifatane na wewe Kojani?
Mzee Ali; Nimewaz hio ndio itakuwa wepesi maana nimesisitizwa asikose Dokta kwenda, hivi kabla ya hao wageni kuja nilikua naongea Dokta namsisitiza kuja, lakini Sheikh kamwambia asije huku kwangu bila wewe, ndio nikajua mtakuja niwaombe twende sote.

Mzee Ali; Wanataka ukaombe msamaha wa nini kwa Dokgta huko Kojani?
Mzee Ali; Yamenikuta, hayasemeki lakini nabidi niyatapike.
Mimi: kama unavyotapisha kiuongo? Hapa ukisema uongo Dokta haji na unajua ndio utakua mwisho wako wa kukaa Dar?
Mzee Ali: Simba, nisamehe sana, ngoja nikwambi ukweli Mkuu. Mimi natafuta rizki tu, yale mambo ya kuwatapisha watu ni kujongezea kipato tu.

Mimi; Sikukuuliza hayo yote, jibu nililokuuliza, nilikupa fursa ya kuongea mwenyewe ukawa huongei, sasa nakwambia, kama hujajibu swali ninalokuuliza, urafiki wetu unaishia hapa na ujua hato jini yeyote kukusaidia utapeli wako, na wala hakua takaepandisha jini hapa kwako.
Mee Ali; Hilo nimeliona, hata yule mwanamke ilikua apandishe hukohuko tulikokua nae nikaona ajabu leo hajapandisha, ndio nikasema nimuhamishie huku.
Mimi: kama hujajibu swali, hatopandisha na utakua huna ujanja, si unaona hata huyo mkuu wenu kaja kakimbia kuniona mimi hapa?
Mzee Ali; Nisamehe, naanza kukujibu. Mi nilikua nakwenda kumuomba msamaha kwa uongoniliomfanyia. Na nimemrishewa nipiga hesabu ya pesa zote nilizochukua akarudishiwe mbele ya wakuu huko na wewe niliambiwa utakuwepo huko, nikuobe msamaha pia kwa kufanay uongo mbele yako na babako.
Mimi; Kwanini unamtaka Dokta aje hapa?
Mzee Ali; Ili nihakikishe anakuja Kojani, tukawatoe hai wanaonisaidia kazi niwarudishe kwao nipewe wengine.
Mimi; Kwanini hujawarudisha hapa ulipompachika nao?
Mzee Ali; Imeshindikana bwana Simba, mpoakawakubwa wamejaribu kuwarudisha kule imeshindaka, hata hawaonekani kabis, hatujui walipo lakini tunajua nguvu sako ndio zimewazuia.
Mimi; Nani kakwambia hivyo?
Mzee Ali; Huyu aliekuja akaondoka hapa, na yeye anaambiwa na wakubwa ake.
Mimi; Mwambia aje.
Mzee Ali; Huyu bwana akija anapirika nyingi sana, si umeona alivyokuja kwanza?
Mimi; Usiogope, mwambie aje, au nimwambie mimi?

Nikamngoja kama dakika tatu.
mzee Ali; Namwabia lakinihaji kabisa, sio kawaida yake. hua nikimwita tu anakuja, hachukui hata nusu dakika.
Mimi; haya tulia, mimi nimeshamwita anakuja, na hafanyi fujo yoyote leo.

Mzee kama akatingishika kidogo tu.
Mzee Ali Salaam, Salaam Salaam, nimekuja mkuu kama ulivyoniita niko chini ya amri yako.
Mimi; Anakusikia huyu?
Mzee Ali; Ndiyo ananisikia.

Mimi: Haya mwambie kinachoendelea na nini kinatakiwa kifanyike haraka sana, au wewe na yeye unajua kitakachowapata. Ilikua kama sauti ya Jini 2 inanambia niseme nini.

Mzee Ali; Sikiliza kiti, huyu Simba ni mkubwa wa wakubwa zetu sisi na wote wanamuheshimu sana na hawataki hata kuwaza vita na ukoo wake na marafiki zake. Kw ahio Ali, umkatie tiketi ya ndege huyu na Daktari ya kwenda na kurudi Pemba, wiku moja kabla ys shughuli kubwa na siku moja baada ya shughuli kubwa, bila hivyo itakua fedheha kubwa Kojani, sherhr haitofanyika kabisa.

Mpigie yule mteja wako anafanyua kiwanja ya ndeh)ge, anajua namna ya kutaka tiketi na namna atavyowapa hawa. Wewe kama utamlipa yule au humlipi mtajuana nae yule. Hii haina mjadala. Wamesema wnajua wenyewe pakufikia na wanajua wenyewe watfika vipi Kojani, wewe wape tiketi zao tu leo hii, zowe na tarehe ya kwenda na kuondoka, ukikosea shauri lako.

Mzee Ali; Kunalingine Mkuu Simba?
Mimi' Ndio, nataka heshima na adabau kuanzia leo, wewe na wakubwa zako na huyu mjinga wenu mfahamisheni. Akikuita tena uje kama kawaida yako usichelewe. Mengine, sisis gtunajua tuongee vipi na wakubwa zako bila kupitia kwa huyu mwizi mwenzako.
Mzee Ali; Nimekuelewa mkuu, naomba niondoke.
Mimi ; Haya kwaheri.

Hakuna cha samasolti wala nini.

Mzee Ali; Samahani Simba, naomba niagize naji a kunywa.

Mimi; Agiza, harakanataka kuondoka.
Mzee Ali; Nyiiie Mabinti leyteni maji chupa mbili haraka.

Mabingti wakaleta maji Mzed Ali wakanywa na mimi nikafungua nikanywa, kuonesha ustaarabu. Mzee akayagida chupa nzima.

Mzee Ali; Nashukuru yameisha salama, Sasa bwana simba kwanza naanza kukuomba msmaha hapahapa mradi mmeongea na hawa wakuu, mimi nikutimiza tu, sasa hizi napigia simu yule binti afanye tiketi, naoimba nimpe namba yako akitaka majina au maelezo mengine. Wewe mpe maelezo yote, leo huyajui majina ta Dokta? yake nayajua yote mpaka la mamake. Yako bwana Simba ndio sina. Nikamwabia haya andika jina langu kamili, Wee binti njoo uandike haraka, akaja binti mmoja mkubwa mkubwa hivi Haya andik, nikampa tena majina, yule binti akawa anayaandika kwenye simu yake.

Mimi; Haya mimi naondoka akiwa gtayari na tiketi ndio anijulishe, leo hii hii baada ya lisaa limoja asinitafute kabla.

Mzee Ali; Sawa bwana Simba, ahsante sana tutawasiliana.
Mimi; Usiwasiliane na mimi wala Dokta kuanzia leo, wasiliana na yule mwizi mmwenzio, nimeshamwambi aje ukimwita. Huamini?

Mzee Ali; hapana, Bwana Simba nimesema kimazowea tu.

Nikanyayuka huyo nikatoka, nikajua wambea walikua wansikiliza mlangoni, na mkewe kakaa nao. Nikatoa Salaam nikaitikiwa na wote mbio mbio. Nikatoka langi uani, kutoka tu nje nikatazama kushoto nikaona Gari ya Mzee, nikawa sina haja ya kuminya pete nikaifata gari, nikaona yupo ndani na mshikaji.

Majini ya Kojani, Pemba 2
Majini ya Kojani, Pemba 3
Majini ya Kojani, Pemba 4
Majini ya Kojani, Pemba 5
Majini ya Kojani, Pemba 6
Majini ya Kojani, Pemba 7
Majini ya Kojani, Pemba 8
Majini ya Kojani, Pemba 9
Majini ya Kojani, Pemba 10
Majini ya Kojani, Pemba 11
Majini ya Kojani, Pemba 12
nimejifunza mengi na naendelea kujifunza mengi kwako na kwa wachangiaji wengine .
naomba kuuliza Simba ..ukisema jini akipanda ni mbaya .lkn katika kisa hichi umesema..
Jin2 ..kama alikuwa anakwambia maneno ya kusema kumuuliza mzee Ally..ok so hapo si amepanda pia au kama ni utofauti naomba unifafanulie pia .
shukran
 
TTaf
Yap iko hivyo unakuwa uko protected na hivyo viumbe. Kuhusu kutibia hapo it depends una tawaliwa na majini wa race ipi na wana itikadi ipi ya kiimani kama race yao ni weusi watataka utibie kwa mitishamba and if race yao ni wazungu waarabu or wachina watataka utibie kwa culture zao ,mfano ukiwa na majini ya kizungu ambayo yana fuata itikadi za kikristo wata kutaka uponye watu kwa kutumia neno la mungu Refer kina mwamposa and the likes it's the same pia endapo kama majini hayo yatakuwa na itikadi za kiislam yatakutaka utibie watu kwa kutumia mifumo ya kiislam 😆😆😆 Mambo ndio yapo hivyo lakini wachungaji na mashekhe hawasemi ukweli 😆😆😆 wanaponya watu kwa nguvu za majini na mizimu then wana brain wash watu kuwa ni kwajina la yesu au allah
Tafuta elim zaid uchache wa elim utafanya upotoshe watu.... Ila pia hongera maana sio haba unejitahid kutoa maelezo mazuri

Japo Kuna angle flan inabidi uongezeke zaidi
 
Uislamu unaweza kusimama wenyewe bila kufanya comparison yoyote na Ukristo.

Waislamu na Quran inasema hakuna Mungu isipokuwa Allah na hana mshirika.

Lakini Ukristo na Biblia inaamini Mungu alimuumba binadamu kwa mfano wake na Ukristo unaamini katika utatu mtakatifu.

Hapo usitegemee hizi imani mbili kuelewana kimisimamo wakati zinatofautiana katika msingi mkuu.
Nakusoma sana Dr Matola sababu umeegama ktk misingi(Foundatiom) labda wewe unaweza kuwa na uvumilivu ila wengine naona kabisa wameshapanic nachelea kuona wakitoka nje ya mada punde tu.


Nashauri tuendee na vionjo na darasa maridhawa la Adamu ni nan?
 
mIMI ATAKA KUJUA
Inatokea post namba 43.


Usiku huo ulikua hauna matukio yoyote, nililala usingizi mnono kabisa, isipokua niliamka alfajiri sana, kutoka kwenye ndoto iliokua ndefu kidogo.

Wakati najitayarisdha kuamka sawa sawa, nikasikia kwa nje sauti ya babu "hodi, hodi, hodi bwana mkubwa bado umelala? Amka tusali bwana. Fanya haraka bibi yako kanipa kahawa na visheti nikuletee".

Nikaamka nikiwa fresh kabisa, usingizi ulikua umenitosha kabisa na zaidi. Kutoka nje nikamsalimia babu nikaenda kwenye mto nikatawadha nikarudi, njiani nikakutana na mwanafunzi wa babu na yeye kishaamshwa na babu.

Babu akanambia kunywa kahawa wakati tunamsubiri mwenzako arudi tusali. Akanitilia kikombe cha kahawa, akanambia kuna visheti pia, nikamwambia visheti baadae babu, tukisha sali. Mwanafunzi aliporudi akakimu sala, tukasali pamoja.

Tulipomaliza kusali, tukatia kikombe cha kahawa tukaanza kunywa na visheti. Kimya kimya, baada ya kama dakika kumi, mwanafunzi wa babu akaaga, akasema atarudi baada ya muda si mrefu.

Alipoondoka tu, babu akaniuliza, vipi umelalaje pangoni? Nikamwambia nimelala hata sijijui kabisa. Babu akacheka. Nikaendelea, isipokua babu nimeota ndoto moja siielewi elewi, sasa hivi ndio inanijia kichwani. Babu akasema, kama unaweza nielezee ndoto yako. Nikaanza kumuelezea.

Nimeota kuna mtu kaja, lakini sura yake siikumbuki, anasema yeye kaja kwa ajili yangu. Yeye anafanya kazi na wewe babu kwa miaka mingi sana, na mimi inabidi nianze kuijua hiyo kazi kupitia kwako na yeye atakua ananisaidia katika hio kazi. Hapo babu sijamuelewa kazi ipi, kabla sijamuuliza ikawa nimeamka.

Babu akacheka, akasema "si nilikwambia wewe ndio mrithi wangu?". Nikamwambia, babu mimi nirithishe mali zako, kazi zako mimi siziwezi. Babu akacheka, akasema mali nikiondoka kabla ya wanangu watarithi wanangu, wacha tamaa. Nikacheka. Babu akaendelea, akanambia kazi zangu ni nyepesi sana Bwana Mkubwa, wewe unachotakiwa kufanya, akija mtu ana shida yake yoyote usithubutu kumwambia hapana au hujui. Usichokijua chochote niulize mimi. Kuanzia ukiondoka hapa wenye matatizo wataanza kukufata, usiwatoe njiani hata siku moja. Wewe wasikilize, nipigie simu, na yule aliekuja ni ruhani wangu, ana akili sana na anajua mambo mengi sana. Saa zingine atakutatulia matatizo ya watu bila wewe kunambia mimi. Lakini yatakujia mambo madogo madogo tu, yale makubwa mpaka ufikie miaka 35 mpaka 45 babu, usiogope. Mpaka wakati huo utakua umeshazowea.

Babu akaendelea, kama umemsikia na umekumbuka ina maana ushafunguka wewe. Huna haja ya kukaa hapa muda mrefu, tutatimiza ada ya siku chache kabisa za kukaa, nazo ni siku tatu. Lakini siku zijazo mwenyewe utataka uje pangoni hapa, utakua na mambo mengi ya kufanya. Leo usijitie dawa yoyote, kakoge maji ya chumvi halafu kakoge maji ya mtoni, ukimaliza njoo tumalizie kahawa.

Nikaenda nikaogelea baharini, nikakuta kuna kama watu watano wapo baharini wanaogelea kwa mbali kidogo na mimi, lakini nikaona wao hawajavua nguo, wapo maji yanawafika tumboni. Sikuwatazama sana nikatoka baharini nikaenda mtoni, nikakoga maji ya mto. Kamba walikua wamejaa tena wameshakua wakubwa wengine, nikatoka.

Nikamwambia babu, kamba naona wamekua wakubwa tayari, akanamabia, hao wa kuanzia kesho babu, kesho kwenye dimbwi lile kubwa hakuna pakukanyaga. Ndio msimu umeanza, kesho ndio watakua kamba wazuri. Tena mbele huko kuna wale wakubwa kabisa, nao kesho wataanza kuvunwa kwa wingi. Babu akaniuliza hujakutana na watu wanavuna kamba huko? Nikamwambia sijakutana na mtu babu isipokua nimeona watu wanaogelea baharini lakini kama wamesimama tu maji yameishia tumboni. Babu akacheka, akanambia wewe macho yashagfunguka hayo. Hao hata mimi niliwaona nilipokua nakuletea kahawa. Babu sasa utayoyaona usiogope, utaona mambo na viumbe vingi ambavyo kwa macho ya kawaida huwezi kuviona. Wale uliowana sio watu, wale ni viumbe vingine kabisa wamekuja kwa umbo la binadam tu.

Nikacheka, nikamwambia babu, mambo yenu nyinyi wazee, ya kiajabu ajabu tu. Babu akanmbaia yashakua yako sasa, usiogope tu. Lakini usiwe na wasi wasi bwana mkubwa, wewe una kinga zote kuanzia utotoni, hii tunakufanyia kama ada tu, wewe ulikua huna sababu ya kuja kama sio ada kukuleta.

Babu akaag, akaondoka zake, ile anaondoka tu akaja yule mwanafunzi wake, kumbe hajaenda mbali alikua anangoja babu aondoke tutu arudi. Kukaa kidogo akaja na yle mwingine na kapu lina chupa ya chai, akasema leo bibi yako kaanza kukupikia kuanzia usiku, kuna mikate ya sinia humu na rosti la kamba. Nikamwambia, lete, maana najisikia njaa, kweli, tukaanza kula weote pale. Bibi yangu alikua anasifika kwa kupika. Wale vijana wakasema wewe usiondoke mapema huku tufaidi vyakula vya bibi yako. Huwa anavifaidi babu yako tu ukiwa haupo, sisi hatuvioni. Nikacheka.


Itaendelea.
Simba.
MIMI NIGEPENDA KUJUA JINA LA KIJIJI HASA, NA KAMA BABU YAK YU HAI,NAKAMA ATARIDHIA KUMFUNDISHA MTU ELIMU HII. HII NI ELMU KAMA NYINGINE WAACHE WAJINGA HAPA, MUDA WA KUWA HUMDHURU MTU
 
Dni
Unajitoa fahamu?

Kuran ni kitabu cha uganga. Kwamba hujui.
Duniani kuna watu wajinga sana! Yaani alivyolishwa Kanisani hata hatumii kichwa chake! Hatuna hiyo katika Uislamu. Waislamu ni 'one of the freest thinking people in the world' Huwezi kuja na mafuta ya upako ukambambia Mwislamu ...
 
mIMI ATAKA KUJUA

MIMI NIGEPENDA KUJUA JINA LA KIJIJI HASA, NA KAMA BABU YAK YU HAI,NAKAMA ATARIDHIA KUMFUNDISHA MTU ELIMU HII. HII NI ELMU KAMA NYINGINE WAACHE WAJINGA HAPA, MUDA WA KUWA HUMDHURU MTU
Kwanza umekuwa mvivu kusoma, halafu unaita watu wajinga.
Kila kitu ulichouliza hapo, alishajibu humu.

Babu alishatangulia mbele za haki, kijiji kipo Tanga, nadhani alitaja kitu kama Maforoni, na picha ya bango ikawekwa
 
Hii Mada ingekuwa na kichwa cha habari kinacho sema.

"Mambo nilivyo yashuhudia baada ya kurithishwa uchawi na babu yangu"
 
mIMI ATAKA KUJUA

MIMI NIGEPENDA KUJUA JINA LA KIJIJI HASA, NA KAMA BABU YAK YU HAI,NAKAMA ATARIDHIA KUMFUNDISHA MTU ELIMU HII. HII NI ELMU KAMA NYINGINE WAACHE WAJINGA HAPA, MUDA WA KUWA HUMDHURU MTU
Mahandakini.

Babu yangu alitangulia mbele ya haki miaka mingi iliopita.
 
Back
Top Bottom