Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

ila we mzee una dharau wewe 😢
 
Nimekuelewa, sana, Waislam pia tunaamini Issa (Yesu) ni Kristo, hilo neno Kristo Kiarabu chake ni "Masih", mdiyo maana sisi tunamwita Masih, unafahamu kwanini ni "Kristo", Kristo ni neno la Kigiriki, kama ambavyo hajawahi kusikia neno "Yesu" akiitwa "Meshikha" alipokuwa duniani na ndivyo hajawahi kusikia neno "Kristo. Kiarami (Aramaic ambayo ndiyo lugha ya mama'ke Issa. Kiarabu na Masih na Kiswahili ni Masihi.

Kuhusu kuwa Qur'an ni maneno ya Allah hilo sina shaka nalo na upo sahihi. Qur'an yenyewe inasema": 4:82. Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu (contradictions) nyingi 82.

Utaona Qur'an yenyewe licha ya vingine, imejiwekea kigezo kizito sana cha khitilafu "contradictions".

Vipi Biblia, imejiwekea kigezo hicho au kingine chochote?
 
😂😂 usichanganyikiwe boss ndio maarifa hayo

Ila naamini kama ulivyosema katika dunia saba alizosema arsis naona anaongelea mbingu saba,na ya sita na saba amesema hana mamlaka nazo.kabisa kuzizungumzia,anyw way,,ngoja tumsome kikubwa vyovyote itakavyokuwa baki na tauwhid juu ya Allah
 
Biblia haijawahi kuwazungumzia Majini katika hali ya kufanya wema.
Bali kutumika katika hali ya uovu tu. Uchawi, uaguzi, urozi nk.
Kama Maandiko mengi yanavyotuambia likiwemo Hilo.

Kama Qurani inawatambua baadhi yao kuwa ni wema basi ni kwa mujibu wa Qurani na sio Biblia na Ukristo.

Hivyo tubaki kuamini hivyo.

Ukristo unawatambua Majini ni viumbe vilivyo katika utawala wa giza chini ya Kiongozi wao Ibirisi Mkuu Lucifer.
Kumbuka hata Ibirisi aliumbwa ili kumwabudu Mungu, na sina taarifa kama naye ana dini kwa sasa.
Nadhani umeelewa hapo.
 
Boss, ndiyo maana nikasema kama huna elimu na jambo haimaanishi kwamba halipo hilo jambo

Kifungu hapo ulichoandika hakikupinga uwepo wa majini,bali kimekataza kutoa sadaka kwa majini ambao wanafanya uasherati na mwanadamu si ndio?

Kwa maana kwamba hao ndio waovu au mashetani,sasa kama hivyo ndivyo inaamanisha kwamba kuna wengine ambao ni kinyume na hao ambao wanamambo yao

Anyway boss,tuyaache kama yalivyo

Asante
 
Ibilisi yeye alishahukumiwa kwenda motoni toka enzi hizo kwasababu ya majivuno na kiburi kwa mola wale

Ila ibilisi ameomba apewe umri mrefu mpaka karibia kiama,,ingawa yeye ni jamii ya majini pia

Kwahiyo hukumu ya ibilisi na majini wengine jamii yake ni tofauti kabisa

Sasa hapa ndo nimekupata vizur,tofauti yangu na wewe inakuja kwenye elimu tu

Asante
 
W We jamaa mgumu sana kuielewa.

Wema wa Majini unaongelewa katika Qurani na sio katika Biblia.

Na hakuna Nabii wa Wakristo aliye ongelea wema wa Majini bali uovu wao tu.

Kwahiyo unataka tukuamini wewe sasa sio.

Majini wema waache waabudu kwa mujibu wa Qurani.

Usichoelewa hapo ninini ?

Inawezekana Uislamu ndio Dini ya kweli Hadi Majini yakaamua kuwa Waislamu.
 
Boss,unateseka ukiwa wapi kwani?

Relux bwana,narudia tena kama kitu huna elimu nacho haimaanishi kuwa hakipo

Binafsi sikujua kama watu walikuwa wanatoa sadaka kwa majini mpaka pale ulipo leta wewe andiko,je ningebisha isingemaanisha kuwa hawakutoa sadaka kwa majini

The same to you now,unabisha kwakuwa huna elimu hiyo au hukupata kusikia biblia inasema hivyo

Asante
 
Mimi elimu ya Majini itanisaidia nini ndugu?

Sijawàhi kuwaona popote pale na wala siwajui.

Mimi nafuata mafundisho ya Yesu Kristo ndugu.

Elimu ya Majini Baki nayo wewe Mwislamu mwenzao.

Imani yangu ni kusikia Neno la kristo tu.
Warumi (Rom) 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
 
Huwa sipendi porojo boss

Asante
 
Naomba kujua arsis na ramdiyin walifahamiana vp
 
mimi kwa mambo niliyopata kuyashuhudia nikajisemea sisi binadamu wachanga sana wa ujuzi wa mambo
na zaidi toka hapo nikaamini uchawi na mambo mazito yasiyo ya kibinadamu yana exist. hua nawaona wanaosema hakuna uchawi kama watu wasiojua lolote katika dunia. dunia ni na ulimwengu shikamoo 🙌🏿
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…